Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sikiliza kwa makini Mahojiano na Mhe. Dr Faustine Ndugulile

>> Monday, July 30, 2012


Dr Faustine akiteta na Nguli Mubelwa BANDIO





Sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano na Mbunge wa Kigamboni (CCM) Dr Faustine Ndugulile ambaye ameeleza mengi kuhusu kongamano kuu la UKIMWI alilohudhuria hapa Washington DC, hali ya mapambano ya UKIMWI nchini Tanzania na pia harakati zake BUNGENI. Kagusia mgogoro wa MJI MPYA wa KIGAMBONI na mengineyo. 

Karibuni


 













Sikiliza kwa makini Mahojiano na Dr Faustine Ndugulile Part 2

Hii ni sehemu ya pili na ya mwisho ya mahojiano na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni (CCM) Dr. Faustine Ndugulile. Katika sehemu hii, amezungumzia suala la mgomo wa madaktari na athari zake kwa nchi. Je! Yeye (ambaye pia ni Daktari) anaamini kuwafutia leseni ni uamuzi sahihi?. Tumesherehekea SIKU YA MASHUJAA NCHINI. Ni kweli kuwa Tanzania TUNA MASHUJAA? TUNAWAENZI VEMA MASHUJAA (kama wapo) na NI VIPI TUNATENGENEZA MASHUJAA WAJAO? Anazungumzia vipi vipaumbele vya matumizi ya serikali kulingana na mahitaji ya mwananchi? Ni vipi/ ama kwa kiasi gani kuna ushirikiano wa wabunge (hasa vijana) toka vyama mbalimbali ili kuipeleka Tanzania mbele Imeelezwa kuwa serikali inachangia 3% ya gharama za mapambano dhidi ya UKIMWI licha ya kuutangaza kama JANGA LA TAIFA. Ni kweli tuna dhamira ya kupambana na ugonjwa huu? Na upi mwito wake kwa wa Tanzania wote?

 KARIBU


   





 Nimetumiwa na JUMA ISSA mahojiano yaliyofanywa na Nguli MUBELWA BANDIO wa CHANGAMOTO YETU aka "The Way You See The Problem Is The Problem" 

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP