Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nilipofika TANZANIA nikakuta RAFIKI yangu JESTER niliyewahi KUKUONYESHA PICHA ZAKE kafariki DUNIA,...

>> Friday, April 08, 2011

.... huo ndio ulikuwa mwanzo wa stori aliyokuwa ananipa RAFIKI yangu MMOJA   kwa jina nammezea!


``Nilihangaika wiki nzima kumtafuta JESTER  na nikaambulia kumuona tu AGNESS na familia yake wako shwari tu. Halafu  JOHN na  Wiliam watoto wa AGNESS  wamekua kweli!´´-akaendelea rafiki yangu.

Ila tatizo langu ilikuwa nimuone JESTER ambaye nili FOLI IN LAVU naye kwa miaka mingi  tokea mdogo  yani. Na nia hasa ya kumuona ni kwa kuwa  nilisikia AGNESS alimfukuza JESTER kwa kuwa alianza kuzeeka na siku hizi yuko  na Prinsi HARRY.

``Na nashangaa ni kwanini Prinsi Harry hajawaua John na William alipoanza kutembea na AGNESS.Kwa kuwa kwa kawaida MADUME wapya huua watoto wa BABA mwingine wakati wanammendea mama yao.´´- rafiki yangu alimalizia sentensi hiyo huku akionekana yuko ndani ya mawazo mazito kweli.



DUH!

Alipofikia hapo HAKI YA NANI tena  ndio akili yangu ikagundua kuwa aongeleacho sio WATU .:-)

Jamani kuna watu wanapenda WANYAMA na usipoangalia unaweza kutostukia TOFAUTI wakati  wakiwaongelea hao WANYAMA na wakiongelea WATU ,...
....kitu kiwezacho kufanya ukadhania stori upewazo ni za WATU kumbe aongelewaye ni NYAU!:-(


Yani nilichanganyikiwa nilipoanza kupewa stori hii na RAFIKI yangu huyu  hasa PALE alipogusia kuwa JESTER hata picha zake kashawahi kunionyesha.


Nanilii kwa kifupi:

Huyu jamaa rafiki yangu ni Muingereza fulani ambaye anapenda sana WANYAMA  na karibu kila mwaka lazima aende KENYA na TANZANIA  kufuatilia wanyama awapendao  hasa SIMBA na anamchezo wa kuwatungia majina.


Jamaa anapenda sana SIMBA na hiyo stori  aliyokuwa ananipa ni ya SIMBA dume amuitaye JESTER ambaye kastukia kafariki ,...
....ni SIMBA ambaye alikuwa anamfuatilia tokea mtoto  , alipokuwa rijali na kuwa DUME la kundi lenye kuongozwa na Simba jike  amuitaye AGNESS na mpaka kupikuliwa na DUME jingine ambalo ndilo dume la wakati huu katika kundi la Agness aliitalo Prince Harry.

Unajua tokea kuanza kuangalia NATURE CHANELS kwenye TV nilistukia kuna watu kibao hasa wamagharibi wakiwa wanaongelea WANYAMA kama huoni wanachoongelea unaweza kufikiri wanaongelea WATU  kwa jinsi waelezeavyo mahusiano ya hao wanyama au hata majina wayatumiayo kutofautisha hao wanyama.

Ila leo nilipatikana kwa kuwa HAKI ya nani wakati huyu jamaa anaanza stori yake nilidhania anamuongelea MTU nimfahamuye. Na haki yanani mpaka alipotoa picha za AGNESS ambaye ni mjamzito na familia yake chini ya ulinzi wa Prince Harry ndio nikawa 100% nauhakika kilichokuwa kinaongelewa ni SIMBA na wala sio MTU.

Swali:
  • Ushastukia  wamagharibi waongeleavyo WANYAMA ifananavyo na waongeleavyo WATU hata kwenye vipindi vyao vya  wanyama?

R.I.P Jester!
Samahani RAFIKI kwa kushea hadharani STORI ya jinsi ulivyonizingua na stori za JESTER  najua huwa unapitia hapa .:-(

Kwa wengine BAADAYE basi!


Au kama ni mpenda JAZZ tubadili wazo kwa kujikumbusha kifo cha nguli wa JAZZ Charlie Parker katika -

The Death of Charlie Parker



Histori zaidi kwa wapenda miziki -
The Charlie Parker Story



Hebu kwetu wapenda muziki wa jazz Charlie Parker atusafirishe maishani kifikira kwa - All the things you are




Au hebu tu twende shule ;

Jazz Guitar - Chromatic Lick Lesson

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 8:17 am  

Duh, mkuu nilipoanza kusoma hii stori ni kaanza khamanika, yaani ukimpenda mama mtu unaua watoto wake...nikasema ni wapi huko, oooh, kumbe ni porini, kwa mfalume Simba.
I like it..SHUKURANI MKUU. Kwani niliposoma hii stori nikakumbuka mjadala uliokuwepo ndani ya daladala, Jamaa walikuwa wakiwaelezea Wazungu jinsi wanavyopenda wanyama, wakasema ndio maana mzungu anaweza kufuga simba, chui nk, na asizurike na huyo mnyama.
'Lakini mwafrika asivyopenda wanyama, hata mbwa, au paka wanamuogopa mwafrika, ndio maana akionekana kwenye nyumba ya mtu , mbwa anabweka kwa hasira...lakini akionekana mzungu mbwa anaguna...'
Mimi nilitabasamu na kutafakari sana huo usemi, ...`kuwa eti waafrika hatupendi wanyama, ndio maana na wao hawatupendi...'je kuna ukweli ndani yake, sijui!...angalia watu tunavyouana kama kuku, (kumbuka sote ni wanyama)

Simon Kitururu 11:40 am  

@M3: Mimi nafikiri kuna mambo mengine mengi yafanyayo ionekana Wamagharibi wanapenda sana WANYAMA. Natumia neno Wamagharibi kwa kuwa nimestukia jambo hili lipo sana Magharibi kwenye watu wenye ahueni kiuchumi kwa kuwa kwa wazungu wa mashariki ambao wengi wao pia wana kibano kiuchumi jambo hili halipo sana.

Kwa hiyo naamini jambo kama tu uhakika wa maisha unaweza kufungua zaidi uwanja wa Binadamu kuona umuhimu wa viumbe vingine.

Fikiria kwenye nchi kama Finland yenye huduma ya afya za mbwa na paka ki wingi wa madaktari ulio sawa na wa BINADAMU usingepewa umuhimu kihivyo kama matatizo ya huduma ya afya za watu zingeadhiriwa angalau kibajeti za nchi kama paka na mbwa wangetengewa fungu la pesa za huduma.

Nachojaribu kusema ni kuwa. Tanzania wakati shilingi mia tano tu za kikombe cha BABU ni shida , hapo huwezi kutegemea huyo afukuziaye shilingi mia tano kwa ajili yake kwa shida awaze sana afya za njiwa zikoje mkoani Kigoma.

Nanukuu``'Lakini mwafrika asivyopenda wanyama, hata mbwa, au paka wanamuogopa mwafrika, ndio maana akionekana kwenye nyumba ya mtu , mbwa anabweka kwa hasira...lakini akionekana mzungu mbwa anaguna...' ´´-mwisho wa nukuu. Hili si kweli na ndio maana Mbwa kibao wakali kwa watu utakuta wapo tu pia kwa hata polisi wa ulaya na hasa kwa ajili ya kukabili wazungu haohao.


Na kihistori hasa ni juzijuzi tu katika VICTORIA time ndiyo hata ulaya kuwa na peti dogs na maswala ya kuwa na mambwa koko kwa ajili ya kuwa na mbwa tu ndani ya nyumba hata katika nchi kama Uingereza ndio ilianza kuwa kawaida.Kabla ya hapo ni kama tu ilivyo Afrika , Mbwa alikuwa ni wa ulinzi, kuwindia au tu shughuli nyingine kama vile kusaidia katika uchungaji wa mifugo na kadhalika.

Na ni kweli inasikitisha jinsi hasa Afrika tunavyouana kama KUKU. Lakini,... chunguza historia ya sehemu yoyote duniani, kuanzia UCHINA, Japani ULAYA mpaka MAREKANI utastukia sio muda mrefu walikuwa wanachinjana wao kwa wao kwa sana tu na labda hata kuszidi ilivyo sasa hivi Afrika.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP