Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUSOGEZWA MBELE KWA TAREHE YA KUFANYIKA KWA KOZI YA WALIMU WA MCHEZO WA NGUMI ZA RIDHA SASA YATAFANYIKA TAREHE 17/11/2011 KIBAHA PWANI

>> Friday, November 11, 2011

BOXING FEDERATION OF TANZANIA (BFT)
SLP 15558
DAR ES SALAAM
6/11/2011.
Email;bft.tanzania2009@gmail.com


Salaam,



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI;

YAH; KUSOGEZWA MBELE KWA TAREHE YA KUFANYIKA KWA KOZI YA WALIMU WA MCHEZO WA NGUMI ZA RIDHA SASA YATAFANYIKA TAREHE 17/11/2011 KIBAHA PWANI


Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) wamelazimika kusogeza tarehe ya kufanyika kozi ya kimataifa ya walimu 30 wa kufundisha mchezo wa ngumi.Sasa itafanyika kuanzia tarehe
17-25/11/2011 Kibaha Pwani.


Awali kozi hiyo ilikuwa ifanyike kuanzia kuanzia tarehe 12-18/11/2011 Kibaha Pwani.


Sababu ya kusogezwa kwa kozi hiyo,imetokana na mkufunzi mkuu wa kozi hiyo,ambaye ameteuliwa na Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) Ndg Azzedin Aggoune kutoka Algeria,kuomba kozi hiyo isogezwe mbele kutokana na yeye kupata dharula nchini kwao na kushindwa kufika hapa nchini kama ilivyokuwa imepangwa.


Awali mkufunzi huyo ilikuwa awasili hapa nchini tarehe 11/11/2011,kutokana na dharula iliyompata sasa atawasili hapa nchini tarehe 16/11/2011.


Aidha kwa sasa makocha hao watalazimika kuhudhuria mashindano ya Kova Cup yatakayoanza kufanyika tarehe 14/11/2011 PR Stadium Hotel.zamani Imasco Centre.

Makore Mashaga
KATIBU MKUU BFT.
Mob; 0713588818.
Email;mashagam@yahoo.com



Nimetumiwa taaarifa na:

--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP