Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAPUMBU aka makende/KORODANI ndio SOMO la leo la CHAPUCHAPU hasa kwa WANAWAKE hapa kijiweni!

>> Thursday, March 24, 2011

Tahadhari :SOMO linagusa swala kwa JUUJUU !:-(


Habari zenu WADADA!
Aah jamani nawasabahi JAMANI  mbona mmenuna namna hiyo?
Naomba TABASAMU kidogo basi!

AKSANTEEEE Dada zangu,....
... na moja kwa moja ngojea tuongelee mapumbu.!:-(

Ndio,...
...najua  kati yenu kuna watundu ambao TAYARI  mshawahi  kuona hii kitu wakati toto la KIUME linaogeshwa au hata kupapasa hiki KIFAA ,...
....tukiachilia mbali na hata kujua kuwa HII NDUDE  ikigongwa inauma kweli  kwa hiyo tayari ni wastaarabu na hamjaribu kubinya  au hata wakati wa ugomvi kupiga teke hiki kifaa  MAKENDE  kwa kuhurumia mchango wake kwa vizazi vijavyo.

Na nashukuru kwa hilo yani!

Ila bado ,...
...wanawake WENGI ni miongoni mwa watu wengi  wasiostukia kwanini  WANAUME wanajihadhari kubinywa KORODANI ,...
...na pia wasiostukia hiki kifaa hakiko kwa ajili ya UZALISHAJI TU  wa malighafi shahawa aka MBEGU za KIUME ambazo ni maarufu sana  kwa kuchafua mashuka kama tu kusababisha mimba zikilengwa kwenye tundu lenye yai  lihitajilo rutuba.:-( Hiki kifaa kina kazi zaidi ya UZAZI  aisee,...
..... kwa kuwa ni chombo kitengenezacho pia HORMONES aka HOMONI  ambazo hutumika kurekebisha mwili wa BINADAMU  kutokana pia na kuwa na mfumo  ujulikanao kama endocrine system au System of Glands  ambazo hutengeneza hizi Hormones na kuzimwaga kwenye damu ya mtu ambazo hurekebisha kuanzia UKUAJI wa MTU, anavyojisikia mtu (MOODS) , mpaka jinsi ni kwa spidi gani unasikia njaa kutokana na hizi HORMONES  kucheza na ndude METABOLISM ya mwili,...


....ingawa NDIO ,...
...kifaa HIKI hujulikana zaidi labda kwa mchango wake wa sperms au kwa lugha ya kitaalamu SHAHAWA na kwa homoni moja zaidi ya aina ya TESTOSTERONE  ambayo inafanya DUME akae kidume ,...
.... yani  fulu MIDEVU  na minywelenywele bwelele mwilini isababishayo hata gizani kama mjanja ukipapasa ustukie ulipapasalo ni dume RIJALI , misuli mikubwa na mpaka bonge za mifupa kiujazo pia,..
....kitu isababishayo BODE la njemba liwe tofauti kidogo na BODE la kimwana mrembo mwenye kiuno kama nyigu,...
...ikiwa na maana inasaidia DUME lisikae  KIJIKE - ki fulu bonge za titi.

Na ukitaka kuijua zaidi hii ndude ninliyopapasa mpaka hapa   ,...
....Testicle,....
.....Testosterone ,....
.......kitu kizima ENDOCRINE SYSTEM,.....
.......hormones ,....
.....au hata kitu Sperm aka Shahawa ,...

.....gugo aka GOOGLE tu hizo MSAMIATIZ,...
....ambazo ndizo nimechezanazo katika somo mpaka hapa MKUU kwa shule zaidi isiyo ya juujuu kama ya vidokezo tu niistuayo hapa KIADOADO.:-(

Lakini kwa kifupi ,....
... nafikiri tutakubaliana kuwa MAPUMBU ni muhimu aisee mdada!:-(
 Hebu tupate kwanza kielelezo cha hiki kifaa :

Hiki kifaa hutunzwa katika kifuko kilichoumbwa kwa mchanganyiko wa ngozi na misuli  ``SCROTUM´´  ambacho kazi yake kubwa ijulikanayo ni kuweka KORODANI kijoto chini ya joto la mwili kwa  kuwa  KENDEZ zikiwa na joto kama la mwili  mbegu za kiume zitengenezwazo huingia udhaifu na kufanya kidume  sio kila goli  lake  lina afya na nguvu  kwa kutokana na joto kuathiri  kitu kiitwacho na wabongao ung'eng'e - Sperm Count.

Na kutokana na hilo mpaka kuna wadaio bila USHAHIDI WA KITAALAMU kuwa labda  MIDUME ijihadhari na chupi aka VIFICHA NYETI vibadavyo sana na kuzuia kazi  ya  kifuko ya kusogeza makende mbali na mwili joto likizidi na kuyarudisha karibu na mwili kama kipupwe kimezidi  kushusha joto za pumbuz .


Hebu tukideku kipicha  kifaa:
Hapa ni kitu kikivutwa juu ikiwa kinabaridi iathiriyo joto litakiwalo katika kiwanda cha shahawa na na kikishushwa chini kidogo  kimnig'inio ikiwa joto la mwili ni kubwa zaidi kidogo kuliko lihitajiwalo kiwandani.

  • Na nadhani  unakiona wakati kimesogeza   BALLS karibu na mwili hapo kulia .


  • Na kikiachanisha KORODANI na mwili huteremka kama ionekanavyo hapo kushoto.Kazi hii ya kupandisha na kushusha GOLOLI hufanywa zaidi na Misuli ya cremester aka Cremaster muscle ambayo huvuta  pia makende juu kama MHESHIMIWA KIDUME ananyege na kitu kimesimama ,...
... kazi ifanywayo PIA  ili kulinda shehena za aina ya KORODANI zisiathiriwe  KATIKA KURUPUSHANI  hasa  wakati mheshimiwa anakula ngoma aka ANANGONOKA.Mpaka hapa nimepapasa,...
....Cremaster muscle,...
.....Scrotum,....
....na Sperm Count ,...
,....ambazo kwa shule zaidi wewe ZIGUGO tu  ukizingati katika taralila hii nazigusia kwa juujuu.:-(


Na kifuko aka KITUNZA MAKENDE  HIKI kinasemekana kuwa na undugu sana na Labia Majora kwa wanawake.Asanteni  WADADA,....
... na nimatumaini  kuna angalau jambo MOJA  ili taralila hii ifanikiwe labda mtalifanya na hilo ni angalau kujiuliza kitu kimoja ambacho kitazalisha  angalau MGUGO aka M-Google kitu kimoja zaidi KUTOKANA na TARALILA HIII  na kujua angalau kitu kimoja zaidi kuhusu hizi KENDEZI ambazo historia yake kwa UZALISHAJI na hata yakufanya MIDUME iote NDEVU  na kuwa na TITI ndogo ukilinganisha na NYONYO za WANAWAKE ,...
....  ni tokea enzi za ADAMU na HAWA.
SASA TARALILA inaegemea  kwa WANAUME zaidi ,...
..... na hii,...
.... ni KITU siriasi zaidi  hasa kwa kuwa inagusa zaidi  SARATANI ya Ze PUMBUZ!:-(

Hebu tuanze upya na  twende shule kuhusu MAPUMBU,...
...kwa msaada wa MWANADADA,...
..... Dr. Susan Jewell  kwa .....
Mdada SUSAN aendelee..Somo zaidi  kwa wanaume kuhusu kucheki hiki kifaa hasa kutokana na saratani ya kiaina ichezayo maeneo kwa kumdeku huyu MDADA akizidi kufunza katika hii-Testicle exam


Kabla sijaacha labda tucheki SHULE MCHANGANYIKO ,...
...hasa kwa  wazazi ambao wamepata mtoto wa KIUME  ambao labda inabidi wajue tu pia  kuna kitu kiitwacho-Undescended Testicle kwa kumsikiliza Dr Steven Friedman


Mpaka hapa kwa shule zaidi unaweza KUGUGO,....

....Undescended testicle,....
...Testicular cancer,..
... ambavyo nimevigusa kwa juujuu .:-(


NIMEACHA!
Samahani tunakumbushana tu  SWALA na  madhumuni ilikuwa nikuchokoza udadisi wako ili udadisi zaidi kujua zaidi kuhusu hii kitu  MHESHIMIWA,...

.....na kama umekwazika au hukujifunza kitu  KATIKA PROSESI  ya KUDAKA USHUSHAJI wangu wa HII ishu KI-UjingaBUSARA maana yake mlengwa wa TARALILA HII haikuwa wewe,...
... na kwa hilo SAMAHANI!!:-(!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mcharia 10:43 am  

Nawaza kwa nini kiungo hicho kina majina hayo yote. Mapumbu, Korodani, Kende, hasua.

Kuna mtu anaitwa "Raia Fulani" aliwahi andika katika jamii forum akiomba ushauri kuhusu Maumivu ya korodani, ilikuwa ni tarehe 12th March 2009 akasema:

Kwa muda sasa nimekuwa nasumbuliwa na maumivu ya kende ya kulia. Kuna muda maumivu yanakuja na kupotea.

Nimejaribu kujichunguza nikagundua kuna kauvimbe kadogo ambako nikigusagusa kinadischarge maumivu kuelekea juu.

Nimeshaona madaktari lkn wanasema hamna kitu wakati mi najua kuna katatizo.

WATOA MAONI WAKAANZA, HAPA NANUKUU BAADHI:

Wa kwanza; Hao watakuwa majirani wanakuloga. Wasiliana na ma-concord!

Wa pili; Korodani ndio pumbu au? Kama pumbu labda itakuwa ngiri hiyo.

Wa tatu; Mzee, pole sana kwa maumivu! Unajua tena maumivu kwenye sehemu hizo yanakosesha raha.

Maumivu ya kende yanaweza tokana na sababu nyingi tu. Mojawapo ni ya varicocele, Urinary Tract Infection, Epididymitis, Orchitis etc.

MWISHO WA KUNUKUU.
Na kuna maoni mengine mengi nimeyaacha.Kwa hiyo nipo MAWAZONI.

SIMON KITURURU 10:18 pm  

@Mkuu Mcharia:

Lakini nadhani tabia iliyoshamiri zaidi ni ile ya kuogopa kabisa kutaja jina la hiki kifaa kwa kuwa kuna waaminio ni matusi!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP