Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Woga wa ukubwa wa NANIHII!

>> Friday, May 29, 2009

Nasikia kuna waogopao kubwa!

Labda ni kweli KUBWA inatisha ingawa pia kubwa inaweza kupwaya!:-(

Saikoloji ya muogopa makubwa hutegemea kwa muogopaji dogo ni nini.

Ukubwa wa jambo KWAKO unategemea na UBONGO wako ulivyojengeka ili kustukia MADOGO ni nini.
Na kwa kawaida unaujenga mwenyewe UBONGO KUSTUKIA MAMBO ingawa pia MAZINGIRA na JAMII inamsaada mkubwa katika kukuponza kwa hilo.

Na sababu za kuhofia kwa kuwa unahisi ni kubwa basi itauma au kukushinda ni jambo lako ULILOJIFUNZA tu!

Na kumbuka,...
.... chochote ujifunzacho kinafundishika kukiacha.

Swali:

  • Unafikiri wakati umezaliwa ni vingapi vilikuwa vikubwa kwako na hukuviogopa kwa kuwa mtoto mwenye umbo dogo na vimekuzidi kimo?
  • Unafikiri ni kwanini kwa kukua na woga wako wa makubwa umekua?
  • Unafikiri makubwa ni yapi ikiwa ukweli ya yako makubwa kwa mwingine ni madogo?


Na ,...
....tunajifunza ukubwa wa mambo hata kwa kusikiliza tu wadaio yaliwaumiza.

Lakini katika mchezo wakuumiza labda na wewe ni muumizaji ndio maana mara kwa mara kuna mambo unayastukia kabla hujaumizwana sio kwa kuwa ni marudio ya maumivu.

Kumbuka tu,..
... TAFSIRI ya ukubwa wa jambo kwako labda kwa mwingine ndio saizi yake na inatosha kabisaaa!

Kumbuka tu,..
... LABDA ukubwa wa jambo kwa MWIZI ni kichekesho kwa JAMBAZI, ingawa duniani hapa kati ya wezi na majambazi waliotajirika zaidi ni wezi .

Swali:
  • Hujastukia wanasiasa wako uliowapigia kura?

Na USISAHAU,...
.... Udhaniapo ni UDOGO wa jambo ndivyo UMUUAO MWENZIO ambaye kwake SWALA ni kubwa na halina udogo kama tu maumivu USIVYOJUA ukubwa wa maumivu ya mkeo kujifungua au ya mjusi kutoa mimba.

Swali:

  • AU?

NIMEACHA!
Ngojea Rolling Stone wanipe- Satisfaction


Au tu Akon na Michael Jackson warudie-Wanna be Startin' Somethin'

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP