Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tukiangalia UTU kwa kuangalia MAANDALIZI ya MSICHANA siku ajuayo KWA MARA YA KWANZA anakwenda kumvulia MTU ampendaye NGUO!:-(

>> Thursday, September 23, 2010

[Tahadhari: Taralila inawazo dhaifu na ukilichungulia labda limekaa vibaya.:-(]

Maandalizi yoyote, yanayo na  kwasababu
Siku ya kutoa yote, ukurutu si adabu
Kwa kuwa si kivyovyote, mtu huenda kwa babu
Andalizi la kuvua, ni silika tu ya utu.


Andao la msichana, kama funzo la silika
Na silika za msichana, UBINADAMU hakika
Za uchafu kuukana, hata usio hakika
Za BINADAMU za UTU , jifunze kwa MSICHANA.


Ya uvulana ya UTU , si kama ya kisichana
Yale yenye utukutu, mbele za watu mchana
Ya kukojolea vitu,mbele hata ya Anna
Hata soni haioni,na hilo si ni bayana?


Utajifunza tu KITU, kwa kufikiria UTU
Na uchi katika MTU, wengi ni KIPIMA utu.
Ya msichana ni UTU, hata yafichavyo KITU
Pasipo ya MSICHANA, ya MVULANA si kitu.






Swali:
  • Unafikiri kila kitu kingekuwa KINAFANYWA kwa maandalizi kama ya siku ya kwanza wajua labda NANIHII inaweza KUNANILIWA -Tanzania kimaandalizi ya kutawala DUNIA unadhani tungekuwa wapi?

  • Unauhakika andalizi la kukutana na mpenzi wako mara ya kwanza kwa nia ya kufanya dhambi ya asili aka UASHERATI hayana mchecheto kiasi kwamba kwa kujiandaa sana kuvaa ambavyo utamvulia mtu ukasahau KUSAFISHA nyumba, kula au kuwa uendacho kufanya ni DHAMBI Kikristo au  KIISLAMU ingawa labda sio dhambi kibaolojia?











Ainisho la taralila:

Ndio,....
...UKIFIKIRIA unaweza kugundua  shughuli za MAANDALIZI  ni tofauti  siku  unuiapo na kujua kesho,....
..... utakwenda KUMSUTA Khadija au tu utafanya wa muhimu  MTIHANI .

Na kujua ya kesho kibinadamu ni kawaida kwa kuwa labda leo umeshajua kuwa utasikia njaa tena kesho ,....
.... kwa hiyo labda MAANDALI ya kama  kesho utakula tena ni maandalizi tofauti kidogo na umeyazoea tokea uzaliwe  na kwa hayo  HUJIHAMI.


Ila,...
... kumbuka tu  KATIKA SWALA HILOHILO LA MSOSI kama itakuwa ni kweli kwako KWA MARA YA kwanza  utakula KONOKONO wa kuchemshwa KESHO,...
.. na kwenu konokono hamjawahikusikia ni chakula ,waweza kujikuta unajiandaa vizuri katika zoezi zima la kukabiliana na HILO BONGE la msosi kwa wastaarabu WAFARANSA  hasa kama lengo ni kujifanya sio mshamba kwa wastaarabu WAFARANSA katika yako ya KUJIHAMI.:-(

Swali:
  • AU?

Ndio,...
... nakubali HII HOJA  ya maandalizi ya MSICHANA siku ya kwanza aliyoamua kuwa leo atamvulia mtu/MVULANA   mpaka kificha eneo ANUAI angeiandika tu vizuri zaidi MSICHANA ambaye kashapitia hilo ndani ya safari ndefu za mpaka NATAKA -SITAKI, Baba MKALI, unajua hii ni dhambi ila nakupenda,....nk.

.... ila baada ya kusimuliwa na MOJA ya hawahawa FLOWERS aka MSICHANAZ jinsi maandalizi ya siku hiyo muhimu yaliyonuwiwa kwa hiari yawezavyo kuwa na shughuli tofauti kabisa KIMAANDALIZI na zenye umakini wa hali ya juu,....
....nikapata MOTISHA wa leo kujiaanda sana katika shughuli zangu kwa kuwa ghafla nikajistukia labda KILA SIKU ikiandaliwa kwa umakini ina nafasi kubwa ya mafanikio zaidi hata ikiwa fanikio lenyewe  kwa KIKISTO ni dhambi ,...
....na Kwa KI BUDHA si dhambi ila BUDHA anafanya lifikiriwe zaidi bila VITISHO.:-(


Swali:
  • Si unakumbuka lakini inasemekana wasichana wengi hata baada ya kujiandaa sana kwa shughuli nzima ya uasherati wa mara ya kwanza , BAADA YA shughuli huwa hawawi na uhakika kama maandalizi yalilipa kwa  kuwa bado hubakia na hisia labda SHUGHULI haikufanywa kwa maringo yenye UFANISI wenye kiwango cha kutosha?
  • Hivi MHESHIMIWA,  hivi LILE halikufanyi ufikirie na HILI?


Ni moja tu ya WAZO MHESHIMIWA na wala usijihangaishe sana kulielewa kama HUKULIELEWA!:-(

Moja kwa moja katika kubadili mkao hapa kijiweni  Trombone SHORTY aachie-Somethin' Beautiful




Bilal arudie-Soul SISTA


Au tu Method Man na D'angelo wamalizie tu kwa-Break ups 2 make ups

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:14 pm  

nanukuu "Tukiangalia UTU kwa kuangalia MAANDALIZI ya MSICHANA siku ajuayo KWA MARA YA KWANZA anakwenda kumvulia MTU ampendaye NGUO!:-(" Duh! mtakatifu Simon hapa kazi ipo!!

emu-three 12:58 pm  

Maandalizi ni sifa ya utukufu, hata `kamvulana kanavyohangaika siku akikubaliwa kuwa kamsichana kana kuja, anahaha kiasi kwamba hata kuku akidonoa mlangoni kwa bahati mbaya atasema
'karibu mpenzi'
Swali: Hivi msichana akimvulia nguo mvulana wake kwa mara ya kwanza, huyo mvulana atakuwa kavaa, na huyoo mvulana itakuwa mara yake ya kwanza kuchungulia nyeti za wasichana?

o'Wambura Ng'wanambiti! 3:59 pm  

Emu-Three! Mmmh!

Ila mkuu hii imekaa viabaya ile mbaya...lol!

Fadhy Mtanga 11:37 pm  

Mtakatifu ya leo kubwa kuliko tena taralila imesindikizwa na mashairi.

mkuu hivi leo umewaza nini? nashindwa kufahamu niseme nini.

Simon Kitururu 8:30 am  

@Da Yasinta: Mmmh!:-(
@emu-three: Swali gumu hilo.:-(
@Kadinali Chacha: :-)
@Askofu Fadhy: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP