Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

``MARA YA PILI´´ katika UTAMU au KITENDO!

>> Tuesday, February 15, 2011

LABDA chochote kirudiwacho kwa MARA YA PILI,....
....kinautamu tofauti hata kama kwa MARA YA KWANZA  hitimisho lilikuwa nikuwa KIDUDE  aisee ni kitamu!:-(


MARA YA PILI,...
... ni kutaka kurudia kuhakikisha kama ni kweli MARA YA KWANZA  ni kweli  kama ikumbukwavyo ni tamu.

Mara ya PILI,....
..... ni bahati  kwa kuwa LABDA sio wengi wabahatikao KURUDIA  cha mara ya kwanza kwa mara ya PILI hata kama cha mara ya kwanza hakikuwa KITAMU!

Swali:

  • Huwa unafikiria umuhimu wa MARA YA PILI hata kama hapa tuongeleacho ni NAFASI ya kurudia MTIHANI mtu aliofeli MARA ya KWANZA?
  • Huwa una mchezo wa kufikiria ni nini tofauti ya MARA YA TATU ukilinganisha na MARA YA PILI baada ya ile MARA YA KWANZA?

Na kunachakujifunza MARA YA KWANZA hasa kisichofanikiwa MARA YA KWANZA,....
... kama lengo ni angalau MTU kujua anafanya nini wakati kapata nafasi ya kugida tena na hii itakuwa kwake ni MARA YA PILI mchezo uleule!:-(

Swali:

  • Si unajua labda kila siku kuna kitu  hata kama hatukistukii  kwa kila  MTU hufanywa kwa MARA YA KWANZA jambo lifanyalo  kuwa kama MTU NI mjanja na  MAKINI mara hii akajifunza KITU  ikitokea chansi ya kuonja tena KWA MARA YA PILI  huyo mdau anaweza KUINGIA KINGI  bila ubabaishaji mkubwa uliozoeleka  katika maisha ya watu  kutokana na ugeni wa ya MARA YA KWANZA?



Ndio,....
..... labda MARA YA PILI ni SPESHO,...
.... kwa kuwa MTU huwa anakaaidia  ka -nini KINAFANYIKA lakini bado hajazoea na kugeuza KIFANYIKACHO ni mazoea tu,...
.....jambo ambalo hugeuza shamrashamra ya UBWABWA wa sikukuu ugeuke mazoea tu kwa kuwa umeshakuwa UBWABWA wa siku yoyote tu  na sio  wa siku maalumu au wa mpaka WAGENI waje.:-(



Ndio,....
... najua kuna wadaio kuwa ni kwa MARA YA NGAPI mtu anafanya KITU haina umuhimu ,...
.....hasa kama MTU bado kabahatika na  kwa kurudiarudia bado  ANAFANYA hicho KITU na safari hii ni kwa mara nyingi tu,...
.....hata wakati HUU ambao naendelea KUWAZA tu mambo kwa MARA ISIYO YA KWANZA  hapa MHESHIMIWA hata ambaye BADO  usalimiaye kama wa ARUSHA na NAIROBI waenzi za   ``NIAJE!´´:-(






Hebu tugewe JAZZ tena itubadili wazo kwa ndude- Picadilly Square

Kamailivyotungwa na:
Carl Allen

Na kudungwa hapa katika mpakuo huu na: Mulgrew Miller - Piano;
David Williams - Bass;
Carl Allen - Drums;
Tom Harrell, Jon Faddis - Trumpet;
Bobby Watson - Alto Saxophone;
Lew Tabackin - Tenor Saxophone



Turudi tu AFRIKA KUSINI ili RAY PHIRI aingilie kati shughuli kwa-Highland Drifter



Au tugawiwe tu pia na Black Coffee kinu - Turn Me On

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 9:20 pm  

Maisha yote ni marudio na mizunguko. Yapo marudio yenye ubwabwa ndio; lakini mengine ni mkate kabisa uliyewiva na kukomaa. Marudio mengine ni kero tupu, lakini mengine ni faida.

Kama wewe ni mwalimu; na wanafunzi wako wanairudia kazi mara kwa mara, basi unashindwa...

1. Kama siyo jinsi ulivyoandaa somo lako...

2. Itakuwa jinsi ulivyoshindwa kumwelewa mwanafunzi wako anamaanisha nini kwa jibu lake.


Kama nawe Mwalimu au Mkubwa fulani unao mamlaka wa kumfanya binadamu mwenzio arudie chochote kile, tafadhali mpe kazi/mtihani sambamba*?(PARALLEL*)...na asirudie shughuli ileile... kwani utakuwa unamtesa usipofanya mabadiliko kidogo!

Kwamasomo ya ubongo wanasema unakosea unapopitisha ujumbe kwa hiyohiyo njia moja katika fahamu, badala ya kujaribu njia zingine wakati kila binadamu inasemekana anazo njia (DENTRICAL CONNEXIONS) kama elfu kumi hivi kwelewa kitu kila kimoja.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP