Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Je tukubali moja ya sifa ya UTANZANIA ni kuwa WAOGA na sio tu wa SERIKALI na VYOMBO vyake?

>> Tuesday, November 08, 2011

Moja ya kisababishacho  asilimia kubwa ya watu kuwa ma-ANONYMOUS kwenye hata michango ya maendeleo mitandaoni ni WOGA wa kuhusishwa na wawazacho.

Watu huogopa VISASI hata bila kujua kama kuna ukweli kutakuwa na kisasi kama uwazacho kinatofautiana na WATAWALA wawazavyo kitu kilichozaliwa enzi za Rais Nyerere ambapo ilijengeka kuwa ukipingana naye hukuweka nje ya mtandao usisikike . Ingawa kuna waliofika kutumia maneno kama ``Uta KOLIMBWA wewe) ikimaanisha mpaka uhai wako huweza kuwa hatarini kama ikijulikana hukubaliani na UTAWALA.

Watu  huogopa kuonekana WAJINGA kwa kusema kitu hadharani   labda kutokana na tokea watoto tunaimbiwa madhara yakuwa wajinga na labda na mpaka viboko kuchapwa kosa likiwa ni ujinga. Madhara yake hata wajuao vizuri yenye hekima na busara wako KIMYA kwa kutojiamini na WAJUAVYO ili wajije hakikishia umma kuwa WAJINGA.

Na moja ya sababu karibu MAJUKWAA yote ni wachache  huchukua muda kuchangia hoja pamoja na kwamba labda mtandao ni ghali na muda hautoshi,... sbabu kubwa bado mimi naamini ni WOGA. Woga wa kujiharibia  kitu  ingawa nasikia kujiharibia kazi aka MLO ni kitu kiongozacho.

Na yasemekana hata kwa kisingizio cha Utamaduni/Mila na desturi . Watanzania ni waoga hata kuonyesha wamempenda mtu hadharani ingawa UKIMWI na magonjwa ya zinaa bwelele yanaonyesha PENZI kivitendo linagidwa kimadhubuti

Kuna ule uoga wa hata kumsema/kumtukana mtu hadharani ingawa  vifanywavyo kwa siri vina ushahidi HADHARANI hata  kwa kupitia mapenzi yetu ya UDAKU yafanyayo vyombo vya udaku kushamiri. Kupigana majungu ambayo ni moja ya dalili za WOGA, .....nk

Tukiachana na hilo:

  • SI nasikia ni MPIRA wa miguu tu ambao WATANZANIA  wengi sio waoga kuambatanisha MAJINA yao na Wafikiriacho kuhusu YANGA na SIMBA?

  • Si nasikia kisiasa bado ni swala liogopwalo na wengi bado hata kujulikana vizuri wanawaza nini kwa kuhofia isijeharibu ulaji?

  • Na ni kiadoado tu  maswala ya JAMII mengine huamsha MIJADALA  na hasa  yakiongozwa na swala la kijamii la MALAVEDAVE ingawa staili ipendwayo katika mijadala hii pia ni ile ya mtu kutotaka kujulikana ni nani?


Naendelea kuwaza!:-(


Hebu Pepe Kalle arudie- Simplicite




Au tu Tshala Muana azime kwa- Benga Nga Na Respect


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mbele 5:27 am  

Nami nawashangaa sana hao akina anonymous.

Simon Kitururu 6:20 pm  

@Mkuu Prof. Mbele:Mimi nafikiri wanapungukiwa sana kwa kujificha nyuma ya kutojulikana kwa kuwa nafikiri moja ya sifa ya UTU ni kutambulika.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP