Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mambo yote MBEYA! -Babu wa LOLIONDO who? Kijana wa Miaka 17 aibuka na Dawa Jijini Mbeya.

>> Saturday, March 26, 2011




Pata Picha za MCHEZO mzima:













Maelezo ya PICHA:

1.Mganga mwingine wa tiba za magonjwa Sugu aliyefahamika kwa jina la Jafar  Welino(17) mkazi wa mtaa wa Mianzini Kitongoji cha Mabatini jijini Mbeya ameibuka na kutoa tiba kwa mamia ya wakazi wa jiji la Mbeya na viotongoji vyake.

2. Umati wa watu ulionekana katika nyumba anayoishi kijana huyo wakisubiri kupatiwa tiba hiyo huku wakiwa na vikombe vyao mikononi. Baadhi ya wananchi waliofika eneo hilo walidai kuwa wamefika hapo kutokana na taarifa za kuwa kijana huyo anatibu magonjwa Sugu bure kama vile ambavyo anatibu Mchungaji mstaafu wa Loliondo Mzee Ambilikile Mwasapila.

3. Akizungumza  kwa niaba ya kijana huyo mama mkubwa wa mganga huyo aliyejitambulisha kwa jina la Edina Sanga alisema kuwa kijana huyo alianza tiba hiyo wiki mbili zilizopita ambapo kabla ya kuanza kutibu alimueleza mama yake huyo kuwa alitokewa na mama yake mzazi a,mbaye kwa sasa ni marehemu akimuelekeza kurithi mikoba yake.

4. Bi.Sanga alisema kuwa mama yake kijana huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa ni mtu mwenye maruhani ambapo kwa kutumia maruhani hayo alikuwa akitoa tiba kwa wakazi mbalimbali mjini Mbeya.Alisema kijana huyo ambaye wamezaliwa mapacha na dada yake aliyemtambulisha kwa jina la Hadija Welino kwamba yeye anasoma kidato cha Nne katika shule ya sekondari Itende.

5. Hata hivyo Bi.Sanga alisema kuwa kijana huyo aliitwa katika ofisi ya Ofisa Mtendaji ili kutoa maelezo ya namna ambavyo anaendesha tiba hiyo na kuwa hata hivyo anaendelea kutoa tiba kwa watu kwa kunywa vikombe viwili kwa muda wa siku mbili. Alisema kuwa dawa hiyo aliifuata katika kijiji cha  Iyula kilichopo wilayani Mbozi na kuwa mara alipofika alianza kuichemsha na kuwagawia wananchi wanaosumbuliwa na maradhi sugu. Aidha umati wa watu walikuwa wamejipanga katika mistari kusubiri tiba hiyo ambapo

6. Mwenyekiti wa mtaa wa Mianzini Bi.Elizabethy Mwakabungu aliweka utaratibu wa wananchi kupata tiba ikiwa ni pamoja na kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya kununulia kuni za kuchemshia dawa hiyo.Akizungumza na umati wa watu waliokuja kujipatia tiba hiyo Mwenyekiti huyo wa mtaa alisema kuwa kila ambaye atapata kikombe kimoja cha dawa anatakiwa kupata kikombe cha pili siku inayofuata.

7. ‘’Mganga katuagiza kuwa kila anayekunywa kikombe kimoja anatakiwa kunywa kikombe cha pili siku inayofuata…yeyote atakayekunywa hatakiwi kunywa pombe kwa muda wa siku saba,’’alisema Bi. Mwakabungu

8. wakipata kikombe

9.maelekezo ya kufika eneo hilo

Pamoja tunaendeleza kupashana Habari








Ndio haya mavituz yanaletwa na MBEYA yetu BLOG ,...
...yaliyonifikia na ujumbe :
``Nimekutumia habari hii kutoka Jijini Mbeya .
Kuna kijana ameibuka nae anatoa dawa .
Hizo ni picha tulichukua eneo la tukio na pia na kila namba ya picha naambatanisha maelezo hapa chini.´´

Kumbuka  katika sentensi  iishiayo na maneno ``MAELEZO hapa chini´´  - maelezo yenyewe  na picha ndiyo hayo,..  ....HAPO JUU.




Hebu Chico Debarge aanzishe upya kwa kubadili mkao wa firigisi kwenye kikaango kwa ndude- Trouble Man


Chico Debarge adadavue kwa kuweka grisi kwenye belingi kwa - Love Jones



Hebu Chico DeBarge amuongelee kidogo BIKIRA katika - Virgin





Au tu Chico DeBarge ajaribu zaidi kuzima tu manyanga kwa ndude - Iggin' Me



1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 8:05 pm  

Ni kiri au nisikiri?


Sijaweza kupata muda wa kusoma kwa undani jinsi serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoshughulikia suala la waganga wa kienyeji.


Labda njia ipo kubwa zaidi ya kuwasogeza katika mambo ya tiba za kisayansi (hiyo nasema kama serikali bado imelikunjia uso suala hilo).


Jamhuri ya Afrika Kusini huku tunataka kuwaingiza nao waganga wa jadi wapate heshima yao kuwatibu wagonjwa. Lakini inaelekea wao wenyewe wanagoma kabisa kwa kudai kampuni kubwa za Ulaya [lazima zitawaibia siri zao za tiba].

Jamhuri ya Zimbabwe waliingiza zamani ushirikiano katika madaktari wa kisayansi na waganga wa kienyeji nasikia, kiasi kwamba waganga wa kiswahili wanatembeleaga hata wagonjwa wao waliolazwa hospitalini za serikali.

Kifupi, kwa ndugu zetu Watanzania na serikali yao ['USIEKISHINDA BORA UKIDHIBITI'...JOIN WITH THEM WAGANGA WA KIENYEJI IF YOU CAN'T BEAT THEM].



Mimi binafsi nimeguswa na kauli ya kwamba kijana huyo 'alimuona' mama yake (A VISION OR A DREAM) akimuamuru afanye uganga huo.

Siri bado ni pana, ndefu, na bado kufichuliwa kuhusu nguvu za ndoto.

Mimi binafsi nimewahi kuota ndoto moja hiyo hiyo na mke wangu wa kwanza usiku mmoja; pia hivyohivyo na baba yangu mzazi.

Siku hizi kila hatua wanaochukua maadui zangu (http://goodmanmanyanyaphiri.blogspot.com/2011/03/brigadier-general-norman-yengeni-busted.html)katika mapambano yangu nao lazima nitakuwa nimeota tayari siku tatu hadi sita kabla ya hatua yao kutokea na sijui inakujakujaje).



Kwa waganga wa kienyeji zaidi, nimefurahishwa sana pia na amri ya mganga kijana huyo anavyohimiza uwachaji wa pombe hata kama ni kwa hizo siku saba (nasikitiaka kidogo hakusema "siku sabini mara sabini").


Na kweli, hapo kwangu mganga amepata FULL MARKS kabisa!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP