IMANI YAKO ITAKUPONYA!UKIWA VUGUVUGU HUTA URITHI UFALME WA...
>> Friday, August 31, 2007
Kuna dini fulani zilinifundisha kitu muhimu sana kwenye maisha.
Ziliniambia kuwa karibu kila kitu kinahitaji sana na kinauhusiano sana na imani yako katika kitu hicho.
- Ukiamini umekula chakula kichafu hotelini baada ya kugundua msalani kuchafu na ni pembeni ya jiko walilopikia na waliko wafadhili wale nzi wahitajio chakula kama wewe, unaweza kuharisha wakati huna vijidudu vilivyokududua.
Nilijifunza kuwa ukiamini kuwa kuna......... na ndio jibu , basi ni mpaka uamini kikwelikweli kuwa kalekadude ni ........ ndio katakuwa jibu.
Niliambiwa...
- Imani yako ndio itakuponya.
- Nikaambiwa kuwa ni lazima uwepo ndani ya hekalu, au ,ujitoe kabisa chumbani, kwa sababu , mguu nnje-ndani = na uko nje.
Nisikufiche!
Haka kakitu kako mawazoni sasa hivi.
Halafu nakaamini kikwelikweli......
- Naamini ukitaka kale kakitu na kama unaamini kabisa nilazima ukapate kale ka....
- Naamini kale kakitu utakapata hata kwa njia uifikiriayo sasa hivi, na sio ile ya mkato aliyokutonya mshikaji kuwa........
Kumbe mshikaji ni wewe!
Nong'oneza tu njia ya mkato kama ni halali!
- Lakini , njia ndefu inafaraja zake.Inakusababishia kujua na kukasikilizia kale ka-utamu kunoga kinamna fulani.
Utakua unajua kwanini na kwa njia gani ambayo umekatolea jasho kukapata kale kakitu bila mjomba kukasaidia au yule mwingine kukupunguzia utandu kwa kudai kuwa; Simon bila mimi asinge......
Usiniulize lakini kama kale kakitu nimekapata tayari au bado!:-)
DUhh!
Najua kuna watu wana haraka sana hata katika..........!
DUH!
Sasaaa.........
Si imani yako itakuokoa?
Si imani yako itakuponza?
Swali :
Imani yako inaku.................?
Pata....
Read more...