Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tunamuangalia BINADAMU aliyeendelea akiendelea BADO kuchamba kwa MIKONO yake hata kama ni kwa TISHU!

>> Wednesday, July 04, 2012

Ndio,....
.... labda kiitwacho ni MAENDELEO na BINADAMU,...
... chaweza kuwa ni kurudi nyuma KIUELEWA,...
... na hata WANASAYANSI watafutao viumbe vingine  katika SAYARI nyingine ,...
... watafutacho hakipo kwa kuwa labda hakipatikani kwa mitazamo ya BINADAMU ya sasa iitwayo MAENDELEO.

Swali:
  • Kwani hujawahi kufikiri labda MAJINI , pepo wachafu au hata MALIKA na vitu vyote visivyoonekana kwa macho ya BINADAMU labda nndio viumbe vya SAYARI nyingine?

Ndio,...
..... labda kwa kutafuta MAENDELEO kwa mtazamo wakimaendeleo wa BINADAMU wa sasa,...
... na wala siongelei wa staili za kuchamba tu,...
... kitokeacho ni KURUDI nyuma kwa BINADAMU kimaendeleo.

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA uliyeendelea!


Hebu Fela Kuti aongelee- Colonial mentality


Au tu azime tena kwa -Shuffering & Shimiling

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

ray njau 2:42 pm  

@Simon;
Mhubiri 1:1-11
1 Maneno ya mkutanishaji, mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu. 2 “Ubatili mkubwa zaidi!” mkutanishaji amesema, “ubatili mkubwa zaidi! Kila kitu ni ubatili!” 3 Mwanadamu anapata faida gani katika kazi yake yote iliyo ngumu anayoifanya kwa bidii chini ya jua? 4 Kizazi kinaenda, kizazi kinakuja; lakini dunia inasimama mpaka wakati usio na kipimo. 5 Pia jua limechomoza, na kushuka, nalo linajitahidi kwa nguvu kwenda mahali pake ambapo litachomoza tena.

6 Upepo unaenda kusini, nao unazunguka kuelekea kaskazini. Unaendelea kuzungukazunguka sikuzote, nao unairudia mizunguko yake.

7 Mito yote ya wakati wa majira ya baridi kali inaenda baharini, hata hivyo bahari haijai. Mahali inapoenda mito hiyo ya majira ya baridi kali, hapo ndipo inarudi ili iende tena. 8 Mambo yote yanachosha; hakuna mtu anayeweza kuzungumza juu yake. Jicho halitosheki kuona, wala sikio halijai kwa sababu ya kusikia. 9 Lile ambalo limetokea, ndilo litakalotokea; na lile ambalo limefanywa, ndilo litakalofanywa; na kwa hiyo, hakuna jambo jipya chini ya jua. 10 Je, kuna lolote ambalo mtu anaweza kusema juu yake: “Ona hili; ni jipya”? Tayari limekuwako tangu wakati usio na kipimo. Jambo ambalo limetokea lilikuwako kabla ya wakati wetu. 11 Watu wa nyakati zilizopita hawakumbukwi, wala wale watakaokuja baadaye hawatakumbukwa. Nao pia hawatakumbukwa kati ya wale watakaokuja baadaye.

Simon Kitururu 6:03 pm  

Asante kwa hii !@Mchungaji Ray Njau

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP