Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati TUPO tusubiriao MELI kwenye uwanja wa NDEGE!

>> Tuesday, February 28, 2012

Ndio,..
... kuna tuyasubiriayo KUSIKO,...

.....halafu tunashangaa TUYASUBIRIAYO yasipojitokeza  huku tukijishaua kuwa tumeyahangaikia.

Swali:
  • Na si kama umsubiriaye anakuja na basi la ARUSHA hata umsubiri vipi kwenye basi la MTWARA yawezekana ni kujipotezea tu MUDA?
  • Na kama utumiacho ni unga wa MAHINDI labda basi si usitegemee upikacho kitageuka UBWABWA?

Ndio,...
.... LABDA maishani,....
.... wengi ya NDEGE  hatuyasubirii uwanja wa ndege,...
.... na ingawa tunayahangaikia ila bado mahangaiko yetu tunakosea pakuyalenga na bila kustukia tunasubiria ya NDEGE  bandarini na ya MELI kule uwanja wa NDEGE na hapo ni kama kabisaa sio kwenye kituo cha daladala MOROGORO ambako hata BANDARI hakuna!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!






Hebu Hugo Nyame arudie - Pardon Madame



Au tu Majoie Ayi azime kwa - Aicha

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 5:44 pm  

Duh! sijui hao akina dada hawana mifupo?

emuthree 12:59 pm  

Hizo kweli ni sawa na ndoto za Alinacha, anawaza kumuoa binti mfalme, baada ya kutajirika kutokana na kuuza vito kidogo vya gilas, au kutokana na kuuza genge....ni sawa na wale wanadai bahari wakati wapo bara ndani ndani kabisa....

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP