Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tunakabili MAISHA kwa Kucheka ,KUNUNA, kulia kama tu KULA SANA,...

>> Monday, February 14, 2011

.... kama tu POMBE kwa   SANA kwa baadhi ya watu ,...
.....labda ni coping mechanism tu a.k.a STAILI tu za BINADAMU za kujaribu kukabili halihalisi IMKABILIO mtu  maishani,....
.... kwa kuwa KIBANO kikizidi  watu hutafuta tu jinsi nyingine ya KULAINISHA hali  hata kama ni ile ya KUJIDANGANYA tu kidogo  tu kinamna.


Na kwa mfano :

KUCHEKA- kuna AUHENI zake kama maishani kuna KIBANO hasa kwa kuwa ACHEKAYE hili si kweli kuwa hana LILE ambalo bado lasumbua MTU.


KUNUNA- kunasaidia angalau kuonyesha dukuduku lipo na ANUNAYE  akimaliza kununa kuna kitu katika dukuduku moyoni hupungua.


KULIA- ni moja ya dawa kwa mwenye maumivu na WENGI wakimaliza kulia hujisikia vizuri.


KULA SANA- kula nifaraja na wengi huchagua KULA hata kama hawana njaa kupunguza mawazo.

Swali:

  • Umechunguza ufanyayo sana LABDA ni  aina tu mojawapo ya kujaribu kukwepa ambayo hupendi kufanya au hujaribu kufanya?


Ndio,...
.... hata kuchukia MTU,....
.... kunaweza kuwa ni aina tu ya kukwepa kitu kingine KWA MCHUKIAJI ambacho kinaweza kuwa ni kile cha  ya MTU achukiwaye ambacho kinafanana sana na YAKEMEWAYO na kuchukiwa yale ya ACHUKIAYE MTU mwenyewe!:-(


NI wazo tu HILI!


Hebu Shihan atusaidie kubadili wazo kwa -Flashy Words



Au Shihan amalizie tu tena - Sick and Tired

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 8:56 pm  

Siri ya maisha haipo katika kukwepa vitu kama hivyo vyote uliyetaja. Nafikiri siri ni kuweza kutumia kwa kiwango tu, wastani au IN MODERATION.

http://www.reuters.com/article/2011/02/11/us-alcohol-idUSTRE71A2FM20110211

Simon Kitururu 9:39 am  

@Mkuu GOODMAN: Lakini maishani kihalihalisi ni mengi tunajaribu kuyakwepa hata kwa dawa temporary kama POMBE ilimradi kwa muda akili haibobei kwenye kitusumbuacho sana au kwa KIMADA ili mradi hasumbui sana kwa kuwa bado ukiwa na KIMADA fantasy zawezekana kuliko MKE ajuaye kila kitu na kufanya mambo mengi yageuke halihalisi ambayo yaweza kuwa inamaumivu masihani!


Na naaamini MODERATION ni moja ya kitu kigumu sana kwa BINADAMU na ndio maana utakuta kirahisi watu wanajilimbikizia ukiwapa nafasi hata kama wanajua kuwa WAJILIMBIKIAVYO hawana muda wakuvitumia vyote katika maisha haya mafupi ya BINADAMU!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP