Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Udhaifu wa KUONA kabla ya KUPAPASA,....

>> Wednesday, January 27, 2010

.....kwa mwenye macho hapa DUNIANI ,....
..... ni bonge la udhaifu uponzao WENGI na ambao umesababisha mengi ikiwa pamoja na ya ;....
  • Ubaguzi wa rangi
  • Baadhi ya embe dodo zisitomaswetomaswe
  • Watu kuogopa giza na kuchagua kuwa nguvu za giza ni za shetani na za Mwanga niza MUNGU
......au tu hata Maimuna kupendewa kwa ujazo wa TITI badala ya roho yake nzuri.:-(




Na unaweza kubisha, lakini KUONA pamoja na mazuri yake yote hapa DUNIANI,...
.... huleta udhaifu wa KUSIKILIZA na KUJISIKILIZA, kitu kisababishacho waonao wengi kusahau mapungufu ya wakionacho hasa kimtazamo wa muda mrefu KISA WAMEKIONA , na wamejiaminisha HICHO kitu kwa sasa NI kidude kizuri.:-(

Swali:

  • AU?

Na udhaifu wa `` KUONA KABLA´´ uathirivyo ,....
... usipoangalia waweza kukufanya ujiaminishe mwenyewe kuwa EMBE DODO ni TAMU kisa MUONEKANO WAKE na kusahau kuwa KUONA EMBE DODO na hata KULITOMASATOMASA embe dodo bado sio kipimo kizuri cha utamu WA EMBE DODO kwa kuwa ni LADHA ambayo huhitaji embedodo LIONJWE kwanza ndio kithibitisho cha UTAMU kipatikane,.....
..... na hapo ni kama hatufikirii MANUFAA YA EMBE DODO ni virutubisho vyake na wala sio muonekano WAKE , ..
....na wala sio hata ule wake UTAMU.:-(

Swali:

  • AU?


Na kuna UDHAIFU WA KUSIKIA kabla ya KUONA.

Udhaifu HUO wa kusikia kwanza pamoja na mazuri yake yote DUNIANI,...
... huweza kuathiri kwa ;...

  • Kudhoofisha makali ya kushuhudia kwako
  • Kukuandaa woga
  • Kukufanya udhani unajua ukweli kuwa Rais Mkapa Fisadi
  • kukuandaa kuamini Maimuna havai chupi

....au tu kunaweza kukusababisha upende MTU au tu SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA kabla ya KUTHIBITISHA MTU HUYO au TARALILA HIYO ana/ina mbivu zipendekazo KWA VITENDO kwako.:-(


Ndio ,...
...sikatai kuwa ``UKISIKIA kabla ´´ unaweza kustukia ni nani KIRUKA NJIA au tu KIBAKA,....
..... au tu KUJIANDAA tu na UCHOCHORO kisa umesikia kuna majangili hapo,..
... au tu kuna MBUYU wenye majini kwa hiyo usipige teke vifuu,....

... na kwa hilo nasikia kuna wapatao faraja.



Na ,....
.. sikatai kuwa nasikia kuna wapatao faraja za ``KUSIKIA KABLA ´´ wengi ambao wanasaidia sana dunia hii iwe kama ilivyo KWA BAADHI YA MAZURI YAKE kwa kuwa tu WAMESIKIA BILA KUONA na sasa hivi WANAJIANDAA tu na;...
  • kwenda MBINGUNI walikokusikia tu
  • kutofanya UASHERATI kwa kuwa wamesikia ya UKIMWI
  • kuwa wafuasi wa siasa za CCM na kufanya TANZANIA tulivu
  • kuwafanya waogope GIZA na kufanya usiku uwe mtulivu

....ila tusisahau tu kuwa moja ya UDHAIFU wa ``KUSIKIA kabla´´ ya kushuhudia ni kwamba faraja yake iko tu katika UWAZO(imagination) UBONGONI mwa mwenye kusikia tu bila kushuhudia kitu ambacho kirahisi husababisha;...
  • WATU kuhukumu watu kwa kusikia tu
  • Watu kuhukumu vitu kwa kusikia tu
... na WAKATI hali halisi ni kwamba wala VITU, Simon Kitururu, au tu Kadala binti ya Kadoda haviko/hawako hivyo.:-(



Swali:
  • Si inasemekana kuna waliosikia tu na kudhani ULAYA bomba kweli na mambo yake ni mswano sana tu?

  • SI kunawasikiao tu na kung'ang'ania ni kweli fulani Malaya?
  • Hivi unafikiri VIPOFU wa macho HAWAONI?


Ndio,...
...pamoja na yote mazuri,...
...KUNA UDHAIFU utokanao na ``KUONA kabla ya KUPAPASA´´ na ``KUSIKIA kabla ya KUONA na KUPAPASA´´,....

  • ... kwa hiyo UKIONA, - kumbuka KITU kina zaidi ya UONACHO na kwahiyo hata kama ni lako LIMCHUMBA lionekanalo NONO kimuonekano, ukiingia kichwakichwa labda lina UKIMWI na kwa hiyo ni vizuri ujue kabisa unalipenda LIMCHUMBA na umelipenda na MDUDU WAKE ili penzi lako lililo sababishwa na KUONA tu MBIVU inaelea, linoge na kusaidiwa kudumu kwa vitendo pia KWA KUWA unalijua LIMCHUMBA kwa zaidi ya lionekanavyo LIMCHUMBA.

  • ...kwa hiyo UKISIKIA kabla ya KUONA kumbuka KITU kama tu GIZA liogopwalo, si lazima ni kweli GIZA linatisha hivyo ukikumbuka hasa isemekanavyo na ISHUHUDIWAVYO na mpaka NA watoto wengi wazuri uwaonao MTAANI ambao WENGI WAO walitengenezwa na wazazi wao vizuri GIZANI kwa kitendo kilichoenda shwari tu gizani na kwahiyo tu kumbuka aliyeoanisha GIZA na vitu vibaya si lazima aaminike kwa kumsikia tu kwa kuwa MABAYA mengi hufanyika kwenye MWANGA na kwahiyo labda nguvu za shetani ni NGUVU za MWANGA na wala sio NGUVU za GIZA.




Swali:


  • Au?
NI WAZO TU HILI MKUU na NIMEACHA!

Tubadili kwa kwenda MALAWI kwa Lucius Banda alete - Tina


Au twende tu na MOZAMBIQUE ninmuache mwanamuziki mwingine aliye uawa Afrika Kusini na waliotaka kumuibia gari miaka michache iliyopita kwa jina GITO

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 7:32 pm  

Wapo wanaosahau kuwa wanapapasa walichoona na utashi wa kupapasa unatoka na kuona ama kutoona (hivyo kutumia mpapaso kujua kilichopo).
Labda kuona hutufanya tuamue kutoona kingine. Na pengine nguvu ya kuona tusichotaka kuona ndiyo inayotufanya tuamini hatuoni. Lakini
Hivi wengi hawajui kuwa wanatenda mengi mabaya kwa kuona kabla hawajawaza na kisha kunena halafu kutenda?
Kwani mwanzo wa mengi ni nini?
Kaona, katamani, kanena kisha kapewa jibu. Labda hakufanya yaliyofuata lakini kwa kuona na kutamani si katenda DAMBI YA KUTAMANI?
Labda "twadogosha" nguvu ya kuona na twaitumia kuamua pa kuanzia kujifanya tumeona.
Lakini kuna nguvu ya ziada ya maono hasa kabla hujaamua kuwaza na kupelekea kunena na kutenda.
Zao la hayo yafuatayo ni zao la KUONA.
Sijui naeleweka?
Naacha
Tuonane NEXT IJAYO

Baraka Mfunguo 6:26 am  

Hapo ni wazi kwamba binadamu tumeumbwa kwa hisia na wakati mwingine hutawala maamuzi yetu. Kwa nini mtu achukue hatua ya kujiua kisa mapenzi ama amehisi amesalitiwa? HISIA.

Kwa nini watu wengine husisimka wasikiapo manukato ya aina fulani yapulizwayo na Mwanamke? HISIA

Kwa nini wakati mwingine waweza kuona kitu ama ukiguswa unasisimka? HISIA

WOW! SINA MENGI

Yasinta Ngonyani 11:15 am  

ninakuu"...kwa hiyo UKISIKIA kabla KUONA kumbuka KITU kama tu GIZA liogopwalo si lazima ni kweli GIZA linatisha hivyo ukikumbuka hasa isemekanavyo watoto wengi wazuri uwaonao walitengenezwa na wazazi wao GIZANI kwa kitendo kilichoenda shwari tu gizani na kwahiyo tu kumbuka aliyeoanisha GIZA na vitu vibaya si lazima aaminike kwa kumsikia tu kwa kuwa MABAYA mengi hufanyika kwenye MWANGA na kwahiyo labda nguvu za shetani ni NGUVU za MWANGA na wala sio NGUVU za GIZA." mwisho wa kunukuu. Hapa, maandishi haya nimeyapenda na nimejifunza kitu.

Simon Kitururu 8:57 pm  

@Mzee wa Changamoto: Unaeleweka Mkuu!
@Mkuu Baraka Mfunguo: Kweli usemacho!
@Dada Yasinta: Asante kama umepata kitu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP