Ukisoma kichwa cha habari hapo juu utajua tu kwamba ni vigumu sana kuweza kuingia kiundani mambo haya kwa kifupi. Kwasababu mambo yote yaliyogusiwa ni magumu na nirahisi kutafsiriwa kiaina nyingi. Jambo ambalo napenda kuligusia ni jinsi jamii yetu ya Watanzania inavyoguswa na mambo haya.
KAVA LA KITABBU CHA KAMASUTRA
Mapenzi, ashiki na ngono ni mambo ambayo yameandamana na binadamu tokea enzi au karne na karne zilizopita. Ukiingia kwenye vitabu kama biblia au hata Kamasutra utakuta maswala haya yameongelewa karne nyingi tu.Na ukikumbuka mila zetu nyingi utagundua ni jinsi ganni yalivyo nywea katika fikira na mioyo ya jamii.
Kutokana na sinema za Hollywood ni rahisi kudhani kuwa maswala haya yako wazi sana katika jamii ya Marekani kuliko Tanzania.Labda kuna ukweli! Lakini kama hivi leo huo ni ukweli, utashangaa ni lini hasa watu walianza kuvunja miiko ya kuongelea maswala ya ashiki na ngono Marekani. Jamii ya Marekani ilistuswa na ripoti ya Dr Afred Kinsey hapo Marekani
ya kwanza ihusuyo tabia za wanaume katika ngono mwaka 1948 na ile ya pili ihusuyo tabia za ngono kwa wanawake 1953.
DR ALFRED KINSEY
Ukisoma habari za huyu Dakitari au hata kuangalia sinema yake utakuta kuwa mambo ya ngono kinamnakubwa yalikuwa hayaongelewi katika jamii ya Wamarekani. Sababu zilikuwa nyingi ,zikiwemo za kidini na za kijamii kwa ujumla. Ukimsikiliza Dr Kinsey atakwambia katika kipindi hicho alichofanya utafiti, ingawa mambo mengi yalikuwa ni mwiko hivyo hayaongelewi,bado, asilimia 62 ya wanawake walikiri kupiga punyeto na kufarijika ndani ya dakika tatu, asilimia 92 ya wanaume walifikia faraja kwa njia ya punyeto. 50% ya wanaume waliooa walikuwa wanapata ngono nje ya ndoa, wanawake asilimia 26 waliondoani wali farijika nje ya ndoa kabla hawajafikia miaka arobaini.Kwa ujumla anasema mwanamume mmoja kati ya sita na mwanamke mmoja kati ya kumi walio kati ya miaka 26 na 50 walikuwa wanafanaya ngono nje ya ndoa.
Kikubwa katika hili ni kwamba mambo haya yalifanyika kwa siri sana.Na kila mtu alijifanya hayajui au ni ukweli alikuwa hayajui. Katika kipindi hiki kumbuka bado kulikuwa na imani katika wanaume kuwa mwanamke hana ashiki na ngono kwake ni kitendo cha kumridhisha mwanaume na cha kutungishwa mimba.Cha kujiuliza ni kwamba kama jambo kama hili lilikuwa la ajabbu mwaka 1953 je miaka hamsini imetosha kuliweka wazi Marekani? Je likowazi Tanzania?
Dini zetu pia tulizoletewa zinatuchanganya sana. Utasoma katika kitabu hicho hicho ukakuta Mfalme Solomon alikuwa na wake mia nane halafu ukaambiwa kuwa kila mtu awe na mke mmoja. Dini nyingine ika kuambia unaweza ukaoa wake mpaka wanne halafu mafundisho yakakubana uwe na mmoja. Ukakuta sehemu nyingine unaambiwa ngono ni kitu kizuri , halafu ukakuta unaambiwa ni maswala ya uchafu sehemu nyingine. Yote hayo yasingekuwa ni kitu kama yasingekuwa yana gusa jamii zetu sana. Ngono uko uchina ikabidi ifundishwe upya maana watu walizidi, na sasa katika jamii yetu ya Waafrika mdudu unaangamiza.
Je ni kweli tunaongelea maswala haya? Je tunachunguza tabia za kikwetu zihusiano na maswala ya mapenzi ,ashiki, ngono na dini?
Matumizi ya mtandao yanakua Afrika. Mpaka nimesoma baadhi ya ripoti kuhusu matumizi ya mtandao kutafuta ngono Afrika. Mimi siamini kuwa bado tunaweza tukawa na ripoti za kuaminika kuhusu hili swala Afrika, hasa kwa kupitia utafiti unaozingatia matumizi ya mtandao.Kwa maana ni watu wengi Afrika hawajaweza kutumia mtandao au kuwa na kompyuta. Lakini kama kuna ukweli ndani ya mtandao, basi Watanzania nasi tumo katika watu waliobobea katika kutafuta ngono mtandaoni. Kwa ujumla bado ni nchi za kiislamu zinazoongoza katika kutafuta ngono mtandaoni.Watanzania inasemekana tunaongoza zaidi katika kutafuta ngono ya watu wa jinsia moja.Inasemekakana Wakenya wakifuatiwa na Watanzania wana google zaidi neno Gay Sex. Soma moja ya ripoti kama hizi hapa ambazo zinagusia mambo haya. Siwezi kusema kuna ukweli katika mambo haya , lakini ni jambo lisemwalo.
Katika kipindi hiki ambacho bado mdudu anaendelea kuua watu katika jamii na elimu ya ngono inafundishwa.Je tunaifundisha sawasawa? Je tabia kuhusu maswala ya mapenzi,ashki,ngono, dini, jinsia yako wazi? Mtandao ni muhimu lakini je wasoma habari mtandaoni wanashirikije kupeleka habari za kuhusu mambo haya katika jamii kwa ujumla?Mimi nadhani bado tuna usiri ambao utatuangamiza. Enzi ambazo mila za asili zilikuwa na nguvu kila kabila lilikuwa na jinsi ya kufundisha mambo haya. Hata kama kulikuwa na upungufu lakini maswala haya yalifundishwa.Siku hizi ndio twazidi kuchanganykiwa.Hata habari za katerero ni mara chache kuzisikia. Nafikiri inabidi kuliangalia swala hili kwa umakini tena.kwa maana sidhani elimu iwafaayo wa ulaya na marekani ni elimu ambayo inatufaa sisi. Naamini tuna hitaji njia ya kikwetu kutatua na kuelewa mambo ya kikwetu.
Matthew chapter 5 (NLT)
27 "You have heard that the law of Moses says, 'Do not commit adultery.' 28 But I say, anyone who even looks at a woman with lust in his eye has already committed adultery with her in his heart. 29 So if your eye - even if it is your good eye - causes you to lust, gouge it out and throw it away. It is better for you to lose one part of your body than for your whole body to be thrown into hell. 30 And if your hand - even if it is your stronger hand - causes you to sin, cut it off and throw it away. It is better for you to lose one part of your body than for your whole body to be thrown into hell.
31 "You have heard that the law of Moses says, 'A man can divorce his wife by merely giving her a letter of divorce.' 32 But I say that a man who divorces his wife, unless she has been unfaithful, causes her to commit adultery. And anyone who marries a divorced woman commits adultery."
Be fertile and multiply; fill the earth and subdue it" (Gn 1:28)
Read more...