Tukiachana na swala la KUKU MJAMZITO.... ....... baada ya KUKU kufanya TENDO LA NDOA kama BATA,.....
.....tuongelee binadamu kiduchu basi!
Kwa BINADAMU kuna TAMADUNI, MILA na DESTURI zifanyazo tuamini KUWA NI ukweli kuwa swala la UJAUZITO ni la wakubwa,.... ..... ndio maana binadamu akiwa mtoto hudanganyika kuwa watoto wananunuliwa duka fulani au kuna ndege anawaleta hata kama anayemsimulia BINADAMU MTOTO HUYO , ana MIMBA.:-(
Na ,... .....kwa kuwa jamii inadai kuwa MASWALA YA UJAUZITO ni maswala ya faragha kuna ambao wamepata mimba kwa kutojua MASWALA YA mpigwa chini huvimba JUU.
NDIO!
Tamaduni zetu wengi zinatufanya tuepuke kuzungumzia mambo fulani:-(
Na ujuzi wa asilimia kubwa ya vijana siku hizi ,.... ......ni wakujifunza wenyewe KUPEKECHA ingawa kuna washangaao kwanini RIJALI kila siku akiingia mtandaoni akilini akiona KIBONYEZO''search ''hakawii kuandika mbele yake neno ''SEX''.
Ndio!
Asilimia kubwa ya WABONGO niwajuao wamejifunza maswala ya KITENDO CHA KUUJAZA ULIMWENGU wenyewe kwa kuwa ndugu na hausigeli hawakuviongelea kwa kuwa MILA na DESTURI ZIMEWAFUNGA mdomo hata WAZAZI.:-(
Na tatizo kubwa katika hili ni kwamba,.... ..... kama huna MUONGOZO itabidi ujishughulishe mwenyewe KUPATIA na kwa bahati mbaya kwa kujifunza bila MUONGOZO waweza kujikuta USHAZOEA KUKOSEA matumizi ya NYETI.
Kumbuka,... ... apataye MIMBA wakati anapata MIMBA kunauwezekano MKUBWA alikuwa anafikiri anapata URODA tu a.k.a MIKASI na sio alikuwa ANAMIMBISHWA.:-(
Kumbuka,... ..... mara nyingi BEBERU LIKIPANDA huwa halifikirii matokeo yake ni kumpa mimba KIMWANA mbuzi.
Na kumbuka ,.... .... mwenye mimba anapendeza kwa kuwa unajua ana mimba LASIVYO ni kweli mwenye mimba huwa ana tumbo KUBWA a.k.a BOMBA LA TUMBO na HUWA anabadilika MWENDO.
Kwa hiyo,... ..... jihadhari kumuuliza MWENYE TUMBO KUBWA asiye na MIMBA maswala ya UJAUZITO kama hutaki kufyonzwa KABLA hujashushiwa bomba la TUSI lenye uzito wa KILO KADHAA lifuatwalo na bomba la KOFI .Na kama wewe mfupi JIHADHARI kwa kuwa labda pia utapewa bomba la konzi lenye KILO TATU na NUSU hivi kwa kukosea wa KUMDADISI.
Na ni kweli,.... ..... ukikutana na mwanaume akukumbushaye MWANAMKE mjamzito, basi inasemekana huyo ANAKITAMBI kitu ambacho SI AFYA kama tu toto dogo lenye tumbo kama mimba linaweza kuwa lina KWASHAKOO , UTAPIAMLO ,nk.....
........ kitu ambacho SI AFYA!:-(
Na ni kweli,... ..... MIMBA ni KIBOKO ndio maana UMEZALIWA.:-(
Swali:
AU?
DUH!
NALIKATIZA wazo hili kabla ya KUONGELEA kuhusu MIMBA ya kuku bila KUOMBA ruhusa ya KUKU!
Swali:
Hivi kweli umesoma mpaka sentensi hii hapa katika SWALA HILI lenye uwezo wa kuwa ni la KIJINGA ?
Unafikiri lini katika ukuaji wako ulistukia MIMBA sio KITAMBI na KITAMBI sio MIMBA?
Unafikiri kungekuwa na uwezekano binadamu wasingehusudu KUTAGA kama kunguru ili kukwepa kuvaa MATENITE DRESI ingawa kasheshe lingekuwa ni zamu za hausigeli kuyatamia mayayi wakati bingwa YUKO kwenye KICHENI PATI?
Kumbuka ni wazo tu NA NIMELIKATIZA nikiwa nakutakia KILA la KHERI katika LAKO LIBENEKE!
Ngojea Kenny Roggers abadili hali ya hewa kwa kitu- You are so Beautiful
Au tu BONGO MAFFIN watukumbushe- MAKEBA Read more...
Na,.... ..... hapa siongelei swala la KUTHUBUTU kwako KUNYA,(samahani kwa lugha ya faragha), namaanisha kwenda HAJA KUBWA, kwa kuwa hata KUKOJOA(samahani tena kwa lugha ya matusi), namaanisha hata HAJA NDOGO unafanikisha ukiwa PEKE yako CHOBISI shwari.:-(
Ukitaka kujihakikishia una nguvu za KUTHUBUTU,... .... jaribu KUTHUBUTU angalau KUJAMBA mbele za WAHESHIMIWA au WAGENI ambao HUJAWAZOEA kwa MAKUSUDI!:-(
Swali:
AU?
Kuna uwezekano LABDA kama UNGETHUBUTU sasa hivi usingekuwa unanisoma na ungesha JIUA zaaamaniiiii HATA kwa kula sana hata MAGIMBI au tu kwa kudai kama nidaivyo MAISHA MAGUMU!:-(
DUH!
Swali:
Au?
Thubutu lakini kama unataka kuwa WEWE na sio kuwa WATU wakufikiriavyo wewe kama tu MUUZA SURA kwakuwa una BOMBA la PUA ingawa MWANIWANE una MIAKILI MINONO na TABIA KIJEBA!:-(
Swali:
Unafikiri kama wajidanganyao KUWA NI wazuri wauzavyo sura , UNAFIKIRI wewe huuzi tabia INGAWA unamaaeneo mazuri KIFICHONI yenye TABIA MBAYA YAKITEKENYWA hata kama BADO yana nywelenywele NJOLINJO?
OK Bingwa nikiacha KUKUZINGUA na UJINGA; SWALI:
Unauhakika umewahi kuthubutu na bado ukabakia MASIKINI?
NAACHA wazo BINGWA!:-(
Ngojea TUKAECHINI ili TUJIFUNZE watoto WADOGO wanasemaje kuhusu KULA KONI katika-Oral Sex the New Goodnight Kiss...
Au tu tusikilize utunzi wa Michael Jackson naLionel Richie katika-WE ARE the WORLD..
KWA MARA nyingine ASANTENI WOTE! Mkiwemo hawa kwenye picha zangu za juzi ya MTONDOGOO....
Ukiwa na pesa za GARI,... ... mwenye gari hakuumizi KICHWA.
Ukiwa huna uhakika wa gari na unauhakika wa MKWECHE,.... ....mwenye gari , ingawa ni mpaka uwe unataka gari ,ANATISHA!
Ukiwa na uhakika UTAFIKA,... .... waliotangulia SI WAJANJA.
Ukiwa na wasiwasi na uwezo wako wa KUFIKA,.... ..... unaweza mpaka kuanza kufikiri UTAFIA NJIANI na waliotangulia kwako WANATISHA.
Ukiwa na mke MZURI,.... ....wenye wake hawakutishi kwa kuwa unaujua MKENGE waliouvaa.
Ukiwa na mke MBAYA,... ... wake wa wenzio wanavutia MNO kwa kukosa KASORO na jicho la ubongo WAKO litabunia MPAKA umbo lao hata la kabla hawajavaa.
Swali:
Hivi kweli kuna mke mbaya duniani?
Ukiwa na MUME MZURI au MBAYA mie sijui nini kinatokea na SAMAHANI kwa KUKOSA UTAALAMU wa HILO!
Ndio,...
.....Ukiwa na uhakika leo hata kuhusu ya kesho,.... ... walionayo leo HAWAKUTISHI.
Tatizo ni;
...Ukiwa na uhakika leo, HUO NI UHAKIKA WA LEO,....
.....na labda kesho utagundua;
Pesa zako zikutiazo kiburi leo hazitoshi kesho kununulia hata mkweche.
Uhakika uliokuwanao leo kesho haupo, na ghafla huna uhakika wa hata kufika kesho kutwa ya KESHO.
Kakitu ambako katafanya MKE wako mzuri leo, USTUKIE kumbe tokea ZILIPENDWA alikuwa mbaya.
NA LABDA,.... .... Kibinadamu, ALAYE SASA HIVI ndiye mwenye uhakika ANAKULA,..
... na siye wengine HATUJAPANIKI TU kwakuwa TUNA MATUMAINI TU kuwa baadaye TUTAKULA.
Uzuri ni kwamba ,... ...BINADAMU huendeshwa na TUMAINI,......
.... ndio sababu ukiwa na kibano LEO unadhani labda utafaidi mbinguni WAKATI labda KIBANO CHAKO unachodhani ni KIBANO LEO ni KILE chakutamani unywe GONGO NA WASHIKAJI halafu usinyimwe TENDO LA NDOA a.k.a URODA a.k.a MIKASI a.k.a MATUSI a.k.a UASHERATI hapo baadaye CHOBISI , ingawa LABDA mambo yote HAYO umeshafundishwa na DINI YAKO kuwa MBINGUNI hayapo, NA kule mambo yote ni JUISI kwa MAZABIBU halafu KUIMBA kwa SANA TU na MALAIKA , halafu kwa bahati mbaya hakuna KUCHOKA.:-(
DUH samahani kama nakukwaza kwa kuwa unadhani nakufuru!:-(
LAKINI,...
....UBINADAMU ni NISHAI KWELI kwa kuwa kama wewe ni BINADAMU na SIO JINI, labda KWAKO hakuna lenye uhakika!
NAACHA wazo na KUMBUKA ni WAZO TU na nakutakia kila la kheri katika kukuza lako TUMAINI. Damn , I am depressed now.(NA samahani kwa kuingizia ung'eng'e KIDUCHU!:-()
PEACE!
Tupitie Kenya kidogo Les Wanyika wadai - Dunia Kigeugeu
Au tubaki tu KenyaSalim Junior adai-Ni sorry Muno.. Read more...
USITISHIKE,.... ...... yote ni katika kukukumbusha kwa KUTEMBEA KWAKO KWA MARINGO kumbuka NI SIKIO linakusaidia kufanya hivyo NA SIO TAKO kama wewe kwa mwendo wako wa maringo huwa unatingisha tako!:-(
Halafu ni kweli,... .... sababu kubwa ya Mlevi kuyumba ni kwamba KALEWA.
Swali:
AU?
Kwani wewe ulifikiri hadithi hii nitaisimulia kwa urefu gani?
Hivi sasa hivi sikio lako ukilichokonoa halina NTA ingawa sikioni mwako hakuna nyuki?
NAACHA wazo MKUU na NAKUTAKIA siku njema KINGUNGE katika libeneke!
LAKINI kama unamuda ngojea Waziri wa Utamaduni wa Brazili a.k.a Gilberto Gill atuburudishe tena kwa- Aquele Abraco
AU Ngojea tu tena Gilberto Gill adai -Waiting in Vain.. Read more...
ANAYEJIHESHIMU ,... ......huaminika kuwa HUWA ndiye asiyoyaongelea MAMBO kama hivyo HADHARANI,....
.....ndio maana kuna wasahauo WAITWAO WAHESHIMIWA wengi ndio wateteao ujinga HADHARANI.
MHESHIMIWA ,.... ..... inasemekana HAVAI HIVYO hadharani,....
.... ndio maana ni bingwa zaidi ya WANAMAZINGAOMBWE kwa UTETEZI wa NGUO kwa MANENO hata wakati akiwa anawazia YALIYOUCHI fikirani HADHARANI.
Na ya MHESHIMIWA yako FARAGHANI,.... .... ndio maana WASIOFIKIRI HUKOSEA wakumuheshimu HADHARANNI.
UHESHIMIWA ni kama MADAWA ya KULEVYA,... .... aliyenaswa na KUHESHIMIWA anajikuta anaung'ang'ania hata kwa kuomba kura za vyeo asivyovistahili HADHARANI.
Na kama unataka kulogwa na MHESHIMIWA,... ....baadaye kidogo baada ya KUWINI chuki za MHESHIMIWA,.....
... toa siri zake za CHUMBANI hadharani.
NAACHA na ni wazo tu MKULU! Kumbuka kama umenisoma mpaka sentensi hii wewe si MTIIFU kwa kuwa nilikuomba kwenye KICHWA cha habari usisome STORI HII!:-)
Swali:
AU?
Ngojea basi tuliwaziwe na The VERVE katika - Bittersweet Symphony
Au ngojea tu Eminem, Jay-Z, Lil Wayne waharibu wimbo huo huo katika -Bittersweet Symphony Remix Read more...
Siku hizi inasemekana,... .... hata kama Binti Khalufani hawezekani kwa kunema, WANAUME hawawezi kustukia a.k.a KUJUA.
Lakini labda hata hapo zamani za miaka fulani iliyopita,.. ... ujuzi wa Binti Khalufani au tu Binti Josef ulikuwa unapimwa kwa utiifu hata kama ni utiifu kwa mambo ya ajabu katika jamii ili mradi jamii inayaona ni DILI kama ya kukubali kutahiriwa KIDUDE na huko huko atahiriwako KUFUNZWA kuamini Mwanaume tu ndio USAHIHI WAKE ni SAHIHI.
Swali:
AU?
Ngojea nianze stori hii upya.......
Hadithi !Hadithi!
Nasikia enzi za ZILIPENDWA , .... ....VIMWANA walikuwa wanafunzwa kutii waume zao !:-)
Na nasikia pia ,... ....ilikuwa kama Mke wako akikushinda kwa HOJA kama tu aendeleavyo kukushinda hoja sasa hivi,.....
..... ilikuwa RUKSA kwa KIDUME kumchapa makofi halafu kabla hajamalizia kulia ilikuwa DILI kumshughulikia kunako apate MIMBA ili achunge adabu zake! DUH !Kudadeki Walakhi!:-(
Kwa kifupi ,... .....WANAWAKE na WANAUME enzi hizo ukitazama na kufikiria kwa jicho la kileo unaweza kugundua walikuwa hawajuani ila mmoja alikuwa anajitoa mhanga ili mwingine AFAIDI.
Swali kiduchu:
Hivi ni wewe ujitoaye muhanga mwenzio afaidi LEO HII au ni yeye ajinyimaye UMIMI ili wewe ufaidi halafu mahusiano YENU bado hayanogi?
Kwa bahati mbaya,... ... Bado naamini leo hii bado siye WANAUME tulio wengi hatulelewi kumuelewa au hata kumjua MWANAMKE. Halafu juu ya hilo, SI RUKSA KUMBWENGA Mwanamke wako hata pale katika klabu ya GONGO au Ulanzi kama tu pale kwa Bibi Kisebengo wauzapo DENGELUA siku hizi.
Kwa bahati mbaya,... ....naamini leo hii hata WANAWAKE walio wengi hawawaelewi WANAUME wanataka nini na kama unabisha WASIKILIZE waongeayo.:-(
Ukitaka kustukia kuwa hali si nzuri,....
Cheki jinsi gani Pochi lako likuzungumziavyo kuliko Roho yako katika maadili ya leo.
Sikiliza watu hata uhisio ni wenye busara wakizungumzia siri ya mahusiano kati ya Mwanamke na Mwanaume hasa wakati unajua siri hizohizo wangapi zimewaharibia ndoa au kupoza penzi hata kama bado kidude wanapata.:-(
Swali:
Umestukia mpaka wafuata dini wamsukumiavyo Mwenyezi Mungu matatizo yao ya ndoa ambayo mengi yao yangetibika kwa wao kuongea tu a.k.a kuwasiliana/kusikilizana?
Unataka kusema hujawahi kusikia, hasa kama wewe ni MKRISTO, wakwepao kuongea moja kwa moja MPENZI na mpenzi kwa madai YA kupitia kwa Yesu na Biblia kitu ambacho huwatisha kuachana na kuendelea kuishi pamoja bila furaha kwa jina la Yesu?
Unaweza kunibishia lakini na LABDA miye siwezi kukubishia mwenzio KWA KUWA mwenzio hapa nawaza tu MKUU!:-(
Ndio ,.. ....labda kati ya Mwanamme na MWANAMKE ukunaji wa kipele unaumuhimu wake ila labda ni muhimu kwanza kustukia uwepo wa KIPELE maeneo na kama ni busara kukibinya nasio kukikuna.
Na unaweza kubisha!
Leo hii tunavyoongea hapa bado WANAWAKE na mambo yao pamoja na KIDUDE chao yanaenda kivyao KAMA tu WANAUME na mambo yao ikiwa pamoja na UUME wao wanaenda kivyao.
Na asilimia kubwa ya wapenzi wenye tatizo la MAHUSIANO leo HII ukiwaweka vyumba tofauti na kuwauliza nini ni tatizo usishangae ukisikia hawana jibu linalofanana kama kwa mfano utakuta:
Mume adai tatizo hana pesa za kutosha, mwanamke akadai pesa si tatizo ila HAKUMBATIWI vya kutosha NA ndio tatizo!
Mwanamume akadai hapewi kidude vya kutosha , wakati MWANAMKE akadai KIDUME nyumbani haonekani na kidude hana muda nacho na katika KUGIDA anakila kwa uchovu ingawa daima NAMWANDALIA na manukato nanyunyizia.
Mwanamke akadai hasikilizwi wakati mwanamume akidai Mwanamke mashoga wamezidi na KIMWANA hapatikani ukitaka angalau KUMNG'ATA sikio.
Mwanamume akadai anatamani NA anafurahia KIMWANA akimfyonza, wakati MWANAMKE akadai alivyofunzwa kumfyonza mtu ni matusi na Kidume AMKOME BABU WEE nyooooooo!.:-(
Swali:
Unafikiri lakini Mwanamume gani siku hizi anauhakika Binti Khalufani kwa kunema hawezekani kabla ya kukutana na Binti Khalufani ki- MKUTANO?
Unafikiri jamii inavyobadilika ni kwanini MAFUNDISHO ya mahusiano kati ya Mwanamke na Mwanaume ambayo ndio misingi ya BOMBA LA FAMILIA hayatiliwi MAANANI yabadilike kukidhi mabadiliko ya Limwanamume na Limwanamke wa leo wajengao JAMII ya LEO?
DUH nimekumbuka miye si mtaalamu wa Mahusiano YA WATU na NAACHA TOPIKI! NIMEACHA na kumbuka hili ni wazo tu na NAKUTAKIA siku njema JEMADARI!
Ngojea niwaachie ARROW wabadili hali ya hewa kwa kitu-Hot Hot Hot
Au tu Arrow waongelee sabuni ya roho kamaitambuliwavyo na baadhi ya watu- - money money
ASANTENI tena WADAU wote ! Asanteni hawapia ambao hamkunitenga siku za karibuni ambao baadhi ni hawa kwenye picha zangu.....
Hata utakekubisha,... ..... kama wewe ni Mtanzania unajua kuwa mpaka leo CCM inabomba la msuli ukilinganisha na UPINZANI.
Na kwa bahati mbaya,... .... kwa muda wote huu chama hiki kinatawala kwa walio wengi hawajala KINGI.
Kwa bahati mbaya,... ..... hata wajanja kibao wanafikia kuamua kuwa WANACCM ili kuwa karibu na KINGI.
Swali:
Unabisha?
Kwa hiyo hata kama huipendi CCM,... .... si vibaya kukiri kuwa kuna kitu wanapatia ndio maana katika STATISTIC zanguMtakatifu Simon Kitururu ambazo sijazifanyia utafiti, ASILIMIA KUBWA YA WENYE nafuu TANZANIA ukichunguza ni WANACCM au wana uhusiano na CCM.
Swali :
Unabisha?
Kwa hiyo,.... .... utake usitake naweza kuwa sijakosea kwa kusema CCM OYEEE, ila zisidumu fikira za Mwenyekiti zenye mrengo wakutunyima KULA KINGI:-(
Swali:
Sijui Watanzania wote tujiunge na CCM kama ndio kwenye ulaji?(au unasemaje Bingwa!)
Kwani kuna sababu gani za kujiunga na CHAMA kingine kama ulaji uko CCM?
Hivi ni kweli unafikiri CCM ni CHAMA CHA MAPINDUZI?
Naacha, na kumbuka ni wazo tu KIBOSILE! Haya basi VIVA CHADEMA!Viva CUF! Ila mnaulaji kwa wananchi wote CCM iwanyimao NANIHII?
Baadaye BASI! Ngojea East African Melody wadai -UTAJIJU JIJI
KATIKA fundisho kumbe ni kweli,..... .....UNAWEZA kulipia kupewa hata GONO kama tu ununuavyo viazi VITAMU.:-(
Na,... ... mpaka konokono wanafanya ngono na kama wewe unafanya matusi/MAPENZI kwa mwingine hiyo ni NGONO tu:-(
Na ,... .....MALAYA ni mtoto wa mtu na inawezekana ni ndugu yako au ni mtoto wa mheshimiwa kama wazazi wako kama SIO MTOTO WAKO na labda uwepo wake duniani ni matokeo ya NGONO tu.:-(
Na,... ..... si lazima ujilazimishe kupata dhambi ingawa unafanya dhambi nyingine kwa kuwa unajua ni dhambi na NONO.:-(
Na,... ..... MALAYA ni kwa wengine kama kwako unaamini ni wako na UKO NAYE na PIA ni MNONO.
Swali:
AU?
DUH ! Naacha wazo MHESHIMIWA na samahani kwa kukupotezea MUDA kwa kunisoma NA labda badala ya kunisoma sasa hivi HAPA ungekuwa uko chooni UKIFANIKISHA!:-(
Swali:
AU?
Unauhakika malaya ni malaya na sio ni FIKIRA ZAKO TU kwa kuwa UNASHINDWA KUTOFAUTISHA ugawaji wake MALAYA na HURUMA au unauchanganya TU na kuwa kwake na roho NZURI ya KUGAWA nanihii?
NAACHA!
Hebu tupitie tena MALAWI tukutane na Fuggie Kasipa +Njati Njedede walete za - Ukanene
Au tupitie tu tena ZAMBIAAngela Nyirenda aburudishe kwa - Ngoma Read more...
KUMBUKA,... ...ujanja wa KANISANI sio UJANJA wa MSIKITINI ingawa zote ni IMANI:-(
Kumbuka,... ....UJANJA wa kanisani labda niwa SADAKA!:-(
Kumbuka,... ..... Ujanja wa MSIKITINI aujuavyo SIO wewe na ni SHEKHE ajuaye ndio maana akiamua UTABINUKA kwa IMANI na ukibinuka kwa kweli hiyo ni staili ya SALA na yote ni IMANI!
Kumbuka,.... ...LABDA kanisani AU msikitini kama ungekuwa MJANJA ungestukia kuna WATU wanatibu hukohuko MPAKA ya UCHI kama tu CHUMBANI kama wewe ni mjanja chumbani na unajua mpaka ujanja wa MIGOMBANI na UNAKIBURI katika KUNG'ANG'ANIA nanihii hata kama hiyo haina KISHIKILIO!:-(
Swali:
AU?
Halafu NI KWELI,.... .... labda ujanja wa TITI ni CHUCHU la sivyo hakuna KINYONYEO!:-(
Na stori hii haina uhusiano na TITI wala CHUCHU na bado hili si kielelezo cha naongea nini.:-(
Swali:
AU?
Ok ngojea niache KUONGEA ! Mtaalamu samahani kama NAKUKWAZA !:-(
Au ngojea tena BURNING SPEAR aongelee UZOEFU katika- This Experience:-(
Au turudi tena TU AFRIKA KUSINI Arthur MAFOKATE agune katika - OYI OYI... Read more...
Ni tusi kuonewa huruma,... ..... kama wewe katika SIGIDA kwa kuwa una SIGIDA ndio UNADHANI unatakiwa kuwaonea huruma wasio na SIGIDA kwa kuwa HAWASUGUI sebule ya kichwa kwa KUSALI mpaka wakaota SIGIDA!:-(
Na KUONEWA HURUMA ,... ......ni siri ya UMASIKINI kama wakuoneao huruma wanakitumbua na wamefikia kukunyima KITUMBUA na huna uhakika na uwezo wako wa KUTIMBUA.:-(
Na si siri,... .... kuna kitu nimenyimwa LEO kama MWAKA JANA kama WEWE TU ,....
.... ambacho kwa kunyimwa nakifanyia kazi na nahisi nitakibugia BAADAYE kwa juhudi.:-(
Swali:
Unafikiri juhudi ni nini na ni lini uliJUHUDIKA na kwa kujuhudika unaweza kuapia HUKUWEZA kufanikisha KULA?
SAMAHANI kama KU-mamaye ni TU-si kwa mheshimiwa kama MHESHIMIWA huwa anafikiria KU-dadaye ni NINI!:-/
Nakatiza wazo KINGUNGE na labda wazo hili ni UJINGA ingawa kumbuka ni WAZO TU na sio USENGWILI!:-(
ASANTENI WOTE na ukiwamo WEWE, lakini kama wewe ni MHESHIMIWA kama WEWE halafu umejikuta UMESOMA mpaka sentensi hii ambayo labda ni UJINGA, samahani!:-(
NAACHA! Swali KIDUCHU:
Unahisi au UNAFIKIRI ni HAKI ya MUNGU au YAKO kuonewa HURUMA na wenye HURUMA wale?
Na hivi KU-shangaziye WALAKHI kwako si tusi,.... .... KAMA utaniahidi kufikiria tena kwako TUSI ni NINI?:-(
Samahani BINGWA! Niko MAWAZONI tu mwenzio!:-( :-( :-(
Ngojea MAXWELL aongelee MAISHA katika MNONONEKO uitwao....-LIFETIME
.....AU tu MAXWELL aendeleee kutuboa kwa kibao...-REUNION..
Kwa KURUDIA kuwa na HAMU ya KITU si lazima safari hii UTAKIDHI HAMU.
Na huwezi kujilazimisha uwe na HAMU na ni kweli kuna hamu hazijirudii kama tu ile hamu ya KUCHOMWA na MIIBA , kuumwa na SIAFU au ile ya maumivu ya LIMTU ulipendalo kukuacha SOLEMBA na Limtu jingine!:-(
Binadamu ni MWEPESI kusahau na kumbuka hilo ukiisahau HAMU,... ....NA ndio maana ALIYEKUWA ANALIA JANA unaweza kukutananaye LEO anacheka ile balaa ingawa ni kweli ana meno kama NGIRI.
Na usidanganyike kwa kuwa labda umeshiba sasa hivi ukafikiri UMETIBU hamu ya KULA hapo baadaye .:-(
Kumbuka,... .... HAMU ni MALAYA na ukiwa na WALI na MAHARAGE sasa HIVI kunauwezekano unajitengenezea mazingira ya kuwa na HAMU YA UGALI kwa CHUNGA.
Swali:
AU?
NI moja ya wazo tu Kingunge na NIMEACHA!
Hebu twende tena Reunion tupate Afrofusion kutoka kwa Granmoun Lele aongelee - Soleye
Au tu Jamie FoxxnaTimbaland wabadili hali ya hewa katika -I don't need it Read more...
Kinyongo kama tu KULAANIWA,... .... Laana haimtesi ALIYELAANIWA na KIMPACHO laana MTU ni KUISHI NA LAANA.:-(
Ni kweli,... .... KUISHI NA KITU ndio KASHESHE na kukifanya kitu ni rahisi hasa kama hufikirii kuwa itabidi uendelee kuishi UKIJUA ni kweli ULIFANYA KITU naKATIKA KUFANYA kumbuka WENGINE wafanyacho ni KUUA!:-(
Kama unakinyongo na mtu ,... .... wewe unateseka na KINYONGO na wala sio huyo MTU.
Na kama unakinyongo na MTU,... ..... na unataka USITESEKE na KINYONGO, basi usiishi na KINYONGO.
Swali:
AU?
KUMBUKA hili NI wazo tu Kingunge!
Ngojea Barbara Kanam aongelee ya - Teti
Au tupitie tena Cape VerdeTalina alete - Pour Te Revoir Read more...
KATIKA dunia HII yenye WAPENDA SURA NZURI ,... .... wenye SURA MBAYA wengi hutambuliwa kwa zao JUHUDI za vitu vyenye SURA NZURI.
Swali:
Unauhakika ni nani mwenye sura nzuri?
Ni kweli unataka mpaka kujua ukweli kuwa ni UKWELI hata kuna KINYEO chenye sura mbaya kwa mtazamaji?
Kwa juhudi unaweza usistukiwe kuwa sehemu zako za siri zina SURA MBAYA kwa kuwa kwa juhudi zako wewe ni TAJIRI na katika utajiri wako baadhi ya MATUNDA YA LA KIJINGA likufanikishalo ULE KINGI , ni lile UFANYALO lisababishalo JUHUDI ZAKO zitambulike kwa HATA WASIO WAJINGA , ...
....na labda likutambulishalo NI JINSI UJUAVYO KUHONGA hasa KWA BILA , .... ......bila kujulikana unahonga kwa wakupao KIKOJOLEO,nyuma ya kikojoleo , chuchu ,NA labda hata MAANDAZI PIA kabla hujapewa KIDUDE maeneo!:-(
Na LABDA ni kweli,....
... INASEMEKANA kuwa ni KWELI kama unatafuta waishio kwa kutegemea SURA ZAO, ... ...JAMII IITAZO NZURI na unataka USITAFUTE, ....
... tembelea shule za waliofeli au tafuta sehemu rahisi zipendelewazo na WASIOFIKIRI au TU pale uhisipo kuna WAJINGA a.k.a WAVIVU wa MHANGAIKO kwa kuwa sura inauzika hata kwa HEDIMASTA.:-(
Swali:
AU?
Na kumbuka,... .... JIHAMI na MTOTO MZURI uaminiye ANAAKILI kwa kuwa kwa kumuangalia huoni kasoro ZAKE ,....
.....na hujui hata UMAHIRI wake wa kutumia NYETI na kinakufikirisha kwanini huoni kasoro ZAKE kwa kuwa labda HUONI KASORO KWA KUWA MJANJA labda HUJUI KASORO ZAKE KWA KUWA anakunya KITANDANI na wewe ni ALEJIKI na MAVI na hata SEBULENI KWAKE HUJAWAHI alikwa!:-(
NDIO! ........INASEMEKANA kirahisi JAMII iwaaminio ni wazuri bado HAO na wao husamehewa hata kama WANAKOJOA KITANDANI!:-(
Na,... ....INASEMEKANA kirahisi JAMII IWAAMINIO NI WAZURI huwapandisha hata CHEO ofisini kama tu KITANDANI , huwaSIKILIZA hata kwa yasioeleweka kama vile yao ya KUGUNA, na pia ni kweli wanaweza kusifiwa kwa USAFI WA CHOO ingawa choo chao bado KINANUKA na ungejua,...
..... labda ni kweli WANAKOSEA hata KUNYA!:-(
NDIO ,..
....ni kweli ukiamini kuna MTU MZURI ,...
....huyo anakuchezea MAZINGAOMBWE na ABRA kaDAbra YAKE labda inakufanya uweze kujikuta umeoa mpaka MTU anukaye UVUNGUNI kwa mnukio ufananao na MAITI YA SAMAKI kwa sana tu ,... ...kisa NI KWAMBATU huwa akikuchekea PUA yako HUZIBA ingawa unajua hata YEYE michezo ya BABA na MAMA yeye ni MTOTO MZURI na bado KATIKA SHUGHULI yeye ni MTOTO!:-(
Na ,... .....LABDA inahitajika kuamini KUWA kama unaamini una SURA mbaya ni muhimu kwako kucheza mazingaombwe ya JUHUDI kwa kuwa KUWASAHAULISHA WATU yako NI sura MBAYA KWA IMANI,...
..... huhitaji JUHUDI kwa kuonyesha UBINGWA WAKO kwa kitu kingine hata ikiwa ni kwa TAALUMA yako ya KULAMBA PEREMENDE ili kusahaulisha WATU matumizi yako YASIYO MAHIRI katika ya KUSHUGHULIKA na PIPI KIJITI katika PIPI iliyo na LIJITI na yote ni ili UPENDEKE tu na ukweli ni kwamba HUPENDI PEREMENDE.:-(
Swali:
Unafikiri mtoto mzuri ukimzoea HUWA unakumbuka kuwa mwanzoni ulidhani uzuri wa MTOTO MZURI wake KWAKO MWANZONI ulikuwa ni SPESHO?
Nakatisha WAZO na kama nimekukwaza SAMAHANI KIBINDA NKOLE, Kadoda au weye Binti Khalufani!
Ngojea Shania Twain aongee katika-That don't IMPRESS ME MUCH
Au turudi tu TANZANIADr REMMY amzungumzie - Karola
Na ni kweli,... ...... HUTUKANI kama HUKUJIFUNZA tusi NI NINI!:-(
Na,.. ...kuna MENGI unayoendelea KUJIFUNZA SASA HIVI ambayo hatuyajui na labda HUYAJUI kwa kuwa hayo si maarufu LEO kwa BINADAMU na yake bin-adamu ya KUJIFUNZA maeneo na jinsi ya kutumia ENEO!:-(
NDIO,... ...huhitaji KUJIFUNZA KUNYA ingawa ni kweli KUNYA huhitaji TAALUMA kama unataka KUNYA VIZURI .
Na.... .... ni kweli kama unahisi unapatia KITU ,...
...LABDA kuna KITU unafananisha nacho ambacho kwako ni MAFANIKIO ndio MAANA kwako hilo ni fanikio na kama hujui,...
....kumbuka hata KWA hilo ULIJIFUNZA!:-(
NA NI KWELI kwa bahati MBAYA,.. ...hata UJITAHIDI VIPI,...
.... bado utakufa huku kuna KITU HUJUI!:-(
Samahani NAKATIZA wazo!:-(
Ngojea turudi ANGOLASAVIMBI aongee nisichoelewa na nisikufiche napenda Kipochugali mpaka nishadeti Wabrazili kadhaa kwa kisa CHA kunogewa tu na WAONGEAVYO Kipochugali.:-(
Na ni kweli sijawahi deti Mpochugali wa Pochugali:-( SAMAHANI kwa kujielezea kubwa kuliko katika swala la faragha na lisilo na UJUMBEmzuri hata kwa KIFARANGA.:-(
Huyu basi Savimbi adanganye wananchi kidogo kama afanyavyo KIKWETE kama naye hakujifunza kwaNYERERE....
Au tu LEADBELLY atusaidie kubadili hali ya hewa kwa ambacho bado sikielewi ingawa naelewa LUGHA katika...-Goodnight Irene
ASANTENI wadau WOTE na hasa ambao hamnitengi kama hawa waliopo kwenye picha zangu za JUUUUZZZZZI ya JAANA!:-(