Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

RASHIDI MATUMLA NA MANENO OSWARD KUZIPIGA Desemba 25

>> Friday, November 11, 2011

Bondia Maneno Osward (kushoto) akipambana na Mada Maugo wakati wa mpambano wao


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni  kuzichapa Desemba 25  mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.

Pambano hilo linatarajia kuwa  la raundi 10 uzito wa kati  litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .

Akizungumza Dar es Salaam jana  Ofisa habari wa Kampuni Adios Promotion ambao ndio waandaaji wa pambano hilo, Mao Lofombo alisema  pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki wakati walishawai kupigana mara mbili nyuma ambapo Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kashinda mara moja mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.

Alisema tayari mabondia hao wamekubali kucheza pambano hilo ambalo litakuwa la marudiano na kwamba  wameshaanza maandalizi  ambapo kila mmoja amejigamba kumstaafisha mwenzie ngumi.

Mao alisema, licha ya pambano hilo linalotarajia kuvuta hisia za mashabiki wa ngumi, pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Rashidi Ally atachapana makonde na Hassan Sweet, Kalulu Bakari na  Athuman Kalekwa na  Shabani Kazinga na Kashinde
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
Mob;+255787 406930
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP