Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tatizo la KUFIKIRIA kabla ya KUFANYA kitu!

>> Friday, November 11, 2011

Ukifikiria hata DHAMBI ,...
....halafu  ukafanya DHAMBI,...
.... labda  LADHA ya dhambi  huongezeka CHACHU!:-(

Swali:
  • Huwa unafikiria kabla ya KUFANYA kitu?
  • Na hufikiri  UKIFANYA bila KUFIKIRIA na UKIFIKIRIA na KUFANYA  kitu kilekile UGALI labda   chaweza kuwa na LADHA mbili tofauti?

Jifunze KUFIKIRIA kwanza ,....
..... na UKISHA kuwa MASTA wa KUFIKIRIA  kabla ya KUFANYA,...
...FIKIRIA halafu FANYA sasa ,...
.... kuna wadaio ndio  WAFANYAO kwa BUSARA wafanyavyo.

Swali:
  • Lakini kwa KUFIKIRIA si yasemekana ndio maana mengi  ya busara kama yangefanyika bila KUFIKIRIA ndio maana WENYE BUSARA hawayafanyi  na kusababisha tatizo liko palepale  kwa kuwa hakuna AFANYAYE TATUZI kwa kuwa wenye TATUZI kitakiwacho kufanyika KIKIFIKIRIWA kwanza HAKIFANYIKIKI?

Ndio,...
.... labda moja ya tatizo la KUFIKIRIA kabla ya KUFANYA kitu,...
..... sio tu kuwa MUDA wa KUFANYA   hautatosha  kwa kuwa muda utatumika pia na KUFIKIRIA kabla ya KUFANYA.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Ijumaa na WIKIENDI njema MKUU!



.....




Turudi kidogo Rwanda ili Somi aanzishe tena kwa - Ingele



Au tu hapahapa Rwanda KIGALI BOYS wazime kwa -Arasharamye

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

EDNA 7:06 pm  

Nimepita kusalimia na kukutakia mwisho wa wiki ulio mwema.

Simon Kitururu 7:49 pm  

@Edna: Asante Mtu wangu na wewe Wikiendi njema!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP