Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

TUJUAYO ya wakati ULIOPITA, wakati HUU na wakati ujao AFRIKA!

>> Monday, February 21, 2011

Nawasiwasi na YALIYOPITA tujuayo kuhusu AFRIKA hata kama WAAFRIKA,...
.... kwa kuwa MENGI  tufunzwayo na WASOMI kuhusu AFRIKA hayakuandikwa na WAAFRIKA walioelewa AFRIKA na WAAFRIKA.:-(
Na na wasiwasi na ilipo WAKATI HUU Afrika,...
.... kutokana na kidhaniwacho ni UAFRIKA kinavyochanganywa na kutojiamini kwa WAAFRIKA na yao ya KIAFRIKA kifanyavyo WAAFRIKA kuiga au mpaka kukana kinamna UAFRIKA kwa jina la MAENDELEO na ustaarabu udhaniwao mpaka na waitwao wasomi wa KIAFRIKA na kufanya mpaka DHANA nzima ya maendeleo  AFRIKA kuoanishwa zaidi na visivyo na asili ya KIAFRIKA na WAAFRIKA.:-(

Na yote haya huchangia niwe na wasiwasi na WAKATI UJAO  kwa ya KIAFRIKA,...
..... kwa kuwa  labda mizizi na SHINA la ya BAADAYE katika UAFRIKA tayari vinaelekezwa MBOBEO katika yasiyo ya KIAFRIKA:-(


Na nawaza tu hapa MHESHIMIWA wakati LABDA sijavaa KIAFRIKA wakati niandikapo huu: 
 UjingaBUSARA!:-(Swali:
  • Hivi unafikiri ni UAFRIKA kuvaa KIAFRIKA?
  • Unafikiri katika ndoto  za WAHESHIMIWA  VIONGOZI wa AFRIKA huwa wanaota KIAFRIKA?
  • Hivi UAFRIKA ni UPI?
Nje kidogo ya SWALA:

Mimi naimba kwaya kwenye CHRIST CHURCH siku hizi na asilimia kubwa ya waimba kwaya kwenye kwaya hii ni WAAFRIKA KUSINI weupe aka WAZUNGU , ...
.... na nasikitika kuwa MWANZONI nilikuwa nashtuka kila wakijitambulisha kuwa ni WAAFRIKA hasa kwa kuwa  hata mara moja hawasiti kujitambulisha  kuwa ni WAAFRIKA kwa mtu yeyote yule.:-(NIMEACHA!
JUMATATU njema MHESHIMIWA!

Na hebu Herbie Hancock aje na Pink, Seal, India  Arie ,Konono N 1, Oumou Sangare na Jeff Beck katika jiwe -ImagineAu tu Herbie Hancock arudi tena na K.S. Chithra, Chaka Khan, Anoushka Shankar na Wayne Shorter katika ndude-The song Goes OnAu tu Herbie Hancock amalizie tu akiwa na K'naan, Los Lobos na Tinariwen kwa - Tamatant Tilay / Exodus

9 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Malkiory Matiya 12:43 am  

Pengine ndiyo kupishana na falsafa yenyewe mkuu.

SIMON KITURURU 8:19 am  

@Mkuu Malkiory Matiya: Si utani labda kuna ukweli katika engo uliyobinyia mtazamo!:-(

SIMON KITURURU 8:19 am  

@Mkuu Malkiory Matiya: Si utani labda kuna ukweli katika engo uliyobinyia mtazamo!:-(

Mwanasosholojia 10:43 am  

Mtakatifu hili ni fumbo kubwa..labda ni KUTENDA kiafrika..si kuanzia kifikra hadi kimuonekano...Hongera kwa kuanza kuimba kwaya mkuu, umenikumbusha enzi zangu!

Goodman Manyanya Phiri 12:22 pm  

Asante Mkuu Kitururu kwa Post nzuri, tena kama kawaida yako, yenye kuvutia! Mkuu Mwanasosholojia naona yuko karibu nami.

Huko Christchurch, Johannesburg au Dar es-Salaam, binadamu akijitambulisha kwako 'yeye ni Mwafrika', wewe unahaki gani kumpinga kutokana na rangi yake?


Si Waarabu, kwa Wazungu (tena wanafanana na zeruzeru waKiafrika), na makabila yote ya ulimwengu wote hapo mwanzoni walikuwa Waafrika?


Sisi weusi wa karne hizi tunao uthibitisho gani kwamba Waafrika wakwanza kabisa walikuwa weusi kama sisi au weupe kama Wazungu na ni hapo baadaye tu kutokana na joto tulipoanza kuwa weusi ikiwa kwa maana ya kwamba ukihimiza rangi ya mtu kuliko ubinadamu: "Mzungu ni Mwafrika kuliko Mswahili"?


Kusema ukweli, siku hapo sisi Waafrika tutakapoacha kukalia rangi ya mtu kabla ya kuchunguza roho yake ndio tutakuwa na matumaini zaidi na bara letu na kwondokana na AFROPESSIMISM.


UAfrika siyo ubinadamu tu, bali ni ukereketwa vilevile, kama ule waMtakatifu!


UAfrika, Uzungu (kuwa mwenyeji wa Ulaya), na kadhalika siyo mavazi, wala rangi yangozi, wala lugha, wala chimbuko wala jinsi ndoto zinavyomjia mtu. Ni kitu kingine kabisa, tena maalum!


Tuchukuwe Bara-X kama mfano.


Ukiwa ungependa kutambulika kama Mbara-X masharti yako mawili tu na lazima yatimizwe yote mawili.


1. a) Umezaliwa Barani-X au umezaliwa nje ya Bara-X na mzazi-mzaliwa-Bara-X (mmoja au wote wawili).

1b). Kama hukuzaliwa Barani-X, wala hunamzazi kutoka Bara-X, OMBA URAIA NA UPEWE!!!2. Unalipenda Bara-X kuliko bara lolote lile lingine ulimwenguni.

SIMON KITURURU 12:37 pm  

@Mwanasosholojia: Nilianzia Morogoro kuimba kwaya katika kwaya ya VIJANA BUNGO pale BUNGO Lutherani CURCH enzi hizo na naona tabia hii haijanitoka bado mpaka siku hizi .

Vipi kwanini umeacha kuimba kwaya?


@Mkuu Goodman:Tatizo ni baadhi yetu tulivyozoea kuunganisha BARA na rangi za watu. Nakumbuka rafiki yangu alienda kama CONTRACTOR katika moja ya ujenzi IRAQ na cha kwanza alichoshangaa ni kukuta WAIRAQ weusi kama yeye ambao ni WAIRAQ kwa generation kibao kwa ujumla hata hawajui MABABU zao walifikajefikaje IRAQ kwa kuwa wanahistoria ya zamani kuliko enzi za utumwa. Na cha kwanza kilichokuwa kinamsumbua ni kuwa hivi kweli wale ni WAIRAQ na kwanini pamoja na vita yote hii hawaonekani kwenye NEWS angalau kuwa wamepigwa bomu!


Na kuna rafiki yangu mwingine MJAPANI yeye alikuwa anaunganisha WEUSI na MAREKANI kwa kuwa WATU weusi aliokuwa akikutananao huko kwa o JAPAN karibu na KAMBI ya WAMAREKANI walikuwa ni WAMAREKANI na mara ya kwanza kukutana na WAAFRIKA kutoka AFRIKA ilimchukua muda kuwaoanisha na AFRIKA.

Tukiachana na hayao:
Umeniwazisha MKUU!

Yasinta Ngonyani 2:36 pm  

Ni mada nzuri sana na yenye changamoto. Maana binafsi pia nimekuwa nikijiuliza hivi mwafrika ni yule aishie Afrika tu au ni rangu au ni utamaduni na sijapata jibu naona hapa leo nitapata jibu:-)

Anonymous 3:13 pm  

Hii mada inahitaji tafakuri ya kina. Mimi pia najiulaza sana kuhusu hili.
Hongera kwakumsifu Muumba kwa njia ya kwaya.

SIMON KITURURU 10:11 am  

@Anony: Asante Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP