Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sherehe za siku ya Kuzaliwa Mwanzilishi wa Dini Ya Sikh Guru Nanak

>> Tuesday, November 08, 2011

Salam,
Maelfu ya wafuasi wa dini ya Sikh walijitokeza siku ya Jumapili tarehe 6 Novemba 2011 katika mjini wa Southall, Middlesex UK ili kusherekea siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa dini yao Guru Nanak aliezaliwa mwaka 1469 nchini Pakistani.
Wakati akiwa na umri wa miaka 30 alipotea kwa hali ya miujiza kwa mda wa siku tatu. Alipo rejea alianza kuhubiri, kufundisha na kuandika dini ya Sikh wakati maisha yake yote. Pia Guru Nanak alisafiri dunia nzima kuitangaza na kujadili dini hii kwa waumini wengine kama waislamu pamoja na Hindus
Kwa Miaka zaidi 550 wafuasi wa dini hii wamekua na desturi hii ya kusherekea siku moja kabla ya kuzaliwa kwake Guru Nanak kwa kuandaa maandamano haya makubwa ya Sherehe hii ambayo hufanyika India pamoja na baadhi ya sehemu za nchi ya Uingereza. Kwa kawaida sherehe hizi huongozwa na wafuasi wakuu watano wanaojulikana kama ''Panj Piare'' wakiambatana waimbaji, wanamuziki na timu ya wacheza upanga (Martial Arts) kuelekea hekaluni kwao ''Gurdwara'' Sri Guru Singh Sabha,  hapa Southall hekalu lao ndio kubwa kuliko yote katika bara la ulaya
Sherehe hizi huanza mapema asubuhi kwa kuimba, kuomba kwa pamoja. Baadae chakula cha kitamaduni kinachojulikana kama ''Langar'' hutolewa bure kwa kila mtu.
Maandamano ya Southall yanaitwa Nagar Kirtan,
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE


chakula kilikuwa bure kwa kila mtu.

halaiki ya kubwa ya waumini wa dini ya Sikh wakisherekea .

Hata watoto nao walikuja kusaidia kutayarisha chakula.

Southall Palikuwa hapatoshi.

wadau wakiwa kazini kutayarisha chakula.

wakati wa kupata mapocho pocho.

Frank akiwa katikati ya mitaa ya Southall kushuhudia sherehe hii .

Maandamano yakiendelea.

Waumini wa dini ya Sikh wakiazimisha siku hii .

Frank akipata chai ya tangawizi na iliki kutoka India.

Muasisi wa Dini ya Sikh Guru Nanak.



Nimetumiwa na :
Frank Eyembe

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP