Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama tu KITU kizuri tusivyoridhikanacho na kukitafutia KASORO,....

>> Friday, March 25, 2011


....katika KUFANYA yawezekanayo ambayo HATUYAFANYI ,...
......labda  wengi wetu tutafutacho ni VIZINGITI na VIPINGAMIZI!:-(



Na wakati ili tupate NGUVU ya kuchukua HATUA na kuanza KUTEKELEZA,....
.....tufikiriacho KUFANYA,....
......tutakacho KUFANYA,....
......labda kihitajikacho ni  MTAZAMO chanya na MATUMAINI katika ya  dalili za WEZEKANO na yawezekanayo na kuanza kufanya kwa kuwa LABDA   hakuna chochote ambacho  kitakosa VIZINGITI na kitakosa VIKATISHAVYO TAMAA kuanza  kama  ukivisaka hivyo,....
.... hasa kwa kuwa kwa kuwaza tu sana KIMTAZAMO HASI na woga wa nini  ni pungufu katika HALIHALISI  YA MTU kabla YA KUFANYA ,...
....yaweza kuwa ndio kitengenezacho KIZUIZI kikubwa cha kutatua matatizo ya mtu na ambacho ndicho hasa  BREKI ya cha kufanya kitu ili kujikomboa- KIPINGAMIZI!:-(


Swali:
  • Au?
  • Kuna mangapi unafikiri HUFANYI  kwa kuwa umejitafutia tu mwenyewe VIZINGITI na vipingamizi na labda hata UDHAIFU ili kuhalalisha HAVIWEZEKANI hata kujaribu  KUANZA pambano la kujikomboa?
Ndio,...
... labda kitu KIZURI ,....
... wengi wetu tunakitafuta KASORO na udhaifu ili kujizuia kitu,....
.... na kwa bahati mbaya labda hakuna kitu ambacho ukikichambua ili kusaka KASORO na  ,....
..... utakosa udhaifu na  KASORO!:-(

Swali:
  • Si unajua  hata MREMBO usiyemuona kasoro kwa kuwa ananukia vizuri bado ukimsachi mpaka utumboni bado utamkuta anatembea na mavi kwenye utumbo?
Ndio,....
.... kama unataka KUFANYA kitu  ,...
... ukitaka kupata vizingiti na vipingamizi vya kufanya hivyo vitu ,...
.... utavipata tu MHESHIMIWA!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA lilengalo WOTE wenye MAAIDIA  ya kufanya MAVITU babu kubwa  ila WANASITA kuchukua hatua ya KUANZA KUFANYA MAVITU hayo MAKUBWA!:-(



Hebu TATUNANE waanzishe vita mpya kwa-Msewe



Tatunane waendeleze...

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP