Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

STAREHE ya kutumia MUDA BINAFSI kuhukumu WENGINE na maisha yao BINAFSI!

>> Monday, January 25, 2010

Ni kweli,...
... kunyoshewa vidole hainogi kama KUNYOSHEA wengine vidole hasa kama kilengwacho ni KASORO.


Na kunyoshea wengine vidole KUHUSU MAMBO YAO BINAFSI inasaidia sana kupunguza muda WA mtu kujichunguza mwenyewe BINAFSi hasa kama lengo ni kukwepa kujistukia zako KASORO.


Na mtu asipokuwa muangalifu anaweza akafikiri kutambua kasoro ni kitu rahisi mpaka itakapotokea AKAFIKIRIA na kustukia ukiwadadisi watu utagundua karibu kila kitu ukionacho hakina kasoro kuna AMBAO wanakikosoa kwa KASORO.:-(

Na haki ya nani uonacho kina kasoro kama tu MATEGE,...
.... kuna apendaye MTU kisa matege mpaka KWENYE ndoto zake za kikubwa za MCHANA ofisini WAKATI YUKO MACHO, ndoto zile za uasherati za kuombea siku moja afanikiwe kupata nafasi ya kufanya dhambi ya uzinzi na MTU mwenye bomba la matege ambaye atamsalimisha kutoka kwa wanaomfuatafuata KATIKA MAISHA HALISIA wenye miguuu imenyoka kama fito za kujengea kigenge cha kuuzia nyanya na vitunguu MIKESE,- na ni miguu iliyonyoka NDIO kitu ambacho kwake ndio KASORO.:-(

Swali:

  • Unafikiri kama mtu ana BONGE la pua kubwa kiuwiano na SURA YAKE imsaidiayo kupumua vizuri na kudaka harufu bwelele NZURI au tu za chooni, huyo anakasoro ya pua au ni yule mwenye pua UJAZO wa kawaida AMBAYO HAINUSI VIZURI na inazingua upumuaji , na ambayo inasababisha astukiwe ZAIDI kwa masikio kama Rais Obama ndio mwenye KASORO ya PUA?
  • Hufikiri KASORO kwa asilimia kubwa ambazo SI UGONJWA zilalamikiwazo ni za KUBUNI kwa aliyenacho ndio maana mwenye aibu kwa midomo minene hushangaa watu wakilipia kujazwa midomo ili LIPS zijazie tako?

Ndio,....
.... kuna watumiao nyenzo ya KUHUKUMU WENGINE katika kuepusha wengine kuwachunguza yao yaliyojaa KASORO.

Na kwa bahati mbaya au NZURI, kwa ung'eng'e wanadai `` IT WORKS!´´,...
... kuhukumu wengine KWA KIPINDI KIFUPI inasaidia sana kukwepa KUJIHUKUMU wewe MWENYEWE.
Swali:
  • Wakati unahukumu wengine si unakumbuka kama kuna lako lihitajilo hukumu wala haliondoki na liko tu lakusubiri?
  • Je, umefanikiwa kuhukumu mtu leo na kusahau kujichunguza yako yenye KASORO kwa muda leo?
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu Aaliyah abadili hali ya hewa kwa kurudia- One in a Million

Au tu Aaliyah adai -Age ain't nothing but number

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP