Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika UBINADAMU-labda HERI mtu agundulike MJINGA yaishe YALE ya KUJIBARAGUZA!

>> Monday, March 26, 2012

Ndio,...
... wengi huangaishwa na kuficha UJINGA ,...
..... mpaka hata hufunga MDOMO ili wasiseme kitu waziwazi WAKASIKIKA,...
..... na hilo tu laweza kuwa ni kigezo kamili cha kuwaita WATUMWA wa MAADILI yaliyotungwa na BINADAMU wenye UBINADAMU .



Swali:
  • Unafikiri wakaao KIMYA huwa WAMEFUNGA mdomo au WAMEFUNGWA MDOMO?
  • Kwani nikijulikana MJINGA ntakufa tofauti na WEREVU  WASIFIWAO wafao tu kila siku?
  • Hufikiri kama ujanja ni kuwa tu MJUAJI , mwenye BUSARA, au tu sio MJINGA ndio ujanja na kitu cha maana labda UJINGA MWINGI usingekuwa unafanywa na JAMII iwasifiao kwa werevu na BUSARA wakati tu labda JAMII yenyewe itafsiricho inakitafsiri kwa KUKOSEA?


Ndio,...
..... kuna WENGI wana hofu hata ya kufungua DOMO sio tu kwenye kuficha UJINGA ,...
..... kwa kuwa hufunga bakuli hata kuficha ukweli kuwa wana nyege,...
.... kisa eti ni angalau wakae kimya angalau usiwe na UHAKIKA kuwa ni kweli hawana hamu ya NANIHII au hawana UJINGA kisa HAWAJAWAHI KUKUTAMKIA hilo!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Jumatatu NJEMA Mheshimiwa!


Hebu Khadja Nin aingizie - Simba


Au aongezee matusi tena katika -Sina Mali, Sina Deni .



Au Khadja Nin azime kwa kutuliza zaidi tena kwa - Sambolera

 

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 8:11 am  

Bonge la wazo la jumatatu hii...Swali je kama ufunguliaye DOMO naye hataki kukusikia au hata kukujibu upwayukacho ni nini cha kufanya?

sam mbogo 12:27 pm  

sina hakika na kufumba mdomo ya weza kuwa ni ujinga!? nakubaliana nawe kiduchu kuwa baadhi ya binaadamu waweza kuziba mdomo,lakini isimananishe wewe ni mjinga kwa kuwa ujasema kitu. yawezekana mjinga akawa niyule aliye kuziba mdomo kwani hujuwa ninini waweza sema juu yake. na amini kama kuzibwa kwako mdomo nikwa hila za binaadamu mwenzio hatakuziba milele wakati ukifika uta fungua mdomo na kuyasema yaliyo kinywani kwako.pia hata ukiwa ni mtu wa kukurupuka kuongea,yawezekana si mjinga kama ijulikanavyo bali hiyo ndo hulka yako,na waweza pata mawili matatu yaliyo na tija kutoka kwa mjinga huyo anaye kurupuka. ila muhimu kama binaadamu ni kusoma mzingira kwanza,kabla ya kuongea,na kujiuliza je nimuda muafaka,pia siyo mbaya kuwa na subira.kaka s

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP