Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

DAWA kwa IMANI,...

>> Friday, March 11, 2011

... labda IMANI,...
... ndio DAWA yenyewe!

Swali:

  • Aponaye kwa IMANI hata kama alipewa mizizi si labda bado ni IMANI YAKE  ndio DAWA yenyewe?
  • Na si inasemekana usipopona katika dawa ziegemeazo kwenye IMANI kwa kawaida unaambiwa imaniyako ni ndogo kwa kuwa ni kwa imani ungepona?


Wakati  kuna wagonjwa wengi inasikika kuwa wako safarini kuelekea Kijiji cha Samunge, kata ya Digodigo Wilaya ya Ngorongoro kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile ili kutibiwa,...
... na wakati nawaza fani nzima ihitajiyo IMANI iliupone katika ile kitu nzima ``IMANI yako ndio itakuponya!´´,....


....naomba tuombee mabadiliko Tanzania,..
... kwa kuwa labda twahitaji zaidi ya IMANI ili tupone angalau hata kama TAIFA tu kwa jinsi hali ilivyokuwa MBAYA!:-(


Ijumaa na WIKIENDI njema MDAU!



Hebu katika kubadili wazo twende tena  Ethiopia kidogo tukatekenywe na mtoto wa Kiethiopia Meklit Hadero katika pini-Leaving Soon




Meklit Hadero alainishe zaidi  lawalawa kwa-It will be Quiet




Au tu ngojea Meklit HADERO aongee huku nikikiri kuwa nina udhaifu naye huyu mdada  ....

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Albert Kissima 1:30 pm  

Mbali na kutibu, labda "imani" inaweza kuwa "kinga" ya magonjwa :-) duh!

Simon Kitururu 1:37 pm  

@Mkuu Albert:Kweli kabisa!

Ingawa sishauri mtu anywe maji machafu ya choonin kwa makusudi huku akiwa na imani ni masafi au hayatamdhuru!:-(

Duh!

emu-three 1:40 pm  

Ndugu zangu, ndipo tulipofikia hapa kwetu, kilichobakia ni imani, amini utapona, amini utashiba,amini umasikini utaondoka...nimesoma masoma mahali kuwa kijana mmoja kamuua baba yake kwa kuamini kuwa ndiye anayezuia mvua!

Simon Kitururu 2:04 pm  

@Mkuu M3: Cha kusikitisha ni kwamba imefikia mpaka chochote kile WATU HUAMINI SIKU HIZI kutokana na kutapatapa kwa watu kutokana na hali ilivyo mbaya!:-(


Na uhakika huko huko Loliondo watu wakisikia kuna mjusi uliokuwepo KIGOMA ambao ukiuangalia tu unapona na kutajirika- kuna watakaoanzisha safari nyingine kutokea hukohuko kwa Babu !:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP