Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

AIBU GANI HII BADO INAENDELEA KULIKUMBA TAIFA LETU!

>> Monday, October 17, 2011

Jeshi la Polisi nchini (PT) kupitia Inspekta Generali wake Said Mwema(Pichani) imetangaza dau la Shilingi Milioni 5 kwa mtu yeyote atakaefanikisha kupatikana kwa mtu aliyemjeruhi mtoto Adam Robert (14) ambaye ni Albino huko Geita ambapo mtu asiyejulikana alimvamia mtoto huyo na kuanza kumkata kata mikono na kisha kutoweka na vidole vya Albino huyo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia mwishoni mwawiki katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang’hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona vitendo hivi vinaendelea kutokea na mwisho wa siku jeshi linataka kutumia fedha za walipa kodi kwa ajili ya kuwapata wahalifu hao, mi nadhani hii njia sio sahihi, sidhani kama Jeshi la polisi wanashindwa kuwapata hawa wanaowatuma wahalifu kwenda kuwadhuru maalbino hawa. Jambo la msingi hapa sio kutangaza dau ni kuhakikisha wale wanaowatuma ndio wanakamatwa na ninaamini jeshi la polisi likishirikiana na usalama wa Taifa inawezekana kuwakamata hawa na kuwatokomeza kabisa, usalama wa Taifa wanafanya kazi gani kama sio pia na kuangalia usalama wa Watanzania hawa! 
Ni aibu kubwa kwa Taifa letu vitendo hivi vinavyoendelea.


Nimetumiwa na:
Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 10:49 pm  

Ni aibu kwa kweli, yaani nchi imekuwa haina mbele wala nyuma...aah!!

Poleni wahanga wa tatizo hili..

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP