Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuna mambo kama DINI na MAPENZI labda MSHINDI ni yule asiyetumia AKILI!:-(

>> Tuesday, November 30, 2010

Na labda ni KWELI,....
....kama mtu anatumia sana AKILI kupenda MTU,.....
.....afanyacho ni MAHESABU na wala sio KUPENDA.



Na ukifuatilia dini ,.....
....utastukia kuwa misingi yake ni IMANI ZAIDI kuliko uhalisia na ukweli wa dini,.....
.....kitu kifanyacho kila mtu aamini DINI yake ndio ya KWELI na za wengine KUNAKITU ZIMEPUNGUKIWA  kwa kuwa ,......

....labda ukweli wenyewe UKITUMIA AKILI ZA MKICHWA KIBINADAMU kinachoongelewa na DINI hakieleweki.:-(



Swali:

  • SI umestukia kila mtu hufagilia DINI YAKE zaidi kuwa ndio ipelekayo watu JEHANAMU ukikosea jinsi ya kuifuata?

  • Na si ushawahi kustukia KAMA UMEPENDA VIZURI MTU kwa kawaida wewe utakuwa hunajibu zuri lielewekalo kuwa ni KWANINI katika watu wote LIMPENZI lako KIBOGOYO kwake ndio umejifia?


Ndio,....
.....kuna mambo KUTUMIA AKILI ndio chanzo cha MATATIZO,......
....kwa kuwa usingetumia AKILI labda wala usingejua HAPA duniani umepungukiwa nini .:-(

Na kwa kutumia AKILI SANA katika kuingia undani sana wa DINI YAKO,......
....waweza kujikuta ndio wazidi KUJICHANGANYA uelewa wako wa HIYOHIYO dini,.....
....kitu kiwezacho kufanya AAMINIYE TU bila uchunguzi mwingi wa kitabu cha DINI ndiye ajisikiaye kuwa na uhakika sana kuna MBINGUNI na yeye huko atakwenda angalau kunywa mataputapu kisa hapa duniani apendacho sana zaidi ya GONGO wakati anasikiliza nyimbo za dini ni MATAPUTAPU.:-(


NI wazo tu hili MTAALAMU!
SIKU NJEMA MHESHIMIWA!



Hebu Coco Mbassi adinye - O Bi





Douleur aingie tu na- Nyouma Nyouma



Au tu na Ndedi Dibango amalizie tu na -Eyo Mè

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory 5:42 pm  

Uelewa tu hapa mkuu, wala darasa halihitajiki kwa mtizamo wangu.

Simon Kitururu 3:27 am  

@Mkuu Malkiory: Ila tatizo kwa wengi kwa kuwa tu wavivu kufikiri,... UELEWA umegeuka BIDHAA adimu.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP