Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NAKUWAZA!

>> Tuesday, February 15, 2011

Na katika KUWAZA mtu,...
.... kwa bahati mbaya ni MACHACHE tu YA  akumbukwaye MTU kwa wakati mmoja naweza KUKUMBUKA!:-(





Na wakati AWAZWAYE mtu ,...
.....alikuwa kafanyia mtu  MAZURI kwa kawaida KUTOKANA na udogo wa kumbukumbu za wakumbukaye MTU kirahisi ni MAZURI  na sio MABAYA ndio watakayo KUMBUKA!:-(

Swali:

  • SI inakumbukwa kwa kawaida SI RAHISI kwa wakati mmoja kukumbuka kila kitu  kuhusu MTU?

Na kwa kuwa labda si rahisi kukumbuka yote ya akumbukwaye MTU;...
....akumbukwaye kwa MABAYA labda hutokana tu na urahisi wa kukumbuka yake MABAYA kuliko mazuri kwa kuwa labda ukweli bado ni kuwa  HAKUNA mtu MBAYA asiye na ZURI hata moja!:-(


NAWAZA tu MHESHIMIWA!:-(


Hebu BEBE MANGA arudie-AMIO



Au tu Charlotte Mbango arudie -Konkai Makossa


3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 10:21 am  

Wapo, kwa maoni yangu watu wabaya 100%.

Tunaposema "hata mbaya anauzuri wake" tunamaana huko anakokupeleka mbaya huyo wakupindukia inawezekana ukaokolewa na wengine WAZURI wakupeleke tena pazuri hata kuliko kabla ya mashambulizi ya mbaya.


Lakini, kutokana na hali ya kupona na kufarijiwa kwako na WAZURI, hatuwezi tukaanza sasa KUMSIFU mbaya kwamba eti 'naye anauzuri wake'.


Hayo yatakua mawazo potofu kwa maoni yangu kwa sababu idadi kubwa wanaangamizwa na kuteketezwa kabisa mbele za huyo MBAYA na nawewe uliyepona ni mmoja tu kwa wachache sana ambao wamepona na kumshukuru Muumba.

Kwa Kizungu ningeyasema hayo ya juu hivi: THE VICTIM'S COMEBACK AND EVEN PAYBACK IS AN EXCEPTION BUT NOT THE RULE.

Hata hivyo, ni ukweli kabisa kwamba ukitaka kuhakikisha unakumbukwa na kuwazwa na MKUU MTAKATIFU SIMON KITURURU MAWAZONI, hakika atakukumbuka UKIMFANYIA MABAYA!


Na hiyo inatokana na jinsi ubongo waBinadamu Mkuu Mtakatifu unavyofanya kazi: kila anaposhtuka, kila anapo kasirishwa au kuumizwa na mtu, maji fulani (a HORMONE) katika mafigo yake yanaingia katika damu na kwanza mbio za kufika haraka sana ndani ya ubongo ila kurahisisha kumbukumbu (THE REGISTRATION OF MEMORY).

Mfano mzuri: wasomaji waBlogi yaMkuu Mtakatifu wengi watakwambia walikuwa wapi siku ya mashambulizi ya 9/11 huko Merikani; lakini hakuna atakayekwambia yeye alikuwa wapi siku ya MSAADA WAKWANZA KUFIKA HAITI BAADA YA TETEMEKO LA ARDHI HUKO.

Sasa hiyo ni maana mpya kabisa ya msemo waWahenga kwamba: "CHEMA CHA JIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA"

Simon Kitururu 10:42 am  

@Mkuu GOODMAN: Mimi naamini hakuna mtu mbaya 100% labda ndio maana mpaka HITLER asifiwaye kwa ubaya alikuwana GIRLFRIEND ambaye alikubali mpaka kufa naye!

Nafikiri moja ya sababu hakuna mbaya 100% ni udhaifu wa KIBINADAMU!

Si amini kuna BINADAMU asiye dhaifu hata katika swala la kuamua tu kuwa awe MTU MZURI!

Kama tukishindanisha mashindano ya kuwa MTU MWEMA bado tutastukia kuwa sio wote WEMA wataingia katika FAINALI ya kinyang'anyiro hicho- na naamini ni hivyohivyo kwa MABAYA hata kwa kujitahidi kuwa BINGWA wa mabaya tukimuekea huyo mtu KAMERA masaa ishirini na nne, twaweza stukia na MAZURI yake ambayo kwa udhaifu wake tu wa KIBINADAMu kashindwa kujizuia kumtendea mtu!.

Na labda ndio maana hata wajulikanao kama MAJAMBAZI katili ,...
... unaweza kukuta majumbani kwao wanajulikana kama BABA mwema kabisa kwa watoto wao au MUME mwema kabisa kwa wake zao hata kama nje huko ni wauaji!:-(

Ndio nakubali kuwa labda si kitu kilichozoeleka kusifia WABAYA,..
... lakini bado kwa roho mbaya ya mtu hata katika kukunyima tu KITU,...
... inaweza ikawa ndio changamoto nzuri kwa mtu na iliyofungua mlango tofauti wa POSSIBILITIES na huo wenye POSSIBILITIES labda usingestukiwa kama mchango wa kutendewa MABAYA haukuwepo.

Na naamini hakuna KIZURI kama hakutakuwa na KIBAYA kama ilivyokuwa labda HAKUNA umuhimu wa MUNGU kama hakuna SHETANI.

Kwa hiyo labda SHETANI ni muhimu na anauzuri wake katika kuchangia watu wastukie ya MUNGU.


Ndio ,...
... inasemekana ni SILIKA ya BINADAMU kukumbuka ukitenda mabaya, na ni silika ya BINADAMu kuvutiwa na MABAYA ndio maana nasikia BAD NEWS hata kwenye TV ndio GOODNEWS kwa kuwa ndio huvutia watu wengi kuangalia HABARI!

Ila bado swali:

Hufikirii labda tumejifunza tu kuweka UBONGO unogewe kurahisisha KUMBUKUMBU kistaili ambayo MAZURI ya watu hatuyaoni kirahisi kuliko MABAYA ya mtu?

Goodman Manyanya Phiri 11:08 am  

Labda tusikilize maoni ya wengine, Mkuu.

Hili suali ni ngumu kweli; na ulinikosha kwamba habari kwenye Tv huvutia zikiwa habari mbaya!

Nakweli!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP