Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MFUMO huweza kumgeuza NYERERE kuwa KIKWETE na KIKWETE kuwa NYERERE!:-(

>> Monday, June 27, 2011

Pamoja na UMUHIMU wa nguvu na akili za MTU BINAFSI,...
.... kwenye MFUMO UFANANAO hata ukiwa na watu wawili tofauti mpaka kiakili na kiitikadi  kama Rais OBAMA na Rais BUSH,...

....katika MFUMO uleule unaweza kukuta matokeo ya watu hao WAWILI wawazao tofauti YAKAFANANA kama tu hayatakuwa ni YALEYALE.:-(

Swali:

  • Si unajua ni kwanini ili UINGEREZA iendelee kubakia UINGEREZA ileile -pamoja na kubadili MAWAZIRI WAKUU ili kuendeleza mkao uleule serikali kwa kawaida hufuata MFUMO uleule wenye MAMALKIA na WAFALME watokao katika familia ileile?
  • Na si unajua kama MFUMO ni MZURI  hata kiongozi mjinga anaweza asifanikiwe kufanya UJINGA?


Ndio,...
....katika mfumo bora unaoeleweka hata kwa NG'OMBE,...
.... yasemekana  HUFANYA ni vigumu kwa ng'ombe hao kupotea ZIZI,...
... kama tu silabasi nzuri  iwezavyo  kuongoza MWALIMU  asiyejua cha kufundisha aweze kuchagua  kufundisha kwa wanafunzi  yenye MANUFAA!:-(

Ni wazo tu hili KINGUNGE!

Hebu DE LA SOUL watulize kwa-Baby PHAT





Ndio ,...
... bado niponipo bado yani!:-(


























3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 12:36 pm  

Mfumo, mfumo...mkuu hapa umenipa wazo la kutafakari kuwa huko Arabuni na jamii yake kuna maandamano ya kuondoa `mfumo wa ufalme'...sasa huko uingereza vipi...maana naona kama ni mfumo uleule wa usultani...au kwa vile kuna `waziri mkuu anachaguliwa kidmokrasia? nimewaza tu mkuu!

malkiory matiya 2:24 pm  

Kitururu: Hapa umenigusa, nchini kwetu Tanzania mifumo kuanzia ya elimu na ya uongozi hainabudi kuangaliwa upya kama kuna nia ya dhati ya kuleta maendeleo.

Simon Kitururu 4:27 pm  

@Mkuu M#: Ukichunguza kiitwacho ni DEMOKRASIA kinachofanya MAREKANI iitwe ni nchi ya DEMOKRASIA labda kikibadilishwa jina sio DEMOKRASIA hicho.:-(

@Mkuu Malkiory: Yani umenena Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP