Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

JINSI ya kuendelea KUMPENDA MWANAMKE aliyeota NDEVU!

>> Friday, May 29, 2009

Penzi kiboko mpaka unaweza kuanza kulisingizia vitu!

Likinoga unalisingizia mpaka utamu lisionalo , likiingia uchachu mpaka saizi ya chuchu inakuwa ishu.:-(

Na mara nyingi kikuvutiacho kwa mtu sio kidevu ndio maana husiti ukipewa chansi gizani kuendelea kumpapasa umpendaye bila kumuona vizuri .Na ukipapasa labda hubobei kwenye kidevu.

Na haki ya nani tena, wakati unamtumbulia macho mpenzi, kama unampenda bado huoni kila kitu ingawa yuko mbele yako!:-(


Ndio!
Mapenzi sehemu nyingi hufanyika gizani au kwa kuyafumbia macho.
Na kama wewe unaweza kufanyapenzi huku unastukia utandu wa buibui kwenye silingibodi , basi ufanyalo sio penzi.

Narudia!
Mapenzi sehemu nyingi hufanyika gizani ndio maana mara zote UNAHITAJI MWANGA ili umjue MTU kabla HUJAMTEMA a.k.a KUMUACHA SOLEMBA!

Nachojaribu kusema ni; DAIMA PENZI HUNOGA ukiwa GIZANI na ukianza KUJUAJUA SANA kwa kuwa uko MWANGANI , kwa wengi hilo ndio misingi ya mwisho wa PENZI au kutonogewa na penzi kama juzi.
Swali:

  • AU?
Sikatai!
Labda utadai kuwa kwa kumjua sana mpenzi ndio msingi imara wa penzi.
Na labda ni kweli kama unaoanisha tafsiri ya PENZI na KUISHI PAMOJA bila MAKEKE na Limtu.

Ndio !
Nakubali kuwa kuna ukweli kuwa kuna aina nyingi ya mapenzi na labda moja ya tafsiri ya penzi ni hiyo yako na unasaidiwa na kutaka kujua kila kitu au kustukia mpaka NDEVU.

Sikufichi!

Inawezekana DEMU wako ana nywele za kutosha tu kifuani a.k.a LAVU GADENI , na sababu za WEYE kutojua hicho kama ni kweli hujifanyi hujui ni kwa sababu YEYE mwenyewe zinamkwaza kwa hiyo anazinyoa ndio kisa hajastukia mpaka leo mapenzi yako ya nywelenywele hata za kiboxi manyoya.

Swali:

  • Hivi unakumbuka binadamu ana nywele mwili mzima ndio maana limtu lako linatoka jasho mwili mzima na ukilipa chansi lanuka kikwapa?

Turudi kwenye Mwanamke Mwenye ndevu....

Naweza kusema,...
....UKIPENDA umependa na umpendaye akiwa na ndevu hizo ndevu kwako za mpendeza.
Swali:
  • Au?
  • Kwani UTU na UKE kwako havitoshi?

Kumbuka ,..
....KAMA WEWE nimtafutaji wa KASORO kila MTU ANA KASORO ingawa katika kasoro ;NDEVU SI KASORO!


Swali:
  • AU?

NIMEACHA wazo na samahani kama nimekukwaza na kumbuka HILI ni moja tu ya wazo!
Nakutakia WIKIENDI KIBONGE na kama unapumzika nakutakia MAPUMZIKO JEMADARI!


Tupumzike tena kwa kujifunza kunyoa sehemu sehemu kwa msaada wa Gillette..


Au turudi tu South Africa tupate Dikgomo REMIX..

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

mumyhery 6:31 pm  

mhu kazi kweli kweli

Mzee wa Changamoto 8:40 pm  
This comment has been removed by the author.
Mzee wa Changamoto 8:42 pm  

Hili si wazo bali ni busara. Si mtazamo bali ni maono. Kwani penzi ni nini? Na kwanini watu hawatalakiani kabla hawajuana? Yawezekana hakuna kujuana katika mapenzi na sitoshangaa kama kuna ukweli katika hili. Si wanasema kuwa penzi ni mbingu nyingine? Aijuaye mbingu ni nani? Ukweli ni mzuri lakini ni mzuri unapotumika panapohitajika. Labda wampenda umpendaye kwa kuwa anayajua mapenzi lakini ukweli ni kwamba hujui kayajulia wapi mapenzio. Akikupa list ya waliomfunza utaendelea kumpenda? Lakini si kakwambia ukweli? Ni sawa na ukweli wa kuacha manyoya ya "bustani ya mapenzi" ambayo yanaweza kumkimbiza mpenzi.
Dawa niaminiyo ni kuyatafsiri mapenzi kulingana na umpendaye. Yaani kwangu mimi nampenda mtu aliye kama mke wangu na kwa kuwa najua hakuna anayeweza kuwa kama yeye exactly, basi ntakuwa naye pekee?
Swali:
Au?
Tuendelee....
Wewe penda mkeo ama mumeo awe kama upendavyo maana unasahau kuwa unapenda awe hivyo kwa kuwa ulishapenda alivyo fulani na kama atashindwa kuwa kama upendavyo basi utampenda aliye kama upendavyo.
Swali:
Unampenda fulani? Ama unataka wako awe kwa namna fulani? Athari zake ni kuwa na fulani fulani na huko kutakupotezea huyo udhaniaye kuwa ni wako.
Sijakukwaza, si ndio? Kumbuka Kaka Simon kaweka tatizo, labda namna nilionavyo ndio tatizo.
Blessings

Yasinta Ngonyani 7:08 pm  

:-(

Simon Kitururu 10:42 am  

Asanteni wote!:-(

Simon Kitururu 6:51 am  

@Mzee wa Changamoto:

Kwa sababu fulani nimerudia mara kadhaa kukusoma ulichoandika:-(

Mzee wa Changamoto 5:22 am  

Hivi FULANI ni nini? Lol
Asante kwa kurudia mkuu. Pamoja Daima

Simon Kitururu 5:01 pm  

@Mzee wa Changamoto: Fulani ni kisingizio

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP