Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati MTU halisi UNAYEKUTANA NAYE na AKUCHEKEAYE kajificha nyuma ya KITU!

>> Wednesday, March 30, 2011

Kuna wajifichao nyuma ya UREMBO,....

.... na kama ni wajinga utachelewa kujua kwa kuwa UREMBO ndio uustukiao.:-(

Kuna wajifichao nyuma ya HARAKATI,...
..... na  wanachofanya ni kufanya uoanishe UTU wao na HARAKATI zao  wakati  wao kama WATU kuwa ni ambalo hawataki liwe ni jambo listukiwalo.

Na kuna wajifichao katika DINI,...
....na wanaweza kuwa wafanyalo ni kutumia DINI na hata MUNGU ili kukurusha kustukia  yao BINAFSi ambayo  yanatisha  kama yakiwa ndiyo moja ya ambalo USTUKIALO

Kuna wajifichao nyuma ya KAZI,...
..... na ukitaka kuwaudhi ruka kutamka ni MAMENEJA wa kitu fulani  kwa kuwa ukiondoa UMENEJA WAO na UONGOZI wao wa  CHAMA labda hakuna lao BINAFSI kama WATU BINAFSi  wajivunialo.:-(


Kuna wajifichao nyuma ya SHULE zao,...
.... na ni tusi kwao kutowaita MADAKTARI hata kama NI UDAKTARI WA KUPEWA  kwa kuwa hicho ndio kithibitisho tu kuwa pamoja na yao yakijinga angalau waliwahi kwenda SHULE au wanaheshimiwa KISHULESHULE  ingawa labda ni vigumu  kwenye hilo kama ni BUSARA za USOMI wao ndilo kustukia  ulengalo .:-(


Kuna  wajifichao nyuma ya WATOTO , mme au WAUME zao,...
.... kwa kuwa yao ili wajisikie MAISHA yana maaana  ni WAUME, watoto, WAZAZI   au WAUME zao waaminikao kuna kitu wamefanikiwa ndio watakalo liwe listukiwalo.:-(


Swali:
  • Umeshawahi kukutana na mtu ambaye hatumii kitu KUJIFICHA nyuma yake ili angalau  kukujengea jinsi UMTAFSIRIVYO?

Ndio,...
.... labda kila mtu kajificha nyuma ya kitu fulani  ,....
... na ukijua ukweli juu ya MTU ,...
.....kiutu labda MALAYA ndiye MLOKOLE na MLOKOLE ndiye MALAYA !:-(


NI wazo tu hili MHESHIMIWA!


Hebu ghafla Loketo waingilie shughuli kwa -Extra Ball



Las-Ketchup wahamishe mashambulizi kwa -Asereje



Au tu Don Omar arudie - Danza Kuduro

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP