Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UNATAKA UKUMBUKWEJE - na DAKTARI wa SEHEMU ZA SIRI baada ya kutoka kuchekiwa na DAKITARI sehemu za SIRI?

>> Friday, February 18, 2011

UNATAKA UKUMBUKWEJE - na mwizi baada ya kumalizana na MWIZI aliyekuibia?

UNATAKA UKUMBUKWEJE-  na MPENZI baada ya  MAPENZI kufa na kubakia ni kitu cha zamani cha kufikiria?


UNATAKA UKUMBUKWEJE - na NDUGU , jamaa na MARAFIKI baada ya uwepo wako duninani kutoweka  na kubakia ni stori tu za wachache ambao bado  kuna kitu kuhusu wewe wanafikiria?




UNATAKA UKUMBUKWEJE- na muuuza MAANDAZI  wa pembeni ya muuza VITUMBUA  pale ambapo ni  VITUMBUA ulipokuwa unavifuatilia?


UNATAKA UKUMBUKWEJE- na muuza VITUMBUA ambaye  vitumbua vyake ulikuwa ndio MTEJA ingawa  labda hatajina lake MUUZA vitumbua hujawahi kulifikiria?





Na kuna watakao kumbukwa kwa kunuka uchi, kukumbukwa kwa UJINGA, uhodari, UBAHIRI, utu wema,.......
...... ingawa kuna wengi ambao tutasahaulika  kwa kuwa,...
.... hata kinachokumbukwa  kwa wakumbukwao  ni tone tu na LABDA ni  kwa mtazamo tu wa staili moja ya WAKUMBUKAO.:-(

Swali:
  •  Si labda Rais NYERERE kwa wamkumbukao TANZANIA wanamkumbuka kwa staili moja tu yenye uhusiano na AJUAVYO KUVAA VIATU na hakuna amkumbukaye kama MCHUNGA MBUZI  huko kwao wakati anamagaga miguuni huko kwao KIJIJINI akiwa fulu  kutembea bila viatu  na labda funza wa mara kwa mara ni fulu kitu cha KAWAIDA?

  • SI inajulikana kuwa labda hata TENDO MOJA  kama lile la NJEMBA KADODA la kuiba chupi ya demu kwa ajili ya kumbukumbu zake kuwa hii ni chupi ya Mwanadada KADALA asifikaye mtaani - huwa hapo kuna MIZIZI ya kumbukumbu MBILI TOFAUTI KABISA KIMUELEKEO  ambazo zinatofautiana ingawa chanzo ni TUKIO MOJA  ambazo huweza kuwa ni -KUMBUKUMBU moja yenye mizizi kutoka kwenye kumbukumbu za DADA KHADIJA- samahani Mwanadada KADALA aliyeibiwa CHUPI - na kumbukumbu yenye mrengo wa  PILI  ichipuayo na yenye MIZIZI kutoka kwa NJEMBA KADODA ambayo ndiyo iliiba chupi ambayo nayo kikumbukumbu inasababu zake za mpaka  ni kwanini haiifui hiyo chupi chafu - na mirengo yote miwili ya kumbukumbu kuzaa kumbukumbu nyingi tofauti ingawa asili zake ni   TENDO MOJA TU lililowahitokea migombani gesti?


  • Hivi MKUU unataka UKUMBUKWEJE?


Ndio,...
.... mie kama Simon Kitururu sina noma kabisa na kusahauliwa,...
..... ingawa kama ikitokea kuna MTU atanikumbuka,...
... ningependa angalau nikumbukwe hata kama NILISHINDWA kuwa ni MTU aliyewahi KUJARIBU!:-(




NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Ijumaa na WIKIENDI njema MDAU!


Hebu  Konono NO. 1 waingilie shughuli...






Konono No. 1 waendelee







Au tu Baloji aje na Konono NO. 1 wamalizie kukuna kipele kwa - KARIBU ya bintou

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:52 am  

Kukumbukwa ni wachache sana wanakumbukwa... Duh Kaka Simon nilipoona kicha cha habari hicho ... ok. Nimesoma huku nikiwa na tabasamu baada ya kufikia hapo kwenye majina ya KADALA NA KADODA:-)

nyahbingi worrior. 6:56 am  

nadhani nitakukumbuka kwa kujari kuisimamami jumuwata.

Simon Kitururu 8:02 am  

@Yasinta: Samahani kwa kukutisha kwa KICHWA!Halafu nahisi unatabasamu vizuri kweli wewe KADALA! :-(

@Rasta Luihamu: Kweli kama wengine watasahau mie hilo Ntakumbuka!

chib 6:26 pm  

Habari ya Kadala imenifanya nijikwae!

Simon Kitururu 6:45 pm  

@Mkuu CHIB: Unajikwaaje ? Au unatembea huku una surf net kwenye simu?

Goodman Manyanya Phiri 10:37 pm  

Yupo Mbunge mmoja huko Wingereza naye alikuwa na sifa (au kero) ya kusoma HANSARD (yale maandishi yaliyoandikwa juu ya mijadala mbalimbali ya bungeni).

Naye aliulizwa siku moja: "Mzee, kwanini uansomaga haya maandishi kwa makini?"

Alijibu: "Mimi nataka nisahihishe kila kosa la mwandishi katika mambo ya SPELLING pale wanavyoninukuu mimi, kwani sitaki vizazi vijao vinielewe mimi kama mtu asiyejali namna ya kwandika maneno"

Simon Kitururu 9:41 am  

@Mkuu GOODMAN: Duh! Yani jamaa alikuwa anajali hoja imeandikwaje kuliko HOJA inamchango gani yani!:-(
Lakini labda kuna kitu kafanikiwa kwakua tunamjadili sasa hivi hapa!


Ila mambo ya kukumbuka ni nusu nusu ndio maana hata kwa WAKRISTO kuhusu YESU kilichonukuliwa ni muda mfupi tu wa maisha yake kitu kifanyacho tufikiri alikufa BIKIRA!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP