Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa kuna WAHOFIA hofu!

>> Wednesday, June 08, 2011

Ndio,...
... kiogopwacho kikubwa ni WOGA wenyewe tu yasemekana.:-(

Swali:
  • Unafikiri kitishacho katika WOGA sio HOFU yenyewe tu zaidi ya KITU  kisingiziwacho kutisha kizalishacho kiogopwacho ambacho ni HOFU?
  • Kwani unafikiri huwa unaogopa nini HASA wakati UNAOGOPA?


Ndio,...
... labda KITU husingiziwa tu katika swala zima la KUTISHIKA,...
.... kwa kuwa kitesacho waoga ni HOFU YENYEWE na wala sio KITU hata kama hapa tutageuza hoja iwe ni woga wa jehanamu ambayo hakuna ajuaye kikweli machungu yake !:-(


Ni wazo tu hili MKULU!

Hebu tugewe tena Shikisha na Sipho Hotstix Mabuse



Au tu Sipho Mabuse arudie tu na - Jive Soweto



Simon Mahlathini &The Mahotella Queens wabadili mchezo kwa - Mbaqanga




Kabla Simon Mahlathini & Mahotella Queens hawajamalizia tu kwa-I'm In Love With a Rastaman


4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:27 am  

Ahsante kwa soma hil: swali je kuna labda sababu ya mtu kuwa mwoga kwa hajui la kufanya anaogopa kutetea upande mmoja? :-(

Goodman Manyanya Phiri 5:52 am  

@Yasinta

Barabara! " ...sababu ya mtu kuwa mwoga..hajui la kufanya..."

Kwa namna ingine: UOGA NI NDUGU YAKE UJINGA!

Ushauri kwa maoni yangu: Kwanza tukubaliane kwamba siku ya kufa utakufa tu, ikiwa kwa panga, risasi, sumu, vijidudu au virusi fulani.

Lakini, kabla ya hayo yote, kuwa jasiri, tetea haki, fanya kazi kama kawaida yako. Ukiwa mwoga basi wewe mtumwa na mwenye kuharakisha kifo chako kwa magonjwa tele ya nyongeza, kama magonjwa ya akili kama DEPRESSION, PHOBIAS, OBSESSION, HYPOCHONDRIA, PSYCHOSOMATIC CONDITIONS, ETC.!)

emu-three 12:19 pm  

Uwoga unajengwa akilini kwa kuzania ubaya utaotokea, na hili linawaathiri wengi hata kupata magonjwa ya moyo!
Juzi juzi tu maeneo ya kwetu kuna watu wamekufa kwasababu ya kusikia mlio wa mabomu yakiangamizwa...sababu kubwa ni hofu!
Swali ni je hofu na uwoga zinakwenda pamoja?

Simon Kitururu 2:05 pm  

Asanteni wote jamani!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP