Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Bado ukweli uko pale pale kuwa SIGARA , bangi, kidude, mbirimbi , POMBE mpaka NYANYA zilizokolezwa madawa ya kuua wadudu LABDA si nzuri kwa AFYA yako!:-(

>> Saturday, April 02, 2011

CHA kusikitisha ni kwamba,....

.... labda karibu kila kitu si kizuri kwa afya yako,....
.... ukitazama maswala kwa kuzingatia kuwa ,....
.... karibu  MAZAO yote sehemu nyingi kutokana na madawa na mambolea yachumvichumvi  NA MADUDE MENGINE yatumikayo ,...
... tukiachilia jinsi WATAALAMU WA SAYANSI  tuwaaminio kuliko WAGANGA WA KIENYEJI wazidivyo kuchezea mazao  kwa KUYAKOROFISHA KIJENETIKS aka Ki- genetic modification ukiyachunguza,...
... labda hakuna lililosalama kihivyo hata kama unatumia kondomu.:-(



Kwa hiyo labda wakati unanyooshea watu kidole,....
... kumbuka LABDA ufanyacho kinamadhara yaleyele.:-(

Swali:
  • SI kuchambia maji labda kuna madhara yaleyale ya kuchambia TISHU ingawa mchambia mchanga  labda ndiye aonaye tofauti?
  • Unafikiri afanyaye kitu makusudi huku akijua madhara yake na afanyaye bila kujua kama akimbiliaye KULA kula mboga za majani  ambazo HAJUI  tu kuwa zimekolezwa madawa GANI kisawasawa YAFANYAYE mtoto mzuri wakike awe TASA kama tu RIJALI awe na udhaifu wa KUDINDISHA MTALIMBO na ni afadhali tu angejilia NGURUWE ki nyama ya kitimoto-  nani ni  anaafadhali?

Nawaza tu!:-(


Hebu Carlos Santana arudie - Oye Como Va



Au tu Carlos Santana aje na Rob Thomas warudie - Smooth

13 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mzee wa Changamoto 2:06 pm  

Duh!!!
Labda ni MADAWA YA KUUA WADUDU ndiyo yanayokufanya uwaze uwazayo na kutuwazisha vema ufanyavyo.
Labda dawa za kuua "vidudu" zimetusaidia.
Labda .......

Yasinta Ngonyani 2:33 pm  

Lakini sasa huyo nguruwe anakula chakula gani?

Simon Kitururu 2:41 pm  

@Rasta Mubelwa: DUH!
@Mtoto Mzuri Yasinta:Kwani Nyuki anakula nini ambaye hafugwi na WATU?:-(

Yasinta Ngonyani 3:00 pm  

Mt. Nyuki anakula unga unga wa maua na miti.Lakini nguruwe anahitaji kulishwa na vyakula vingi alavyo nguruwe ndivyo tulavyo sisi wanadamu. ....nijuavyo mimi

Simon Kitururu 3:09 pm  

@Yasinta: Sasa mbona uliniuliza kama una majibu?:-(

Ila unauhakika Adamu na Eva walikuwa wanafuga nguruwe au tuamini tu kuwa Nguruwe wanahitaji BINADAMu wawalishe na wakijitegemea watajipikilisha na UGALi itakuwa chakula chao?


Usikonde Yasinta! Nimepata hoja yako na kumbuka asili ya nilichokuwa naongea kwenye TARALILA ni MAWAZO tu!:-(

Na katika kuwaza kwangu bado naamini kuwa kuna wanyosheao vidole watu wengine kuwa wafanyayo si AFYA wakati hao wenyewe wafanyayo hayana AFYA!:

Ni hilo tu!

Tabasamu basi Kipenzi!:-(

Mwanasosholojia 4:00 pm  

Teh!Nimeipenda ya Adam na Eva...nafikiri kulikuwa na "nguruwe pori", hawa hawalishwi wanajilisha wenyewe, nawaza tu Mt.

Yasinta Ngonyani 4:16 pm  

Sasa kama hao nguruwe wanajilisha/walijilisha basi watakuwa nao wanakula wanakula chakula kilichopuliziwa madawa pia.. kutabasamu ha ha ha haaa:-(

Simon Kitururu 4:23 pm  

@Yasinta: Mmmmh!

Kwahiyo unataka kusema Mchicha wenye MADAWA na NGURUE aaliyekula mchicha wenye madawa ngoma DROO ki kusaidia watu wajisikie kufakufa?
@Mwanasosholojia:
:-)

Yasinta Ngonyani 4:41 pm  

nanukuu "Swali:

SI kuchambia maji labda kuna madhara yaleyale ya kuchambia TISHU ingawa mchambia mchanga labda ndiye aonaye tofauti?
Unafikiri afanyaye kitu makusudi huku akijua madhara yake na afanyaye bila kujua kama akimbiliaye KULA kula mboga za majani ambazo HAJUI tu kuwa zimekolezwa madawa GANI kisawasawa YAFANYAYE mtoto mzuri wakike awe TASA kama tu RIJALI awe na udhaifu wa KUDINDISHA MTALIMBO na ni afadhali tu angejilia NGURUWE ki nyama ya kitimoto- nani ni anaafadhali?" mwisho wa kunukuu kwa hiyo labda tuaache kula vyote...najiuliza tu kwa sauti

Simon Kitururu 4:47 pm  

@Mtoto Mzuri Yasinta: Mmmmmh!

Yasinta Ngonyani 5:04 pm  

Nini tena mbona mmmmmhhhh kwanini Mtakatifu wewe? Ningekuwa na .... we acha tu....

Simon Kitururu 5:07 pm  

@Mtoto Mzuri mwenye macho ya GOLOLI Yasinta: MmmmH ! ,....
.....ilikuwa ni mguno tu wa kuashiria umenifikirisha!:-(

SI unajua Mguno MmmmmmH!,...
...dhambi zake ikiwemo kukubali , KUSIKIA utamu, ....nk?

Yasinta Ngonyani 5:10 pm  

ok! kumbe:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP