Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ALMASI na MCHANGA -bado LABDA ni MCHANGA ambao ni MUHIMU zaidi kwa BINADAMU hata kama kunawasiouona SPESHO!

>> Sunday, November 13, 2011

Na kitu SPESHO kuunganishwa na uchache wake  ,...
.... labda ni tatizo tu lijengwalo na WATU  kuoanisha WINGI na UKAWAIDA ,...
..... kitu kifanyacho kufanya watu  kutafsiri kama kitu kina WATEJA WENGI wafanikiwao kukipata kugeuka  mpaka zaidi ya KAWAIDA,...
... KITU KIFANYACHO kama hicho kidude ni UKE basi ni ule wa MALAYA.:-(

LAKINI:
  • Si umestukia kuna waoneao wivu  vitu MAARUFU kwa kigezo cha  kuwa hupendwa na WENGI?
  • Kwani tofauti ya KUPENDWA na WENGI na KUGAWIA wengi kitu si hutegemea na tafsiri tu  ili HASI igeuke CHANYA?
  • Na si unakumbuka kuwa pia kutokupendwa na WENGI  huweza kugeuza hicho kitu kisichopendwa kuwa SPESHO?





Katika DUNIA izidiyo kuona na kutambua MMOJA MMOJA na MOJAMOJA kama SPESHO,...
..... unaweza kushangaa vingi vilivyo kwa WINGI labda ndio kwa wengi  ndio MUHIMU hata kama hawavitambui kwa wingi wake kuwa ni SPESHO.:-(


Swali:
  • Kwani  KIPENDWACHO  au APENDWAYE na wengi  kigezo kikuu ni umuhimu?
  • Na si yasemekana ukichunguza waweza hitimisha KILA KITU na KILA MTU ni SPESHO kivyake?

Na  VINGI kwa WINGI  vinamchezo wa kurukwa  kwa  vigezo vya USPESHO,...
... ingawa kiumuhimu labda bado MCHANGA ulio MWINGI  ndio MUHIMU kuliko  ALMASI chache zibebazo sifa  ya USPESHO machoni mwa watu,...
.. kitu ambacho kikijengewa hoja vizuri,...
.. hitimisho laweza kuwa MCHANGA kiumuhimu ndio SPESHO zaidi ya ALMASI.

NI wazo tu hili KINGUNGE!




Hebu MwanaFA aanzishe upya kwa -Bado NIPONIPO



Profesa J aingizie-Hapo SAWA



Au turudi tu KENYA ili CANIBAL na SHARAMA wazime kwa-KICHWA KIBOVU


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:57 pm  

Duh! bonge la wazo:-) jumapili njema mkaka!!

Simon Kitururu 4:47 pm  

@Yasinta: Jumapili njema kwako pia mtoto mzuri!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP