Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Simon KITURURU kwanini unapenda KUBLOGI?

>> Friday, March 04, 2011

Samahani kuna wadau wamenivuta pembeni kuniuliza mara kwa mara  MASWALA yachezayo na kitu ambacho  majibu kwa KIFUPI ni:


Mwanzoni nilianza kublogu kwa KISWAHILI katika kukidhi maswala binafsi tena labda YA KIBINAFSI -na swala kubwa ilikuwa ni nia ya kuendelea kuitumia lugha ya KISWAHILI hasa kwa kuwa tokea mwaka 1996 maishani mwangu  kiswahili kilikuwa kinapigachenga hasa kwa kuwa sikitumii nyumbani, MASHULENI, kazini au hata baa na MAKANISANI kwa sana hasa kutokana na kujikuta nimechanganyika zaidi na watu wasiojua KISWAHILI!:-(  - ni jibu la kwanza la kwanini napenda KUBLOGU.

Na kwa kifupi kiswahili nilikiachia ``O-Level -MOROGORO Sekondari enzi hizo katika maswala ya kukitumia kimaandishi  hasa kwa kuwa mie sio muandikiaji BARUA watu mzuri na na hiyo ndio kirahisi ilibakia kama moja ya kona ambayo ningetumia KISWAHILI kirahisi! - ni nyongeza kidogo ya Jibu hilo hapo juu.


Pili, napenda KUBLOGU  kwa kuwa kunafanya nichangamshe akili na kuwaza mambo ambayo sio Profesheni yangu ukizingatia kuwa tokea MAZENGO HIGH School mpaka  kwenye vielimu vya juu yake zaidi  mpaka kwenye kazi engo yangu  zaidi iko kwenye UCHUMI na BIASHARA na kwa kuandika BLOGU ambayo haizungumzii UCHUMI na BIASHARA  nalazimika kuwaza mengine ambayo sikabiliani nayo mara kwa mara KIPROFESHENI  kila siku kwa kuwa najaribu kuandika kila siku angalau kwa saa MOJA kitu fulani.

Hilo hasa ndio maana utastukia niandikayo hapa  nitofauti na nilichosomea  na kwa  kuandika hapa naamini napata mwamko wa kuyatafiti na kujisomea hayo mengine ambayo SIKUYAENDEA SHULE.


Swali jingine niulizwalo sana hasa ikitokea nimetaja jina la sehemu za siri ZA BINADAMU  waziwazi  a.k.a HADHARANI hapa  kijiweni ni kuwa:


Simon huogopi itakuja kukurudi hii kitu unavyoandikaandika  tu mambo kwenye BLOGU YAKO ambayo kuna waaminio sio ya KIHESHIMA  hata ambayo labda  ni MWIKO kwenye jamii ya KITANZANIA kuzungumziwa HADHARANI hasa kama  iko siku utaamua kugombea UBUNGE ambao ndio DILI namba moja siku hizi la ulaji fastafasta au tu ukitaka kuomba kazi MBONGO ambaye ataku GOOGLE na kukuta  unaandika UJINGA?


Jibu:
Kama ulivyoona POST zangu naziita UjingaBUSARA na  naamini kwa hilo nakubali labda kuna UJINGA  naouandika HAPA ingawa  kwangu kuna BUSARA zake pia ndani ya UJINGA ndicho nachoamini. 

Kwa hiyo kwa vile naamini kwenye UJINGA HAKUKOSI BUSARA kwa afikiriaye anaweza kupata BUSARA huwa sitishiki na wapendao KUHESHIMIKA ambao hugeuka mpaka watumwa wa kutaka WAHESHIMIKE mpaka kuhofia kila wasemalo na kufanya kwa vipimo vya HESHIMA ni nini kwa WATU wengine ambao labda hata katika MAISHA yao HAWAHUSIKI.

Mie ukinidharau sawa na UKINIHESHIMU   mambo BIYE tu -hasa kama unagundua kuwa labda ni kazi za  UJINGA kusaidia watu kustukia BUSARA ni nini na ni kazi ya WASIOHESHIMIWA ambao labda nipo na MIMI  kufanya WAHESHIMIWAO kuonekana spesho na kwa vipimo vya watuonao wengine kuwa ndio tusiojiheshimu waweze kujulikana vizuri ni kwanini hao ndio wanastahili KUHESHIMIKA.

Na kuhusu nijihadhari na nachoandika ili baadaye kisije kikasababisha nikakosa ulaji- najua FALSAFA hiyo - ila naogopa sana kutumia falsafa ya kuogopa tu kwa nisiyoyajua kwa uhakika ya BAADAYE. Mtazamo wangu hilo ni swala la kutishana zaidi tu hasa ukigundua kuwa labda hakuna BINADAMU mwenye uhakika KESHO italeta nini kipya  katika maisha ya mtu.

Falsafa yangu ni ya KUISHI SASA - na nafanya kazi kwa bidii  na ukinikuta najirusha huwa  najirusha kwa bidiii vilevile -nikiamini  kila DAKIKA naijali na naiishi navyoiweza na ikiwezekana SAA HIYO HIYO hata kama bado  ni kweli si kwepi kuangalia kuwa siui uwezekano wa kuikabili BAADAYE kwa kujifunza MAUJANJA kielimu kila siku na kuangalia uwezekano wakutoua misingi ya mlo wa BAADAYE  kabisa maishanni.

Ndio,..
.... nahisi ningekuwa naishi TANZANIA ningekata nywele labda zaidi kwa kushindwa kuzihudumia hasa kutokana na VUMBI kuliko kuzikata  ili nifananefanane na wafanyakazi wa BENKI  ili wenye kuchukia NYWELE aina ya RASTA wasitishike sana kunipa kidude, ULAJI au tu kutonizingua sana na maswali kemu kemu.- NI jibu la swali :UNGEKUWA  na nywele staili hiyohiyo ya MARASTA  kama ungekuwa unaishi TANZANIA?

Na naamini zaidi katika KUJIAJIRI na katika hilo pia  nafikiri ningetafuta jinsi ya kuishi na staili ya nywele niipendayo kuliko kudanganya watu kuwa MAPANKI au BONGE la upara ndio  staili yangu. NI mambo ya baadaye haya lakini kwa kuwa mpaka sasa sijalazimika kwa sana kukata NYWELE ingawa BABA yangu hazipendi na hamuhusudu wala Bob Marley na kwa bahati mbaya mie sio wa kwanza katika familia kuwa na nywele staili hii.


Ndio,...
.... kidini mie naamini MUNGU mpaka leo ingawa mie sio RASTA KIIMANI  kama watu wafikiriavyo KIRAHISI  kwa kuwa tu falsafa na imani hiyo haipandi kutokana na kutoamini baadhi ya misingi ijengayo imani ya URASTA mpaka siamini sana ya HAILE SELASIE  maswala ambayo yanagusa MARASTA.:-(

Ndio,....
.... nimezaliwa kwenye familia ya mama Mmenonite - baba MLUTHERANI na kuanzia  ubatizo ,Sunday School mpaka kipaimara ni ndude nimezichezea zaidi kwenye ULUTHERANI ingawa Mchungaji Moses KULOLA alishawahi kuniokoa nikajisikia bonge la MLOKOLE kipindi fulani .UNAJUA  tena maswala ya kujaribu kumtafuta MUNGU tena.  Na  natokea kwenye famili yenye watoto watano na  katika hao kuna mpaka WASABATO kama dada yangu nimfuataye.

Ndio,...
... teknikale mie ni MUISLAMU kwa kuwa nilishawahi kuwa MUISLAMU na kuna waaminio kuwa  ukishaingia UISLAMU hakuna kutoka na kwa mtazamo wa hao  mimi ni MUISLAMU.Kwa kifupi nimenyuka madhehebu na dini kadhaa katika maswala.

Ndio,...
.... sivuti bange wala sigara ila ULABU ndio kilevi changu ingawa nafikiria KUACHA  na kuna wakati ilikuwa ni KILAJI na demu ndio moja ya vitu vinavyo malizia siku yangu ingawa hapo ni baada ya kumaliza kupiga muziki AMBACHO KILIKUWA KILEVI CHANGU -ambayo bado ni hobby yangu niifanyiayo kuanzia KANISANI  mpaka kwenye ROCK & ROLL clubs.

Ndio ,...
....kwa miaka kadhaa nilikuwa lead singer wa Progressive Rock Band ingawa nshapiga mpaka MAKWASAKWASA katika bendi za Kikongo , tukiachilia mbali DANCEHALL na Roots Reggae.Ndio, nimeacha maswala ya DEMUZ kama kilevi na DINI imerudi  kusaidia hilo kwa kuwa naamini huwezi kuacha kitu bila kukiziba na kitu kingine. Bai ZE  wey jumapili ijayo mie ni  Lector  na nisomacho ni kutoka Psalm 31:1-5 kutoka kwenye Old Testament na Galatians2: 19-21 mbele ya Kanisa ambalo linanisaidia kutopunguza muda wa kujisomea BIBLIA ambao kuna wakati  unahitaji kitu kikupemsukumo ili uendelee kusoma. Na nasoma KORANI pia kama kawa na chngamoto ni malumbano ya WATANZANIA ambao sikuhizi FASHENI ni kutishania mapigano kati ya WAKRISTO na WAISLAMU.

-Hilo hapo juu ni jibu la: Vilevi vyangu ni nini?

Ndio,...
... BABA ni MPARE na mama MJITA na nasikitika kikuongea lugha zote mbili hizo hazipandi vizuri ingawa nahisi nikijaribu kuzitumia bado kunauwezekano nikaopoa MCHUMBA  kwa kuzitumia kwa hiyo labda ukizitumia kwangu usishangae nikakuelewa vyema tu na kufanikiwa kukutukana kidogo ili upandishe jazba!:-(


Nafikiri nimejibu vya KUTOSHA hasa kwa MDAU   Jose wa Dodoma, Lucy na HASSANI na wengine  -ambao nimechanganya na kuwajibu wote kwa pamoja hapa  kwa kuwa e-mail na hamu ya kujua mliyoniuliza imetokana na KUNISOMA hapahapa katika TARALILA zangu za UjingaBUSARA.

NI  HILO tu na ASANTENI wadau kwa kunibwenga chembaz na maswali hayo na kwa mara nyingine ni matumaini yangu nimeshibisha hamu yenu ya kujua ndude kidogo zaidi kuhusu MIMI KINYANGALAKATA Simon Kitururu.

Na  MWISHO:  

Moja ya kitu nikipendacho kuhusu KUBLOGI ni kama hivi - WADAU  kufahamiana ambao labda TUSINGEFAHAMIANA.

TUKO PAMOJA!

Hebu Tito Puente aingilie kati na kubadili mchezo  kwa - Morning




Au tu Yerba Buena wamalizie tu kwakurudia tena -Guajira

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Rachel Siwa 12:48 am  

wawooo @kaka Kitururu hata nami nimefaidika sana kukujua zaidi na kunufaika,kujifunza kupitia wewe!

kweli wewe ni kisiki cha mpingo kaka!!umesahau kuwa wewe ni mfafanuaji mzuri sana wa mada,hasa maisha na malezi,japo ulikana wewe si mlezi/mzazi1.

Ubarikiwe sana na Mungu akujalie Mke mwema,mimi dada yako nahitaji sana nishuhudie Harusi yako na watoto pia!.Asante sana!.

Faith S Hilary 4:09 am  

Wow this is absolutely amazing! Sijapata kungumza na wewe kwa karibu (or private...) lakini nahisi kama nimekujua at least labda 50% hehehe. Shukran kwa wote waliouliza maswali na kaka Simon majibu yametoka aina yake. I love that!

Simon Kitururu 8:29 am  

@Rachel na Candy 1:Asanteni kwa kutonitenga hapa kijiweni!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP