Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KOZI YA MAKOCHA WA NGUMI MKOA WA PWANI YAOTA MBAWA

>> Friday, November 18, 2011




Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuhuzuria kozi ya makocha iliyotarajia kuanza jumamosi ya kesho ata hivyo kozi hiyo iliota mbawa baada ya mkufuzi alieteuliwa na chama cha ngumi cha dunia (AIBA) kupata dharura kozi hiyo iliyoandaliwa na kamati ya Olimpic (TOC) iliota mbawa na kufanya makocha hao kutojua hatma yao baada ya kufika Pwani bila kupewa stahiki zao walizoahidiwa katika barua ikiwemo usafiri wa kwenda na kurudi pamoja na chakula ambavyo hawajapatiwa na kujitafutia usafiri kwa njia yao wenyewe kurudi mikoani kwao.

Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini (BFT), Michael Changalawe (kulia) akizungumza na makocha wa ngumi nchini wakati walipowasili, Kibaha Mkoa wa Pwani Juzi kwa ajili ya kozi ya mchezo huo na kuambiwa kozi hiyo iliyoandaliwa na kamati ya Olimpic (TOC)  imehairishwa kutokana na mkufuzi wake aliyeteulia kupata dharura . Hata hivyo, makocha hao kutoka mikoa mbalimbali ya nchi walinyimwa stahiki zao hususani maladhi na posho za nauli za kuwarudisha mikoani walikotoka na kupatiwa kwa makocha wachache tu kinyume na barua walizopewa makocha ya kuwa watalipiwa gharama zote za kwenda na kuwarudisha mikoani kwao.


Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania


Nimetumiwa taarifa na:
SUPER D

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP