Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

>> Saturday, June 16, 2012

Mrusi wa Matumla amemkimbia baada ya kuona rekodi yake nikali. Wawili hao walikuwa wacheze katika mpambano uliopewa jina la “The Rumbleon the Mountain” na ulikuwa ushuhudiwe na mcheza sinema maarufu kutokanchini  Marekani Deidre Lorenz ambayeatakuwa anashiriki mbio za Mount Kilimanjaro marathon mjini Moshi tarehe 24Juni mwaka huu.

Deidre Lorenz anajulikana sana kwa sinema nyingi mojawapozikiwa The Santorini Blue, PerfectStrangers, The Big Fight na nyingine nyingi. Hata hivyo Deidre Lorenzataingia mjini Moshi akitokea nyumbani kwake New York , Marekani terehe 21 Junitayari kikimbia mbio hizo za Mt. Kilimanjaro Marathon.

Bondia huyo wa Urusi Vitaly Shemetov ambaye anajulikana kama“Siberian Tiger” aliingia mitini kiaina baada ya kupelekewa tiketi za ndege yashirika la Kirusi la Aeroflot yeye na kocha wake. Hii ni mara ya kwanza kwampambano wa kimataifa ulioandaliwa kwa pesa nyingi kutofanyika baada ya bondiammojawapo kuingia mitini kwa woga.

Bondia Rashid Matumla anayejulikana kama Snake Boy anarekodi ambayo mpaka sasa hakuna bondia yeyote wa Kitanzania aliyeweza kuifikia.

Matumla ameshawahi kuwa bingwa wa Taifa, Afrika Mashariki naKati, Bara la Afrika, Mabara na Dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi Duniani(WBU). Akiwa chini ja DJB Promotions bondia Rashid Matumla ambaye kwa sasandiye Kamishna wa TPBC kanda maalum ya Dar-Es-Salaam alionyesha ubingwa wa haliya juu.

Hata hivyo Rashid Matumla amepangiwa kupigana na bondia mwingine siku za usoni  ili kupooza machungu ya kukimbiwa na Mrusihuyo!

Imetolewa na:

Onesmo A.M.Ngowi
President IBF/USBA for Africa
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)
Director, Commonwealth (English Empire) Boxing Council (CBC)
Director, BRAND-Africa
Coordinator, Moshi Sister Cities Committee
Coordinator, International Education & Resources Network (iEARN) to Tanzania

Technology House, 35-38 Ghalla Road
P.O BOX 1106, Moshi - Tanzania
Tel:  + 255-2727-53434 (Office)
Tel:  + 255-2727-55118 (Residence)
Cell: + 255-754-360828
Fax: + 255-2727-54743
E-mail:  ngowio@yahoo.com
             ibfafrica@yahoo.com
             onesmongowi@hotmail.com
Webs:   www.ibf-usba-boxing.com
             www.commboxing.com
             www.iearn.org

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP