Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Leo JUMATATU kama siku ya kufikiria KAMA ulidanganya vizuri JUMAPILI uliyoipita!

>> Monday, March 22, 2010

Labda waongo wazuri LEO,...
....ni wakumbukao walidanganya nini siku za JANA zilizopita.

Na labda mwenye AKILI ambaye anadanganya mtu LEO,...
....katika kusaidia kufanya uongo wake udumu vizuri anatakiwa kukumbuka ADANGANYACHO LEO na baada ya kumaliza kudanganya ADANGANYACHO LEO kuKIkumbuka ALICHODANGANYA LEO SIKU ZIJAZO  kama anataka uongo huo WA LEO ubakie na sura ileile na asiugeuze kuwa NI UKWELI siku zijazo kwa BAADA YA KUDANGANYA   kuchukulia alichodanganya KAMA NI kitu kilichopita.



Swali:
  • Unakumbuka mwaka jana muda kama huu ulijidanganya nini ambacho kinaathiri kitu maishani mwako ambacho kimaisha KAMA HUJIKUMBUSHI KUWA hicho ULIJIDANGANYA hutaweza kukipita?

  • Kwani hujui KUDANGANYA vizuri kudumuko ni kazi ya WENYE akili wakumbukao kuoanisha uongo wao wa leo na ULE wa siku zilizopita?
  • Unakumbuka labda leo kunakitu umedanganya  na unakichukulia kitendo hicho kama kitu kilichopita?
Ndio,...
... labda KUSEMA KWELI  hurahisisha mambo kama nia na madhumuni ya MTU ni kujulikana MKWELI,...
... na kama UNADANGANYA lakini ukiwa na lengo lilelile la kuonekana MKWELI  wahitaji kutumia akili vizuri LABDA ZAIDI YA MSEMA KWELI  na pia jaribu kutosahau  uhusiano wa ya leo na ULIYODANGANYA yaliyopita.:-(


NIMEACHA !
Kumbuka hili ni wazo tu MHESHIMIWA ambaye angalau katika KUTONGOZA hudanganya mtu!:-(

Hebu kwa kuwa leo ni JUMATATU tujikumbushe JUMAPILI kwa kuwasikiliza Maroon 5 wakiongelea-SUNDAY MORNING

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP