Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Je, una kijana ambaye yuko jobless? NARCO tuna ajira yake

>> Saturday, February 25, 2012

NAFASI ZA KAZI ZA WAKALA MAUZO “SALES AGENTS”


“Kongwa Beef” ni Nyama yenye Ubora wa Kimataifa inayozalishwa na
NARCO, Kampuni ya Ranchi za Taifa Limited ambayo hivi sasa inafanya
maboresho ya namna ya kuwafikia wateja wake wa nyama ya “Kongwa Beef”.
Ili kuhakikisha tunawapatia wateja wetu huduma zinazozidi matarajio
yao, tumeamua kutoa nafasi 200 za Wakala Mauzo “Sales Agents” kwa
vijana wa kike na wa kiume wa miaka 18-30. Hii ni fursa muhimu sana
kwa vijana wote wenye uzoefu au wanaopenda kujenga uzoefu na kufanya
kazi katika upande wa Masoko na Ujasiriamali.

Kama unashauku ya kupata nafasi ya kutafuta oda za “Kongwa Beef”
kutoka kwa wateja, basi hii ni nafasi yako.


MAJUKUMU YA WAKALA MAUZO WA “KONGWA BEEF”

 Kutangaza Ubora wa Kongwa Beef na kutafuta oda kutoka kwa wateja
kwenye maofisi, mahoteli, na taasisi mbalimbali.
 Kugawa vipeperushi na kushawishi wateja kununua “Kongwa Beef”.
 Kukusanya na kutunza kumbukumbu za wateja na mauzo
 Kuelimisha wateja wajue Ubora wa Kongwa Beef


MALIPO NA FAIDA UTAKAZOPATA


 Utalipwa kwa kila kilo moja ya nyama utayoleta oda na kuhakikisha
imemfikia mteja kupitia wasambazaji wetu.
 Kadiri utakavyoleta oda nyingi zaidi na kuhudumia wateja vizuri
zaidi ndivyo utakavyopata kipato ki-kubwa zaidi.
 Utakutana na mazingira mazuri ya kufanyia kazi na kupata changamoto
za kujiendeleza kitaaluma na kimapato.
 Utapata mafunzo ya masoko, biashara na ujasiriamali ili kukuwezesha
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
 Vyeti vya heshima na vya mafunzo vitatolewa
 Utapata fursa ya kuendeleza ujuzi na taaluma yako katika fani za
biashara,ujasiriamali na masoko.


TAALUMA NA UZOEFU UNAOHITAJIKA


Mwombaji:-
 Awe na uwezo mkubwa wa kutoa huduma inayozidi matarajio ya wateja.
 Awe na uwezo wa kujieleza vizuri kwa Kiswahili.
 Uwezo wa kuongea Kiingereza kwa ufasaha itakua ni sifa ya nyongeza
 Awe mwenye shauku ya kuuza sana.
 Uwe na uwezo wa kuandaa na kutunza kumbukumbu za wateja na taarifa
za Mauzo na Masoko.
 Awe Mbunifu na Anayependa Kujiendeleza


NAMNA YA KUTUMA MAOMBI


 Andika barua kwa mkono bila kuchapisha na uambatanishe “CV” yako
pamoja na barua kutoka kwa wadhamini watatu (3) mmoja kati yao awe
mzazi au mlezi wako. Barua ziwe na namba za simu za wadhamini
 Ambatanisha namba za simu na anuani ya barua pepe kama unayo.
 Ambatanisha barua kutoka kwa Serikali za Mitaa iliyogongwa Muhuri
na yenye picha yako.

Maombi yote yatumwe kwa:

Meneja Mkuu,
Kampuni ya Ranchi za Taifa Ltd (NARCO),
Mavuno House, Azikiwe Street,
S.L.P 9113,
Dar es Salaam.

Simu : +255 22 211 0393/211 1956
Barua Pepe: info@narco.co.tz
Tovuti: http://www.narco.co.tz/

Tuma maombi yako kwa kuleta mwenyewe ofisini au kwa Posta. Kila
tutakapopokea maombi tutayafanyia kazi mara moja.

*********Wahi Wateja Wanatusubiri Tuwahudumie**********


Regards,

Immanuel Barikiel Mnzava
Marketing Manager
National Ranching Company Ltd (NARCO)
Mavuno House, Azikiwe street
P.O. Box 9113
Dar Es Salaam
United Republic of Tanzania
Tel +255 22 211 0393
+255 22 211 1956
Fax +255 22 211 1956
Mob +255 753002035
+255 715831241
+255 787831241
Web: http://www.narco.co.tz/

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 2:02 am  

Vipi kuhusu usafiri?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP