Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Stori ya MTANZANIA MMOJA mwenye NJAA na haki ya nani sio MJINGA!

>> Saturday, March 12, 2011

Ilikuwa ni usiku wa manane ,...
... na kama mara ya elfu kumi hivi ya kujigeuzageuza kitandani kwa HAMDALA  kutokana na kukosa usingizi hasa  kwa kuwa NJAA inamuuma na ndipo Hamdala alipofikia uamuzi  kuwa  kesho itabidi aende tu stendi ya mabasi ya pale Msamvu, Morogoro  ili kwa mara ya kwanza  ajaribu  kazi mpya ambayo tokea utotoni aliisikia kwa umaarufu wake sana  ambayo ni ile ya  kuwa KIBAKA a.k.a kwa ung'eng'e  PICKpocketing.


'''SHENZI KABISA huyo nyambisi ! Piga kibaka huyo! Mwizi huyo !Makende ya mama yake  mwanaharamu huyo  na leo ataipata msenge huyo!  Kuma la MAMA YAKE  lenye mapumbu   pumbafu kabisa huyo !´´ - ghafla ndio makelele yaliyotawala akili yake yatokanayo na kumbukumbu ya mara ya mwisho kushuhudia KIBAKA akilamkong'oto   kama miaka miwili iliyopita akiwa UBUNGO stendi ya mabasi ya kwenda mikoani  pale  Dar-es- Salam , akifunga safari yake ya mwisho kurudi kwa wazazi  wake Morogoro kwa kuwa maisha ya Mjini Dar-es- Salam yamemshinda  .

Siku hiyo ghafla ikarudi  upya akilini utafikiri  ni jana tu aliishuhudia !

Hata kifikira tu mbele ya macho alishuhudia bonge la KIPIGO cha kibaka ambaye  alimshuhudia  akijaribu kuiba ndizi za mwanadada mmoja msafiri  ambaye tetesi zilidai  alikuwa naye anaelekea kwao MADABA  akiwa mjamzito kutokana na kufukuzwa kazi yake ya  uhausigeli  na MAMA mwenye nyumba baada ya kudai HADHARANI kuwa ni Baba mwenye nyumba ndiye aliyempa mimba kutokana na kumgeuza kitoweo kila mama mwenye nyumba akienda kazini na watoto wakienda mashuleni.

Jasho likazidi kumtoka Hamdala kwa jinsi alivyokuwa anakumbuka kipigo cha Kibaka yule  ambaye ilifikia mpaka mdada aliyeibiwa ndizi hizo mbili  za  aina ya NDIZI kisukari kuanza kuomba watu wamuache Kibaka wa watu  kwa kuwa kashapata fundisho- ingawa umati wa watu ulionekana kunuia kuua kabisa kwa kudai wamechoshwa na vibaka.

´´Sitaki kukuona hapa kuanzia kesho!  Asubuhi nisikukute nyumba hii! Mimi nilimuoa mama yako na sio wewe kama unataka kaolewe na wewe na wanaume wenzako kama ilivyofasheni yenu nyie vijana siku hizi! . Ni mechoka kulea mitoto  mivivu kazi kula na kunya tu!´´ - ni sauti nyingine iliyojirudia tena na tena  mwa Hamdala AKILINI -huku akijiuliza hivi ni sahihi baba yake wa kambo yule kumtamkia yote haya mbele ya mama yake  ambaye anajua alimpenda baba huyo ndio kisa akaolewa naye wakati Hamdala bado mdogo.

Na alijikuta apatacho ni kuzidi kuchanganyikiwa tu  jinsi alipozidi kufikiria ni yapi  ambayo yamemgeuza hivyo  Baba yake huyo  wa kambo aliyemuoa mama yake  baada tu ya baba yake Hamdala kufariki  - ambayo ndio ya mwisho aliyosikia wakati anafukuzwa mezani asile kabla ya kwenda kulala kwa kuwa anaonekana ni mzigo tu   pale nyumbani tokea arudi kutoka Dar-es- Salaam  alipokuwa anajaribu kujiajiri kwa kuwa Mmachinga - kabla hajanyang'anywa biashara yake iliyokuwa ndio mtaji wake wote akiwa mitaa ya kariakoo akibangaiza -  na  mgambo waliomvamia  na kumnyang'anya kila kitu kwa kudai kuwa alikuwa anafanya biashara bila kibali na katika purukushani hizo  kujikuta hana kitu na kilichobakia ni nauli tu aliyojua angalau itamfikisha kwao Morogoro.


Ngo ngo ngo ! Hamdala akasikia mlango unagongwa  kwa taratibu na kufunguliwa kidogo  halafu ndizi mbili zikasukumizwa chumbani huku akisikia sauti ya mama yake ikinong'ona ``Mwanangu  angalau kula ndizi hizi  na ondoka asubuhi sana Mme wangu asije kunitesa zaidi na mimi . Lakini njoo kwenye  kama saa tano asubuhi akiwa kaenda kazini ili angalau ule vizuri kabla hujaenda kuchakarika. Mwanangu unajua tena mimi sina kazi na mume wangu ndiye nimtegemeaye kwa malezi na unajua hata akigundua hiyo kesho kuwa ulirudi kula  mie ntakuwa mashakani! Lala salama mwanangu!´´


Ingawa Hamdala alikuwa na njaa. Ndizi zile mbili zikawa zinazidi kumkumbusha jinsi yule kibaka katika stendi ya mabasi Ubungo ambaye nusura afe kisa ndizi mbili za kisukari.´´ Hivi hii ni alama iashiriayo na mimi nitapigwa vile nikiwa KIBAKA    kesho nini?´´-Hamdala alijiuliza.


Wakati  akiendelea kufikiria jinsi atakavyo anza  kukwapua pochi za wa mama  , waleti za wakaka walizozihifadhi kizembe na pia simu za mkononi kwa mara ya kwanza maishani mwake pale stendi ya  mabasi   Msamvu kesho yake, bila hata kujua akajikuta akipitiliza na kuwaza yote aliyopitia maishani .

Kwa mara nyingine akaanza kupitia kote alikoenda kuomba kazi kuanzia  za uhausiboi  nyumba ya jirani , kuhudumia bustani kwa mzungu,  kuomba kuchoma chipsi pale  kwenye baa ya Mangi, mpaka alivyojaribu kuomba kupiga debe kwenye mabasi ya Abood  kitu ambacho kote kwa sababu tofauti alionekana hafai kwa kukosa uzoefu  au tu kitu anachoanza kuamini kuwa ni kukosa kwake tu bahati maishani.


Akafikiria na wote wenzake waliomaliza naye Kidato cha sita ambao siku hizi anawakwepa kwa jinsi wanavyozungumzia maswala ya vyuoni ambako yeye kutokana na kukosa ada na pia ukweli kutokana na kusoma kwa taabu hakufaulu vizuri - stori zao kuona zinamzingua .

Na kwa muda akamkumbuka mpaka  demu wake wa zamani  ambaye demu huyo alimtema kwa kumuona Hamdala kutokana na hali yake ya kimasikini hana mpango na kuanza kuchukuliwa mbele zake  na wenye pesa .

Na karibu ALIE  pale  alipokumbuka mara ya kwanza mbele ya macho yake aliposhuhudia kuwa demu wake mwanana anachukuliwa na mtoto mmoja wa tajiri wa Kihindi pale Morogoro mjini  ambaye alikuwa anajua kuwa huyo jamaa anamchezea tu na wala hatamuoa wala kumtambulisha hata kwa ndugu au wazazi hasa kwa kuwa inajulikana wazi jinsi familia hiyo idharauvyo waafrika weusi na jinsi pia ijulikanavyo kwa jinsi yule kijana anavyojibosti  kuwa yeye banduabandua tu totoz  zikijilenga.

Na machozi  yakamtoka  kabisa alivyokumbuka jinsi alivyoishiwa nguvu kwa kushuhudia jinsi demu wake yule zilipendwa mwanana alivyoonekana kuridhika sana mbele yake alivyoopolewa na mtoto wa tajiri  na kuonyesha bila hata haya  furaha kupita kiasi kama mtu aliyewini bonge la bahati nasibu wakati  hata anashikwashikwa  tako  huku akifunguliwa mlango aingie kwenye  gari maridadi la yule mtoto wa Kihindi mbele yake Hamdala huku Hamdala akiwa hana la kusema na wala hata janja ya kufurukuta hana kutokana hasa na kujua akifanya purukushani ya kumgombania kimwana atapigwa hata na wapambe wa mtoto wa tajiri ambao kwa kujipendekeza wapo kila kona aendapo kutokana na kupigwa ofa za vya bure vya hapa na pale.

Bado  kimsikitishacho zaidi  ni  yale ajuayo kuhusu huyo demu wake wa zamani yaliyomkuta  siku hizi ingawa bado hasahau alivyoteseka kujaribu kumsahau ! Kwa kuwa  demu wake huyo siku hizi kalazimika kuwa mpaka  malaya wa waziwazi  kabisa ajiuzaye.

Na iliuma zaidi kukumbuka jinsi  demu huyo   alivyomkatalia alhamisi iliyopita tu kumgawia kidude kwa adoado kama tu kujikumbusha ZILIPENDWA kwa kudai kama anataka alipie kwa kuwa hawezi kumgawia bure huku ana watoto watatu wenye njaa na hana jinsi nyingine ya kujipatia  kipato kingine  akiwa karibu na nyumbani  ili kuishi yeye na watoto wake .

Na bado kwa shingo upande mpaka leo anakumbuka jinsi alivyofukuzwa pale  kwa kuwa mteja WA MPENZI WAKE HUYO WA ZAMANI alikuja na huyo kipenzi wake wa zamani alivyofikia kudai anajuta kuwa penzi lao halikudumu na asingependa kumuona tena kwa kuwa anamtia uchungu tu -  huku akisema aondoke haraka kupitia mlango wa nyuma kwa kuwa  hakutaka mteja afikirie kuwa hajajiswafi ya mteja aliyepita  kabla ya kumpokea yeye mteja mpya   . Kwa kuwa huyu mteja anamchezo wakutaka kumsafisha  hata kwa sabuni ya mbunju sehemu za siri hata masaa yote aliyobuku akihisi katoka tu kumuhudumia mteja mwingine kiutu uzima .

Na MTEJA HUYU  leo alikuwa kabuku  masaa mawili   atakayo kujivinjari naye kwa staili tatu  azipendazo - moja ikiwa ni chuma mboga ,.Ya pili ile sungura mjanja . Na ile staili mpya ya tatu ijulikanayo kama kutapatapa kwa bata mfa maji za kiuasherati kama tu zile nyingine za kimishenari POZISHENI -ambazo mteja huyu ananogewa nazo kweli na hakawii kulipia zaidi ya bei ya makubaliano.

´´Kokorikooooo!´´ ni mlio wa jogoo uliompiga Hamdala kama nyundo kuwa asubuhi imeingia . Na kwa haraka Hamdala akazigida zile ndizi mama yake alizomletea kisiri  usiku. Na  baada ya kujinyosha  akajisemea kwa sauti ya mnong'ono kuwa `` Leo ni siku yangu ya kwanza mie Hamdala kama MWIZI wa mifukoni na KIBAKA asiyeheshimiwa katika jamii! Eee MUNGU nisaidie!´´

Na  huo ndio ulikuwa mwanzo wa maisha mapya ya Hamdala kama KIBAKA  .

Na baada ya miezi tu kwa jinsi alivyofanikiwa sana kwa kuiba sana simu na na Pochi za akina mama ambavyo ndio ilikuwa ndio speshalaizesheni yake- sasa hivi yuko katika  mipango kabambe na baadhi ya marafiki zake wawili wengine ambao alikutananao hapo hapo MSAMVU stendi ya mabasi   pale MOROGORO wote wakiwa ni vibaka na wezi wadogowadogo,...
...kwa mara ya kwanza wanafanya mkutano wakujaribu kuangalia uwezekano wa kuingia hatua nyingine katika maisha waiitayo kiswanglish ``BIG TIME ´´ ambayo sasa hivi hiyo ni kujaribu  ``UJAMBAZI!´´



Swali:
  • Kwani unafikiri VIBAKA wengi hujitakia kuwa vibaka Tanzania?
  • Na si inasemekana kwa BINADAMU mwenye akili hufanya yawezekanayo tu kwao -na moja kwa kawaida huanzisha jingine?

Ndio,...
... kuna uwezekano kama tu WATANZANIA wenye njaa ambao sio wajinga wastukiavyo ulaji uko kwenye UBUNGE au siasa kwa ujumla siku hizi ,...
.... labda ni WATANZANIA wenye njaa  na ambao sio wajinga haohao katika kutatua kitu FULANI  hufikia pia katika uamuzi wa kuwa VIBAKA au hata MAJAMBAZI yote ikiwa tu ni matokeo ya KIBANO na kutumia akili  kitu kifanyacho wafikie kwenye uamuzi KIAKILI ambao kwa watu wengine wasio tembelea viatu  vyao  SI MZURI.:-(

Swali la kizushi:
  •  Si inasemekana kuna WAHESHIMIWA wenye njaa zao fulani wasio VIBAKA au MAJAMBAZI  ambao ni wezi hata kuliko VIBAKA na MAJAMBAZI ingawa wizi wao wanatumia kalamu  ambao nao ni kwa kuwa walikuwa na njaa na elimu zao  ambazo kuna namna zimewafunza KUIBIA WANANCHI sio UJINGA?
  • Kwani unafikiri KIBAKA mzuri kama tu  JAMBAZI mzuri huwa hawana AKILI?
  • Hivi MWENYE NJAA na ASIYEELIMIKA  hapa TANZANIA ni nani unafikiri ni hatari zaidi?
Na ndio ,...
....  stori ya HAMDALA ni ya kutunga tu .:-(


Ni wazo tu hili hata kama limepinda  MHESHIMIWA!:-(
Jumamosi njema MDAU!

Hebu tumtembelee J Dilla katika studio yake..



J Dilla amwage-Think Twice



Common amuongelee J Dilla



James Dewitt Yancey aka J Dilla aka Jay Dee aendeleze kulainisha kwa -Won't Do



Au tu Jay DEE amalizie tu kwa kuja na Havoc & Raekwon wamalizie kwa - 24K Rap

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 8:33 pm  

Nimejifunza mengi sana kutoka ktk hii hadithi. Japo wasema ni ya kutunga ila inaonyesha umefanya kazi kubwa sana ya kuitunga.

Christabell

Simon Kitururu 12:47 pm  

@Christabell: Asante kwa kunisoma na kunitembelea hapa kijiweni Mkuu!

Na nanafurahi umenipata nilichokuwa nalenga ingawa sio kweli ilikuwa ni kazi kubwa hivyo kuja na tungo hii kwa kuwa ni tungo tu yakujitakia mwenyewe.

Karibu sana tena na tena Mkuu hapa kijiweni!

o'Wambura Ng'wanambiti! 3:18 pm  

Dah...Hii imetulia kabisa mkuu!

Si kila aliye jela ana hatia you know?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP