Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

DEMOKRASIA ya nchi kama TANZANIA haitakomaa kamwe bila WAPIGAKURA wake KUELIMIKA!

>> Thursday, February 24, 2011

Haiwezi kuwa ni DEMOKRASIA kamili kama WAPIGA KURA ambao ni watu muhimu katika DEMOKRASIA hawaelewi wayapigiayo kura KIUNDANI - kisa katika yazungumzwayo na WAGOMBEA KURA kwao hayaeleweki kisa katika hayo HAWAJAELIMIKA .

Huwezi kuwa na WAPIGA KURA ambao hawajaelimika na KUJUA waambiwayo katika KAMPENI za uchaguzi na WAGOMBEA nafasi za UONGOZI kuwa ni POROJO au LA - na kuamini una viongozi halali wakati tunajua kuna wapiga kura vigezo vyao vyakupigia mtu kura ni MSOSI kwenye makampeni, kanga na mashati ndivyo vilivyoamua nani apigiwe kura na sio SERA ZA  mgombeaji zenye manufaa hasa kutokana na kuwa na jamii ya wapiga kura ambao hawajaelimika.



Na itaendelea kuwa ni DEMOKRASIA YA BANDIA TANZANIA kama habari sahihi ziwezazo kufumbua watu macho zitakuwa ni miliki ya watu wachache na hazitapatikana mpaka vijijini kwenye shina ambako kuna WAPIGA KURA wengi na kufanya wajue UKWELI - wajue ukweli wa ni nini kinaendelea katika nchi yao ili waweze kuwa wapiga kura waelewao ni kwanini wanapiga kura huku maamuzi yao yakitawaliwa na habari sahihi na sio porojo tu za KAMPENI za WALIOZOEA KUDANGANYA  ambao wanajua wapiga kura hawajui kwa kuwa hawajapata  bahati ya kuelimika.


Na UPINZANI ambao ni changamoto , mchango wake utakuwa ni hafifu kama hautachangia kalika KUELIMISHA JAMII hasa kwa kushindwa kuwa na misingi ya kufikia watu mpaka kwenye shina a.k.a grassroot vijijini kuelimisha watu misimamo yao na kufunza watu haki zao za kuanzia ni nini HAKI ZAO mpaka ni nini wategemee kutoka kwa viongozi wao na serikali yao kwa kutobahatishabahatisha kwa kuhakikisha  wanahabari sahihi -WAMEELIMIKA.


Na labda tunahitaji somo la URAIA mashuleni kupewa kipaumbele hasa kama litachangiwa kwa mtazamo usio wa CHAMA TAWALA tu bali pia na UPINZANI  -bila kusahau vita hii ya kusambaza elimu ya WATANZANIA kuhusu mambo yahusuyo nchi yao yasiruke njia zozote ziwezekanazo kutumika kuelimisha WAPIGA KURA kuanzia kwa njia ya mdomo kwa mdomo, REDIO, magazeti na njia yoyote ile iwezekanayo kuelimisha JAMII ili angalau tuwe na WAPIGA KURA wanaojua wanalofanya  na sio wanapiga kura tu kutokana na SHAMRASHAMRA za kufuata mikumbo  na jazba  wakati asili ya kwanini wanafuata mkumbo ni ukweli kuwa kuna jambo hawajui kwa kuwa HAWAJAELIMIKA!:-(.


Nawaza tu kwa sauti!:-(







Hebu Christopher Tin aingilie kati akiwa na SOWETO GOSPEL CHOIR na kurudia wimbo - Baba Yetu

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory 12:50 am  

Kitururu, naunga mkono uchambuzi wako kwa asilimia mia moja. Ikibidi programu ya elimu ya watu wazima irudishwe kama ilivyokuwa wakati wa mwalimu Nyerere. Msisitizo ukiwa katika utoaji wa elimu ya uraia kwa watu wazima ambao hawakupitia mkondo rasmi wa elimu.

Simon Kitururu 12:38 pm  

@Mkuu Malkiory Matiya: Kwa bahati mbaya inawezekana kuelimisha WATU hakuna manufa kwa baadhi ya WATAWALA wetu na hilo linaweza kusababisha iwe vigumu swla kama hili kuungwa mkono kwenye nyanja zote.

Inasemekana elimu kwa WANANCHI ni moja ya chanzo cha usumbufu wa WANANCHI kwa viongozi watawala wenye malengo ya kula kilaini au kula huku wasistukiwe!:-(

emu-three 1:09 pm  

Nakuunga mkono mkuu, na elimu hii itolewe sio shuleni tu, bali itafutwe mbinu ambayo kila mtu ataipata hiyo elimu.
Kwa ujumla raia wengi wa nchi hii ukiwauliza kuna umuhimu gani wa kupiga kura, wengi watakujibu, ili kuwahalalishia wakubwa `kula'
Demokrasia ni kitu geni katika vichwa vya Watanzania, na kwanini iwepo, ...hata haki ndogo ya mtanzania ya kupiga kura, kutoa maoni, ikiwemo kuandamana, au kupinga jambo ambalo linaonakena kuwa sio sahihi, ni mtihani kwa watanzania. Watu wanaogopa!

Simon Kitururu 3:05 pm  

@Mkuu M3: Ni kweli kabisa watu wanakata tamaa kwa maana inaanza kuwaingia watu kichwani kuwa kila uchaguzi KURA tunapiga lakini mambo ni yaleyale!

Kitu hiki kisipofanyiwa kazi mapema watu watachoka na biashara za kupiga kura wakati wanashuhudia walaji ni wengine tu ambao WANATAWALA na matokeo yake wat watajichukulia sheria mkononi na kutotaka kufuata uchaguzi wala nini bali ni vurugu tu ili mradi kila mtu ajichukulie chake.

WOGA unamwisho wake na ndio maana hata MBWA koko ukimuandama sana atakuvamia tu na kuwa mkali - na nasema hivi kwa kuwa wakati niko mdogo niliwahi kuandama mbwa koko na mwisho wake alinitoa baruti na ni kwa bahati nzuri TU hakuniuma tu vizuri!:-(

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 5:23 pm  

Mada nzuri Mtakatifu. Kama mkereketwa wa masuala ya kitamaduni pengine hii ni nafasi nzuri kwangu kupenyeza hoja ya lugha zetu za kiasili. Kwa sasa ni marufuku kutumia lugha yo yote nyingine mbali na Kiingereza na Kiswahili katika masuala rasmi yakiwemo kampeni za Kisiasa - hata kama hao unaowahutubia hawaelewi Kiswahili au Kiingereza. Pengine hizi shule za kata zitasaidia lakini nilishangaa mwezi wa sita mwaka jana nilipomsikia mgombea mmoja akihutubia kijijini kabisa ambako kwa uzoefu wangu wasikilizaji wake hata Kiswahili hawakifahamu vizuri. Mwanasiasa huyu hata hivyo alikuwa anachanganya Kiswahili na Kiingereza kwa wingi. Nilibaki nikijiuliza ni wananchi wangapi waliokuwa wanaelewa hasa alichokuwa anakisema?

Mtu unakuta anafafanua sera zake na kutoa data kibao za Kiuchumi kwa Kiswahili na unabaki unashangaa kama kweli wasikilizaji wake wanamwelewa sawasawa hasa kule vijijini. Hili la lugha mnalionaje au bado hofu za ukabila zimetukamata?

Kuna ubaya gani mtu akifafanua sera zake kwa lugha ambayo watu wanaifahamu na hivyo kuweza kumwelewa zaidi?

Nakumbuka kuna wakati Mh. John Cheyo alihutubia kule Magu kwa Kisukuma na hii ilikuwa "front news" kwenye magazeti "Cheyo Maji Shingoni: Ahutubia kwa Kisukuma". Yeye alijitetea kwa kusema kwamba alikuwa anaamini kwamba watu aliokuwa akiwahutubia walikuwa hawaelewi Kiswahili cha ndani kiasi cha kufahamu vizuri alichokuwa akitaka kuwaeleza. Alishinda!

Simon Kitururu 6:35 pm  

@Mkuu MMN:

Mimi naamini Tanzania tumezoea sana kutishana na mpaka hili la UKABILA kwa sasa hivi mimi naona ni la TISHA TOTO zaidi kuliko kitu kingine.

Naamini kwa sasa hivi ni vigumu sana kurudisha ukabila hasa ukizingatia jinsi tu Watanzania walivyo tawanyika kila mahali kutoka kwenye maeneo ya makabila yao na pia ukizingatia kuwa lengo za kutumia lugha za KABILA fulani hasa hapa tuongelealo nin la jinsi ya kuelezea mchango wa watu kwa nchi yao na sio tu kwa nia ya kutaka kuwa watu wajitoe katika nchi na ya nchi.

Mie naweza kuamini unaweza kutumia KISUKUMA kuelezea vizuri ni kwanini wajifunze KISWAHILI na KIINGEREZA ukaeleweka vizuri kuliko ukawaeleza kwa KISWAHILI moja kwa moja.


Na nin kweli kabisa kutokana mpaka na matatizo ya LUGHA watu wengi ambao ni wapiga kura wanapiga tu kura bila kuelewa na kwa kutumia tu vigezo dhaifu vya ni kwaninni wanampigia mtu kura kisa wamesikia ni MCHUNGAJI , Daktari au tu ndio mwenye mabasi ya DAR mpaka MORO bila hata kujua mchango wa huyo mtu kwao na kwa TAIFA utakuwa ni nini -kama sio ni POROJO tu!


Na pia nasikia kuna maaeneo ni ujiko kuondea lugha za kigeni. Kuna rafiki yangu anadai huko kijijini kwao hukohuko Usukumani kulikuwa na jamaa yeye kazi yake ni kutafsiria watu WAZUNGU wakija wakati kumbe yeye mwenyewe KINGEREZA kilikuwa hakipandi ila wanakijiji walikuwa wanamsifia hasa wakistukia WAZUNGU hawaelewi anasema nnini basi wana -conclude jama anamwaga KIMOMBO mpaka Wazungu wenyewe hawaelewi!:-(

Na ilinitokea wakati mmoja Zanzibar - nilafanyakazi kama MC kwenye ZIFF (lile tamasha la FILAMU ) wakati linaanzaanza. Basi kuliuwa na MC mwingine anajua KIARABU .

Basi wakati mimi naangaza kwa KISWAHILI na KIGEREZA moja yamalalamiko niliyokuwa nayasikia kutoka kwa wahudhuriaji show ilikua JAMAA MBARA huyo kisa accentyagu ingawa wananielewa na yule jamaa aliyekuwa anatangaza kwa KIARABU alikuwa anashangiliwa labda kwa shamra hata kuliko akina CIHIWONISO na ANDY BROWN au Hukwe ZAWOSE walikuwepo siku hiyo kisa kaongea kwa kiarabu tu.

Mwisho nikawa nauliza watu hivi wanaelewa KIARABU anachoongea- na jibu lilikuwa asilimia 95 hawauwa wanaelewa ila walikuwa tu wanamuaona yuko juu kisa anamwaga KIARABU!


Kai ipo!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP