Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mimi na Profesa Bhekizizwe Joseph Siphatimandla Mxoveni Mshengu Bigboy Shabalala

>> Thursday, May 24, 2012

Kama unaladha fulani ya nanihii KIMIZIKI ,...
... utajua hii ilikuwa BOMBA sana kwangu na wajanja fulani,...
.... kukutana na HATA nikiacha KILE cha zaidi KILICHOONGEZEA kutengeza uhusiano na NGULI haswa ikiwa ni NGULI HUYU!!





Hebu nimuachie NGULI HUYU  akiwa na kundi lake ....na zaidi...


...katika ndude-Knocking on Heavens Door

 

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emuthree 9:14 am  

Upo mkuu, tupo pamoja tu kama kawa

Yasinta Ngonyani 9:56 pm  

Wengine wana bahati kuonana na wale ambao wanazipenda kazi zao na pengine hata kuwahusudu...Huwa najiuliza kama ningepebda kuonana na mtu mmoja na kula naye chakula au tu kukaa na kuongea kwa siku moja....mmmhhh

ray njau 5:24 pm  

Mtani wangu naona umeamua kuonyesha na kutangaza kuwa wewe nawe ni wewe katika wale wenye uwezo na kipaji cha kujenga mduara wa mahusiano mema kijamii.
----------------------------------


1 Mkumbuke, sasa, Muumba wako Mkuu katika siku za ujana wako, kabla siku zenye msiba hazijaja, au miaka iwe imefika wakati utasema: “Sipendezwi nayo”; 2 kabla jua na nuru na mwezi na nyota havijawa na giza, na mawingu yamerudi, kisha mvua kubwa; 3 katika siku ambayo watunzaji wa nyumba wanatetemeka, nao wanaume wenye nguvu wameinama, na wanawake wanaosaga wameacha kufanya kazi kwa sababu wamekuwa wachache, na mabibi wanaochungulia madirishani wameona giza; 4 na milango inayoelekea barabarani imefungwa, wakati sauti ya jiwe la kusaga inaposhuka, naye mtu huamshwa na sauti ya ndege, na mabinti wote wa wimbo hutoa sauti ya chini. 5 Pia, wameogopa chochote kilicho juu, na kuna vitisho njiani. Nao mti unaozaa lozi hutoa maua, naye panzi hujikokota, na pilipili hupasuka, kwa sababu mwanadamu anakwenda kwenye nyumba yake ya muda mrefu, nao waombolezaji wamezunguka barabarani; 6 kabla ile kamba ya fedha haijaondolewa, na bakuli la dhahabu kuvunjwa, na mtungi ulio kwenye bubujiko la maji kuvunjwa, na gurudumu la maji kuvunjwa. 7 Kisha mavumbi huirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho yenyewe humrudia Mungu wa kweli aliyeitoa.

8 “Ubatili mkubwa zaidi!” akasema mkutanishaji, “Kila kitu ni ubatili.”

9 Na ijapokuwa mkutanishaji alipata kuwa na hekima, pia aliendelea kuwafundisha watu ujuzi, naye alitafakari na kutafuta kwa bidii, apate kupanga methali nyingi kwa utaratibu. 10 Mkutanishaji alijitahidi kutafuta maneno yenye kupendeza na kuandika maneno sahihi ya kweli.

11 Maneno ya wenye hekima ni kama michokoo ya kuongoza ng’ombe, na kama tu misumari iliyopigiliwa ndani, ndivyo walivyo wale wanaoshughulika mno kukusanya maneno; wametolewa kutoka kwa mchungaji mmoja. 12 Kuhusu jambo lingine lolote zaidi ya haya, mwanangu, jihadhari: Hakuna mwisho wa kutungwa kwa vitabu vingi, na kushughulika navyo sana huuchosha mwili.

13 Huu ndio mwisho wa mambo, kila jambo limekwisha sikiwa: Mwogope Mungu wa kweli na kushika amri zake. Kwa maana huo ndio wajibu wote wa mwanadamu. 14 Kwa maana Mungu wa kweli ataleta kila kazi katika hukumu, kuhusiana na kila jambo lililofichwa, liwe jema au baya._Mhubiri 12:1-14

Simon Kitururu 10:31 am  

Nipo Mkuu!@M3

Inawezekana lakini!@Kadala Yasinta

Umenitisha unajua kiinjili lakinin Ila sijui nitishike?!@Mkuu Ray Njau!

Yasinta Ngonyani 2:20 pm  

Simon kweli? je naweza kuonana nawe pia? maana ni....

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP