Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Swala la KUONGEA kirefu katika KUFIKISHA ujumbe MFUPI!

>> Sunday, January 18, 2009

Karibu mara zote UJUMBE ni mfupi ingawa kuna wasifiwao kwa kuongea kirefu!

Binadamu alivyokuwa mvivu, angekuwa mahiri wa lugha kila atakalo kusema lingekuwa na UREFU wa herufi moja.

Na labda....
.....ninajieleza kirefu kwa sababu NINAJARIBU kujieleza na si MTAALAMU WA KUELEZEA.

Na....
......Unabahati kama bado kuna wasikilizao kila neno lako katika hadithi YAKO ndefu yenye ujumbe CHEMBE MOJA, hasa kutokana na ujuavyo kupigisha tikitaka maneno na sentensi, katika kumkwaza hata Sista wa Kikatoliki kuanza kufikiria labda ngono NI muhimu au Padre wa Kipagani kuanza kufikiria labda ni kweli ulawiti ni dhambi na sio tabia mbaya tu isiyo na uhusiano na dini ya WAHESHIMIWA wenye dini.

Swali:

  • Katika hadithi yangu ndefu kwani ni nani anafikiri nafikisha hata ujumbe mmoja?
Na.....
.....Katika kufikisha ujumbe kuwa jamaa limekaa vibaya kuna walioimba wimbo wenye maneno;.....
''DUKA LA MZUNGU liwazi. LAUZA mchele na NAZI.Kaniona mimi kafunga.......''


Na labda....
.....kama neno moja lingetosha kuelezea KUNYA tusingetakiwa kuleta maneno mengi yaharibuyo ustaarabu wa SIMULIZI za HAJA KUBWA uwezao kudakwa kwa neno moja lisomekalo au kutamkwa; ''KUNYA''

Na labda pia,....
.....ingawa binadamu wanasifiwa kwa kujua kuongea mpaka KICHINA, tukumbuke mpaka SISIMIZI wanajua kufikisha ujumbe KWA MPENZI SISIMIZI kuwa wapi kuna chakula-kibonge cha sukari na kuhakikisha TAIFA LA SISIMIZI halikumbwi na janga la njaa kama liwakumbavyo BINADAMU wenye maneno KEDEKEDE , WAVIVUUU, halafu wanasikia njaa haraka.


Lakini....
......Ongea tu KIREFU kama inalipa au inakusaidia kutonuka MDOMO.
Swali:
  • Si unasikilizwa?
NAACHA!



Ngojea tena Martin Luther King Jr ajaribu kufikisha ujumbe kwa kumuongelea Malcom X....




Au tu Rick James azungumzie ya COLD Blooded....





Pata baadhi ya picha zangu na wadau tuliokuwepo maeneo juzi ya jana...ASANTENI WOTE!
Photobucket


Photobucket


Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP