Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Dawa CHUNGU saa nyingine NDIYO mgonjwa AHITAJIYO!:-(

>> Friday, November 18, 2011

NDIO,...
.... saa nyingine kwa mpenda UTAMU,...
... huweza kuchanganya kila TAMU na UZURI wa kitu ,...
...kitu kifanyacho kwa kupenda kwake UTAMU kuathiriwa kutostukia kuwa TIBABU la RIDHISHO kwake ni ndude CHUNGU.




Swali:
  • AU?

ILA yasemekana kwa bahati mbaya TAMUTAMU KUNOGA inamchezo saa nyingine kwa BAADHI YA WATU kiladha zao  kunasia,...
.... kwa MALAYA wa kulipia MTAANI zaidi ya kwa MAMA WA NYUMBANI,...
.....kwa totoz  la kilokole ambalo ni MALAYA  CHUMBANI kama liliopolewa disko vile ZAIDI  ya BONGE la totoz la  kilokole  ambalo chumbani liko kama KANISANI ambalo linaheshima za kilokole zote  kwenye mpaka ya UNYUMBA HALALI usio DHAMBI chumbani,...
....kitu ambacho labda ni swala la kuchunguza ni kwanini kwa mtu saa nyingine anasahau maji ni matamu SANA kiladha  na kuongelea juisi kama ndizo TAMU  kwa kuwa hazina maji mengi KILADHA.

Swali:

  • Si unakumbuka kuna watu hawana LADHA mdomoni?
  • Na si unakumbuka PILIPILI sio kionjo kitamu kwa kila mtu MDOMONI?

Ndio,..
.....KIDAWA,...
.... MCHUNGU  saa nyingi  HUYO ndiye DAWA,...
... na kihitajiwacho kisichopendwa ladha  mara nyingi labda NI DAWA na NDICHO MUHIMU ZAIDI   hata kama  kwa kuwa kitibiwacho  hakiitwi UGONJWA  basi na TIBABU  hata lile  lisilo na mahaba  nalo haliitwi DAWA .



Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(




Hebu kwenye GITAA LA BEZI  aingilie kati VICTOR WOOTEN nimuheshimuye kwenye chombo  ili aanzishe vita mpya kwa -U can't hold no groove if U aint got no pocket




Turudi KAMERUNI ili mpiga bass nizimiaye kazi zake Richard Bona aanzishe upya kwa - Djombwe



Halafu Richard Bona azime tu dozi tena kwa- Ekwa Mwato

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 10:35 am  

Ladha ya utamu tulipewa na Mwenyezi-Mungu enzi zile za bustani. Na hatukupewa peke yetu, bali hata nyani, paka, nyoka na kiumbe chochote kile kingine kinao uwezo huo.


Enzi hizo tulikuwa ndio sisi kabisa (wala sio Simon) "Wajinga Busara"; kwani tulitembea uchi kama wanyama wengine bila kuona haya (hata hivyo hatukuwa na maradhi yoyote yale kwani Bustani yetu ilikuwa dawa yenyewe). Na ladha ya utamu ilikuwa ndio mwongozo wetu katika ujinga wetu kutofautisha chakula halali na vyakula kama matunda yenye sumu (yalikuwa machungu).



Siku moja tulijanjaluka lakini (yaani tukageuka HOMO SAPIENS au binadamu wa kisasa). Badala ya kutustiri, ladha tamu ikageuka STAREHE.

Hadi leo ukitaka kuishi duniani siku nyingi kama alivyokupangia Mungu, OGOPA PATAMU TU (isipokuwa patamu kihalali kwa mfano unyumba katika madhumuni ya kuleta watoto duniani chini ya utakatifu wa ndoa)

Yasinta Ngonyani 1:14 pm  

Ladha!mmmhh nimewaza tu kwa sauti hili neno LADHA...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP