Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa MOJA ya janja ya MAZINGAOMBWE ni kukuonyesha hiki ili USIONE kile!

>> Saturday, October 15, 2011

Hebu tuanze kupapasa ndude kwa KISWANGLISH:

Janja za wanamazingaombwe zinawekwa katika makundi matatu;
Misdirection, Illusion and Forcing.

 
Katika MISDIRECTION siri ya tumizi hilo ni kwa kuwa  yajulikana kutokana na udhaifu wa UBONGO wa Binadamu,...
.....na focusing on one thing can make a person  oblivious to other things that would otherwise be obvious.

Kwa hiyo,...
....misdirection lies at the heart of magic. It is the art of diverting the audience's attention away from  the act itself. In neuroscience terms, misdirection relies on the fact that the brain has a very limited supply of attention.

Ndio,...
.....na kuchekelea kanyau ni noma kwa kuwa ,.......
....  another mysterious way of manipulating attention of a person  is with humour.



Na achekaye wakati anacheka,...
... wakati huo  hawi makini katika kuangalia hata vya wazi mbele yake.
.........kwa hiyo  akuchekaye wakati anachekelea kanyau huo ndio wakati  rahisi kumficha kitu  cha wazi mbele yake hata kwa mfano  badala ya kujifuta mdomo unaweza wakati huo kuchokonoa pua na kuondoa kamasi lililokuganda bila kustukiwa.:-(

Na another key tool in the magic repertoire is ILLUSIONS, particularly cognitive illusions. Hizi zina  rely on the fact that much of what you think you see is actually invented by your brain.

Na,....
...perception is not about capturing a full picture of reality, but taking snapshots of the world and making the rest up.

Kwa hiyo,...
....MENGI  ufikiriayo unayaona MKUU ,..
... inasemekana hutungwa tu UBONGONI mwako.:-(

Sasa tukiacha kuzunguka MBUYU ngojea tu niingie katika nataka kusema nini katika UjingaBUSARA huu:

Okei,...
... nachojaribu kusema,....
...kumbuka UONACHO kama kuna mtu anakuonyesha hata KISIASA labda ota machale kwa kuwa labda uoneshwacho ni silaha tu ya kukufanya USIONE jambo kwa kuwa bize katika kuangalia jambo jingine.

Swali:
  • Wabongo mnakumbuka BABU wa LOLIONDO alivyoondoa makali ya hata mambo mengine katika siasa za Tanzania?

Okei,....
.... nachojaribu kusema,...
.... kumbuka  wakati MTU anacheka kuna wafumbao mpaka macho na hapo tukiruka kitendo cha kuchekelea hutuliza mtu katika kustukia mambo.

Swali:
  • Huja stukia ZE VICHEKESHO hata kama sio vya ZE Comedy ni muhimu kwenye mihadhara fulani yenye waheshimiwa KUHUTUBIA ambayo hutumiwa hata katika HOTUBA na Waheshimiwa akina Rais NYERERE wenyewe pia kwa dhumuni hilohilo kiaina?
  • Na kama umeenda kwenye mazingaombwe si ushastukia huwa unachekeshwa mara kwa mara na mwana mazingaobwe ?

Okei,....
... nachojaribu kusema,....
.....kumbuka kuwa ukishawishiwa na kushawishika  wala huhitaji kuona picha nzima kuwa jamaa aingizaye mkono mfukoni afanyacho ni kufungua zipu tayari kuchojoa.:-(

Swali:
  • Kwani unafikiri ukishahisi unaibiwa KURA unahitaji kuona kabisa kura ziitolewavyo kwenye kisanduku cha kura au tu kumuona uhisiye ni mwizi wa kura pembeni ya kiboxi  manyoya cha KURA inatosha?

Ndio,....
... wazo limepinda na sijajadili kikugusagusa kitu FORCING kama itumikavyo na WANAMAZINGAOMBWE ingawa wote twajua Mwanamazingaombwe hata achezaye na KARATA huwa akimuambia mtu achague KARATA bila yeye kuiona ,....
.. afanyacho ni kum-FORCE achaguaye KARATA kuamini afanyacho ni chaguo lake na Mwanamazingaombwe hajui kuwa kifanyikacho na KADI ya karata atakayochagua Mwanamazingaombwe anaijua kwa kuwa ni yeye aliyemchagulia hiyo kadi  MTU hata wakati anamwambia mtu achague Hiyo KADI ya KARATA!:-(

NIMEACHA na ndio ni RUKSA kutonielewa!:-(
Jumamosi NJEMA Mheshimiwa!

Hebu tudeku-Selective attention test ile iliyoandaliwa na Daniel Simons and Christopher Chabris.



Au ghafla Ferro Gaita waturudishe Cape Verde kwa kuingizia ghafla -É si propi





Halafu Mdada Denise Belfon apenyeze tena -Licks


1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

sam mbogo 6:34 pm  

Hivi unaweza kuwa mwana siasa vilevile mwana mazingaombwe? kama jibu ndiyo utaitwaje . kama siyo /hapana kwanini?. kwa hakika mazingaombwe ni mchezo/sanaa nzuri sana inayo mfanya binaadamu kwa kinywa chake akiri ukweli na uhalali wakile kitokeacho baada ya abra kadebra!(moja ya misemo muhimu katika mazingaombwe) nikweli maishani wakati mwingine huwa tuna tendeana mazingaombwe mengi tu,mfano kauri aitoayo mtu anapokuja kukopa hutanguliza imani kwanza kwamba jumatatu nitakurudishia fedha yako,kwa hakika ni mazingaombwe kwani mkopwaji atakuwa na uhakika huo wa juma tatu,ila kwa mkopaji nisiri yake atafanyaje mpaka jumatatu iwekweli,muhimu ni ile imani ya kukubali asemacho mkopaji. kaka S

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP