Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Chakula cha KIZUNGU ndio chakula gani hicho?-Chakula cha KIAFRIKA ndio chakula gani HICHO?

>> Friday, June 15, 2012


Nimestukia kuna katabia ka WAAFRIKA kusifia MAJINA ya vyakula vya KIAFRIKA na kwa WAZUNGU visemekanavyo ni vya KIZUNGU,...
... bila kusahau WAARABU, Wahindi, Wachina ...nk....
....na hii ni bila kukumbuka kuwa labda CHAKULA sio MAJINA wala UTAMU wa CHAKULA,...
.... kama mahitaji ya MWILI ndio yalengwayo.



Swali:
  • Hivi tunakumbuka ni nini MWILI wa BINADAMU yeyote unahitaji -kitu ambacho chaweza kuwa ni zaidi ya kuhusianisha WATU wa ENEO fulani na VYAKULA vyao hata kama sio  KIMAJINA  hasa ukizingatia labda ni virutubisho tu fulani fulani ndivyo muhimu kwenye hivyo vyakula ndio MUHIMU kuliko lililobobea kimtazamo ambalo ni MAJINA tu na staili za MAPISHI ya kiitwacho ni  CHAKULA?
  • Si yasemekana CHURA wakukaanga  na UGALI -labda  uhitajicho mwilini mwako ni CHURA kwa kuwa ushakunywa uji wa MTAMA asubuhi na wala sio UGALI?

Ndio,...
.... labda mambo mengine ni ladha na MAZOEA tu,....
.... kwa kuwa  MTU ahitajicho zaidi ni MATEMBELE au tu MATE  kipenzi litakalomfanya asile sana asivyohitaji MWILINI!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

Hebu Koffi olomide a- Civilise

 


Aongezee tena-TCHATCHO DU SORCIER

 


Au tu YOUSSOU N' DOUR akatizie denge ya KOFFI Olomide halafu wazime kwa-FESTIVAL

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emuthree 3:12 pm  

Ambiere,unanikumbusha, kuku wa kidhungu, yai lakidhungu,...kwasababu eti ni kubwa!

Kweli tembea uone,....hivi najiuliza hata hii kuvaa kata nanihino ni `mtindo wa kidhungu,maana kuiga tembo kunanihino utananihino...

Yasinta Ngonyani 3:19 pm  

Chakula cha KUZUNGU je? akila mwafrika atakufa au atakuwa mzungu? Na je Chakula cha KAFRIKA akila mzungu naye atadhulika? Mimi jibu langu hapana! kwa hiyo hakuna chakula cha KIZUNGU wala KIAFRIKA...

sam mbogo 4:26 pm  

kama nimemwelewa vizuri Mtakatifu, anamana kwanini watu wana sema hiki nichakula cha kizungu,na siyo kwamba nicha wazungu nikiwanamaana wawezaruhusiwa kukila au laa!.nahii nikutokana na dada Yasinta alivyo uliza swali na kulijibu,samahani kama nitakuwa nimekupata vibaya Da Yasinta. mimi kwa mtazamo wangu sidhani kama kuna ubaya kusema hiki ni chakula cha kiafrika au cha kizungu ,nk. kimantiki kila kitu hufananishwa katika kuleta uelewa kutokana na mzingira yake.mfano, unapo kula wali ukiwa tanzania,nakwakuzingatia taratibu za kiupishi,kwa mazingira yaliyo kuzunguka lazima utambuzi katika ufananishi utakuwepo,hasa ukimkaribisha wali huo mtu kutoka nje ya tanzani anahususan ulaya,wali huohuo ambao ulaya upo lazima mgeni huyo atakuuliza jinsi ulivyo upika,na majibu yake ndo yatayo muongoza katika kusema hiki ni chakula cha kiafrika,yaani wali huu umepikwa kiafrika/tanzania.nafikiri ni lugha tu katika kupeana maalifa ya vyakula,tatizao letu sisi waafrika/tanzani huwa hatuandiki vitu vyetu na ndomaana ukienda mahotelini/migahawa utakuta ,maneno ,mbalimbali,chakula cha kichina,ambacho kinajulikana,tusione haya kusema vyakula vya kitanzania kama vile matembele,na ugali wa mhogo. kakas.

Anonymous 5:09 pm  

Custo,

Hiyo clip ya Koffi na Youssou nilipoiona mara ya kwanza kutoka katika series ya DVD ya Africa Dance nadhani ni series namba 7nilicheka sana tena sana.

Editor aliyetengeneza Africa Dance Number 7 ni bonge la mchizi yaani kabla ya hii clip ya Koffi na Youssou kuna clip ya Kofii na mcheza show wake mmoja kibonge cha Mama. Huyo mama anamwaga radhi mpaka unaona haya kuangalia. Hiyo clip ikiisha tu inaingia clip ya Koffi na Youssou. Wachezaji wa Koffi wote wamevaa hijab akiwemo yule mama halafu mpiga picha kila saa anamrudisha rudisha! Nyimbo inakwisha wakati Koffi anamwambia Youssou "..Salaam aleikhum.." ikifika hapo hata kama huna kicheko lazima utacheka. Ukipata nafasi njoo nyumbani tuangalie Africa Dance ninazo zote kuanzia One mpaka Nine pia nimepata Naija DVDs na zingine mchanganyiko.

KUHUSU VYAKULA VYA KIAFRIKA NA KIZUNGU

Kwa maoni yangu vipo vyakula vya Kiafrika na vya Kizungu hata vya Kiasia na vya Kilatino. Vipo vya Kitanzania na vya Kihaya na vya Kichaga na vya Kimakua na vya Kikenya na vya Kikikuyu na Kikamba nk.

Sam,

Kati ya Mtanzania na Mkongo nani anaweza kusema matembele ni chakula cha kikwao zaidi? Hebu jaribu kuwachokonoa jamaa wa Kikongo unaowafahamu kuhusu hili usikie maoni yao.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP