Ukipenda ,...
.....KIJAMBO cha mpenzi kinukacho sio BUGHUDHA.:-(
Swali:
AU?
Ukipenda NI kama tu UKIAMINI dini yako ndio ya kweli,....
.....utamu wa kibano chake kwa wapendao burudani za sehemu za siri watadai kiwepo hata mbinguni ingawa ukikifikiria baada ya kumchoka mpenzi LABDA ni BUGHUDHA.:-(
Kwa kifupi nilitaka kukuuliza MHESHIMIWA :
Hivi ni mangapi unamficha MPENZI?
Huwa unamstua mpenzi kuwa ananuka?
Si unajua kunavitu unavifanya wakati umelala na washuhudiao ni watu WENGINE?
NDIO,....
... kuna uwezekano UKISINZIA kunavitu unafanya na huvistukii tu ndio maana UKIZINDUKA unashangaa jirani yako ana BENZI uitakayo halafu wewe bado hata Corolla YAKISHIKAJI huna.:-(
Ndio,...
.... ukisinzia KUNA KITU unafanya zaidi ya KUSINZIA na kimojawapo ni kuachia vyako WENGINE bila kujijua na LABDA ukijiuliza MWENYEWE unaweza kudhani hivyo vyako wavishuhudiavyo kwako WATU wengine kuwa HUNA.:-(
NI WAZO TU a.k.a UjingaBUSARA HUU na nimeukatizia MHESHIMIWA ili usitishike!:-(
Mdomo wa kulia ndio huohuo wa KUTAPIKIA kilichoingizwa MWILINI.
Sehemu za siri zenye kiburudisho KWA WASIO MAPADRE ndizo hizo hizo zenye kutoa Uchafu mwilini au ndizo zilizo karibu na chakutolea uchafu a.k.a kimba/timba MWILINI.
Tako zuri ulipendalo wakati linatikiswa mtu akitembea eti ndilo hilohilo tumizi lake kubwa ni kukaliwa au tu kuficha kijambio mwilini.
Swali:
Kama unadharau kazi ya tako , unafikiri ni rahisi kukaliwa au kutunza kijambio?
Halafu eti mikono ya kuchambia ndio hiyohiyo isaidiayo kupeleka chakula mdomoni ili kiende Mwilini.:-(
Halafu eti Kitovu na Mavuzi KWA WA KUBWA zaidi tu yakuwatia madoa WATU kunauwezekano havina kazi MWILINI.:-(
Swali:
Hivi mkuu bado unanisoma tu?
Unauhakika usomi ujinga ?
Si unakumbuka kusoma ujinga ni mazoezi ya akili pia?
Ndio,...
... eti limwili la binadamu lina KICHWA na moja ya tumizi la KICHWA sio kusoma NA wala sio kutumia akili!:-(
NIMEACHA wazo MHESHIMIWA!:-(
Hebu Alpha Blondy akite-LES CHIENS
Au ngojea tu tubakie Ivory Coast ili Alpha Blondy akune kwa- Brigadier sabari
Au tuhamie Ufaransa kidogo katika kubadili ili DAFT PUNK wanyuke katika kupoza mshawasha kwa ushauri- Make love
Au tubakie hapahapa Ufaransa ili St Germain wafankifai kwa mara nyingine kwa ndude- Sure Thing
[Tahadhari:Kuna uwezekano wazo limepindia kushoto zaidi ya kulia katika taralila hii!]
Katika kuchagua,...
... unaweza kuwa unatishika NA MAJINA yaambatanao na wenye taaluma kuliko hata TAALUMA yenyewe waliyonayo kwa kuwa ukifikiria UNAWEZAKUSTUKIA ,...
.... kuna uwezekano NESI na DAKTARI vipofu wenye utaalamu na GOVI wanaweza wakawa wazuri katika tibabu lako LA KUKATWA JANDO kuliko NESI na DAKTARI waonao lakini utaalamu wa kucheza na GOVI kimatibabu hawana.:-(
Swali :
Si unaweza kutishika tu kwa kusikia NESI na DAKTARI watakaokutibu ni vipofu wakati gonjwa lako linahitaji ajuliaye kupapasa na wala sio aonaye?
Unauhakika ni asilimia ngapi ya magonjwa uliyowahitibiwa NESI au DAKTARI alikuwa anatumia macho kuyaona ili upewe KLOROKWINI?
Ndio,....
.... labda MAHUBIRI mazuri ambayo yatakufanya uende mbinguni MWENYE NAYO ni yule umkwepaye kumsikiliza ukiwa na nyege za kutishwa kuhusu JEHANAMU au SHETANI kisa KIUTAMBULISHO anaitwa tu KIBAKA , kiruka njia, MPAGANI au tu KIDUME anajulikana kwa kupenda kukuna sehemu za siri wakati anaongea na WATU hadharani kitu ufikiriacho kuwa si sahihi kufanyika kwa akuhubiriaye kuhusu MUNGU hadharani.:-(
Ndio,...
... inawezekana moja ya kimsaidiacho MGONJWA kupona ni imani yake tu kuwa ANATIBIWA vizuri na MTU au MADAWA yanayoaminika kitu ambacho kinasababisha pia KWA IMANI hata manabii wa uongo wanao watu LUKUKI wakirio kuwa waliponywa nao HADHARANI .:-(
Swali:
Si unajua nesi akuchomaye sindano aliyevaa glovu anaweza akahatarisha imani yako ya kupona ugonjwa kwa VIDONGE alivyokupa ukigundua wakati anakupa vidonge alitoka haja kubwa na hakunawa mikono vizuri baada ya MTAWAZO ingawa mikono yake haijagusa vidonge kwa kuwa kavaa gloves?
Si umeshawahi kusikia eti hata YESU alikuwa anasema ``IMANI YAKO IMEKUPONYA´´?
Sitanii, wewe kwako ni afadhali Nesi au Daktari wako ndio awe KIPOFU?
Kama wewe sio kipofu umeshawahi kufikiria KIPOFU anakuaminije wewe bila kukuona au tu anastukiaje unabonge la makalio?
IMANI nishai,...
.... inaweza kusababisha uamini mke wako ulimkuta bikira wakati unamjua mtoto wake ULIYEMKUTA NAYE alelewaye na wazazi wake.:-(
Imani NISHAI,....
.....kwa kuwa inawezajengwa bila USHAHIDI kama vile tu UDEKUVYO KWENYE MASWALA YA DINI ila kwa imani tu UKAAMINI UNESI au UDAKTARI haumfai KIPOFU kwa kuwa kwa imani unaamini ILI DAKTARI akutibu malaria inahitajika AKUONE ili ustukie kama anakuelewa hasa kwa jinsi wakati anakudadisi ili kujua ni GONO au MALARIA ndicho kinachokusumbua UMDEKU anavyokuuzia kwa huruma na upendo LISURA lake.:-(
NI wazo tu hili USINUNE Mheshimiwa!
Cheka basi kidogo !AU?
Basi bwana NIMEACHA!:-(
Au tu tupate mnyumbulisho kutoka kwa GILBERTO SANTA ROSA anyuke kwa - VUELA LA PALOMA
Au tu Machel Montano na Xtatik wanyuke tena - Big Truck
FIKIRIA hii spichi ingekuwa ni ya RAIS mmoja wa TANZANIA na asemacho hapa Martin Luther King Jr kiwe kinamaa kuwa huyo Rais wetu MTUKUFU kashaona TANZANIA ielekeapo KUNAUNAFUU kwa MTANZANIA MNYONGE na kunanukia bonge la pilau[hasa kama wewe ni mpenda pilau] hebu sikiliza kwa mkao wakumtafakari HUYO Rais wa TANZANIA kuwa anaongea kuwapamoyo WATANZANIA
[Tahadhari: Wazo katika taralila HII limepinda !:-(]
Ukifikiria utastukia kuwa katika kila uliogopalo kuna MWINGINE anashamiri katika hilo bila UOGA uliokuwa nao KUHUSU HILO wewe.:-(
Swali:
AU?
Ndio maana,...
..... uchochoro UUOGOPAO kuupita kuna ambaye hauogopi na kageuza hapo makao a.k.a OFISI yake ya KUKABIA watu ambaye kwa jina la kitaalamu huyo ni mjanja kwako.:-(
Ndio maana,....
.... kwa uogopaye WACHAWI unajua kuwa kuna watu ambao hawaogopi uchawi kitu ambacho kimewasaidia zaidi ya kutoogopa uchawi kuliko aogopaye uchawi wamekuwa wenyewe WACHAWI labda HATA katika eneo lako.:-(
Ndio maana,....
.... katika ujasilimiamali weye ukichacha hata kama ulishawahi kujichungulia ukastukia unasehemu nyeti kisura ambazo zinauzika MTAANI na unawajua waliojenga nyumba na kupandishwa vyeo kwa UFUNDI wa tumizi la NYETI waweza kujikuta unaogopa kufanya mauzo ya NYETI ZAKO NONO kama wengine ambao walitatua tatizo lako katika eneo lako kwa mauzo ya kiungo kitu ambacho unaamini hakiwezekani kwako.
Swali:
Sasa kwanini wengine na sio wewe?
Unafikiri wengine wanakuzidi nini mpaka wanafanikiwa kuwa mafisadi katika UFISADI uushindwao , wakati wewe unadai unamuogopa Mungu hata kuonjesha watu uzinzi kama wenzio wafanyao UZINZI ambao vifaa vyake vya tumizi kama hamu na pembejeo za kazi unazo?
Ndio,....
.... inasemekana MAKUZI ya mtu yanaweza kumsaidia mtu kutokuwa na tabia ya kudokoa MBOGA JIKONI hasa akihisi hakuna watu.
Ndio,...
.....inasemekana MAZINGIRA yanasaidia kurahisisha baadhi ya MDADAZ kutoa nyonyo kwenye umati KIRAHISI ZAIDI katika swala muhimu la kucheza SINDIMBA KIFUA WAZI hata kama tukiachilia mbali lile swala la KUTOA NYONYO kirahisi zaidi kwa baadhi ya mdadaz HADHARANI katika kunyonyesha TU toto lenye njaa ambalo limeanza kulilia NYONYO a.k.a HOTELI YA MTOTO mbele za watu.:-(
Ndio,...
....inasemekana ELIMU inaweza kusababisha MTINDIO WA AKILI usababishao TOFAUTI YA WASOMI WAWILI usababishao aliyeelimishwa KIKRISTO akubaliane na MTINDIO WA AKILI wakuwa UKIPIGWA KIBAO SHAVU MOJA geuza na jingine UBWENGWE TENA na aliyeelimishwa KIISLAMU au KIYAHUDI apate MTINDIO WAAKILI umsababishao UKIMBWENGA KOFI SHAVU la kulia akurukie kichwa halafu kabla hujatulia akukabekabali ifuatwayo na gonge la ngwala na kama unamakende labda ayasigine wakati anakutukana PAMBAFU WEYE mbele za watu.:-(
Swali:
Unabisha?
Cha kusikitisha ni kwamba,....
.... labda weye kisa sio MWIZI, malaya na UNAOGOPA WACHAWI, giza na unatabia pia ya KUTOPENDA ukitoka tu chooni mtu MWINGINE aingie baada yako kwa kuwa unajua unautaalamu mkubwa wa kunukisha choo HARUFU MBAYA kitu ambacho hupendi watu wajue,...
... tabia zote hizo labda ni zako tu kwa kuwa kama ni MALEZI , mazingira hata elimu , vyote vinalingana na wengine kwenye familia yako BABA mmoja na MAMA mmoja mliokulia nyumba moja mkaenda shule moja WASIO NA TABIA HIZO na pia hata katika MTAA WENU pale kijijini JANGILI, mwizi wa mapera na FISADI wote ni ndugu zako wa damu ingawa baba aliwazaa nje NA WEYE eti ni ASKOFU ambaye mtoto wako wa pili wakike atakuwa mchawi baadaye akikua vizuri baada ya jitihada zako zote za MALEZI mazuri ya staili za kumfunza kumuogopa MUNGU vizuri.:-(
Cha kusikitisha ni kwamba,....
.....labda WENGINE wanaonekana wanaweza ndio maana ni MAPROFESA siku hizi ingawa wewe ulikuwa unawazidi akili darasani na bado weye ni mesenja kwa kuwa tu HUJARIBU KITU hata katika kusawazisha tu maisha yako kitu ambacho kimekusaidia kutogeuka MALAYA au mchawi au tu kisababishacho watu usiue,...
.....ingawa pia kimesababisha usijaribu kwenda shule ANGALAU YA MASWALA YA JANDO zaidi angalau ikusaidie kumridhisha umjaliye zaidi hapa duniani ambaye ni MKE WAKO angalau katika tendo lililobarikiwa na SHEKHE liwasaidie kuujaza ulimwengu hata wakati lengo la tendo ilikuwa liwe ni KIBURUDISHO MURUA TU, wakati MKEO ANARIDHIKA vizuri.:-(
Swali:
AU?
NDIO,...
..... ni kweli KADODA sio KADALA,.....
......na labda hiyo ndio sababu kubwa ingawa GIZA lisilo mdhuru KADALA hilo halimdhuru KADODA,...
...ila KADODA anaweza geuka JAMBAZI ajifichaye GIZANI na KADALA akageuka aogopaye GIZA kwa kuhofia ajifichaye gizani ingawa kiukweli KADALA hamuogopi KADODA mchana.
Swali:
Ushawahi kujiuliza kwanini aogopaye MAJINI hajiulizi inakuaje kuna mwingine kazi yake ni kwenda kwenye wenye MAJINI ili kuyaagua na kuyafukuzilia mbali?
Ushawahi kujiuliza kwanini UOGOPACHO kukifanya na hapa siongelei swala la kujamba hadharani wengine wanakifanya hilo KIRAHISI kama wanafyonza AISHIKIRIMU YA UKWAJU vile kitu ambacho weye huwezi?
Ndio,...
..... WEWE sio WAO na labda ndio maana LIMPENZI lako baya NA HULIPENDI VIZURI ingawa lenyewe LINAKUPENDA SANA kitu kilichorahisisha ukonalo kwa kuwa ulipendalo kikweli lile ZURI KINOMA UNALIOGOPA KULIAMBIA kitu ambacho wenzio wanafanikiwa KUFANYA ndio maana wana LIMPENZI ZURI ingawa limpenzi lenyewe eti HALIWAPENDI VIZURI.:-(
Ndio,...
.... labda MALEZI, elimu, MAZINGIRA na.......
.... vyote vinategemea wewe ulizaliwa ni MTU WA AINA GANI na kuna uwezekano pamoja na KUKULIA MAZINGIRA ambayo UZINZI ni DHAMBI ukifanya mazoezi vya kutosha unaweza kujikuta weye ni PROFESA WA UZINZI kama tu wengine ambao wamefanyia mazoezi UFISADI, KABUMBU, au hata kubulogi walivyogeuka MAHIRI ingawa hawakuzaliwa kukiwa na KOMPYUTA na wala BLOGU hazikuwepo.:-(
Swali:
Hivi si kuna uwezekano kila mtu kazaliwa na chembechembe za UFISADI kwa hiyo klihitajikacho ni NAFASI ya KUFISADI na MAZOEZI ya kunoa jinsi ya KUFISADI vizuri bila kudakwa kama MAFISADI mahiri wajulikano ila ushahidi hakuna?
Unauhakika kwanini ni WENGINE na sio wewe MALAYA wakati mchakato wa maisha ni uleule kwako na kwao?
Ndio,...
....Nakubaliana na WEWE,...
...kunyoshea wengine vidole KUNA utamu wake.:-(
NAACHA WAZOhili nikishukuru uwepo wa MIMI na WEWE, wao na WALE kitu kisaidiacho uwepo wa MAFISADI kwa kila uwepo waogopao KUFISADI, uwepo wa MALAYA kwa kila awapo mchoyo wa kuuza tendo la unyumba, UWEPO wa WENYE IMANI KALI kwa kila WAWAPO WASIO AMINI kitu ambacho kinaifanya DUNIA HII iko ilivyo kitu ambacho naaamini hakiko HIVI au HAKIKUUMBWA KIWE HIVI KIBAHATI MBAYA !:-(
Nakutakia SIKU KIBONGE Mheshimiwa hasa ukikumbuka hili NI WAZO TU!:-(
Tubadili MUSHKELI kwa kumsikiliza YOUSSOU N'DOUR anyuke mkito-Bamba
Afroman abadili kidogo kwa -Because I got High
Au tu Warrior King aje live katikakurudisha ustaarabu mkuno -Education
....kama tu wasio hamu ukiwachunguza nyuma ya kitunza kinyeo labda wana TAKA.:-(
Leo na HAMU...
...taka na TAKATAKA na kwa kuwa LEO laweza kuwa jina la MTU labda ni taka ,.....
.....katika kitakiwacho KWA WATAKAO LABDA ni TAKATAKA.:-(
Leo katka tamu ya HAMU,...
... labda vyote VITAKIWAVYO kwa ASIYETAKA ni takataka.:-(
Swali:
Ushawahi kuwa na hamu NA KITU halafu wakati hupendi mabiringanya ukaona biringanya na kufikiria labda BIRINGANYA tamu?
Umeelewa?
Si unajua si lazima uelewe?
Wazo la leo NI HAMU na hamu inawezekana ikawa ni ya BAGIA katika siku ya tamanio la mishikaki kwa mwenye chachandu ambaye ukimpa MSHIKAKI kwa kujivunga anaweza kusema anataka ingawa atakacho sio CHACHANDU wala MSHIKAKI.:-(
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA KIFALSAFA na usijali kama huelewi hii KINDEGATENI!:-(
NI wazo tu hili kwako AJUZA!:-(
Ndio NI WAZO TU HILI MKUU WA WAJANJA na sitaniii hata kwako Mdada mwenye HAMU UIFICHAYO KIJANJA na PAPAA mwenye HAMU ambayo ina kufanya uchovye cha hausigeli KIJANJA !:-(
NIMEACHA!:-(
Hebu nibadili kwa kumpata The great MIKE TYSON atukumbushe ni nini waheshimiwa wasio wajanja wakumbukavyo katika ya -Mike Tyson's
Au tu Richie Spice anyutrolaizi lawalawa na MKITO - Uptown Girl
Au tu Richie Spice akiwa ni miongoni wa watu wavutao wakisifiao na hakuna siku nimekutananaye kimemzingua avutachokimemzingua aendelee halafu jiulize ni wangapi UWAJUAO watumiao wako fiti hivi kuanzia kutunga vyombo mpaka kuimba walivyovitunga kama afanyavyo huyu katika ndude- MVUKE
Au tu nimuachie huyu hyu Richie Spice asifie katika kitu -Brown Girl
....ndio maana MALAYA na MLOKOLE wote wanafanikisha wakilengancho kidude walichokinuia kukipandisha mzuka.:-(
CHA KUJIULIZA:
Hivi Tanzania na RWANDA kama ni nchi zenye NIA kwa nini RWANDA inasemekana sasa hivi kupatia njia wakati Tanzania bado tokea ipate uhuru kwenye nia zake hapapatikani njia au ikipatikana inabonge la makorongo na kama unatakakuelekea Kigoma unaweza jikuta Mbinga?
Hujastukia ni kwanini naanza kufikiri PENYE nia pana njia MBOVU pia?
Nalikatiza hapa hili wazo nyoko a.k.a shenzi kiduchu!:-( BAADAYE!
Hebu tuburudike kwa kudeku maswala ya Wazungu na Watu weusi bila kuwasahau wenye rangi nyingine mwanana katika kidude kitafitiwacho kwa watoto -STUDY shows how children view race bias
Au tuendelee tu na burudani hiihii katika-
Au hebu tu Jocelyn Beroad abadili kidude kwa -Ti tak isi
Au na Malaika nao walete katika kubadili mkuno ndude-Destiny
``SIMON eeh, MSICHANA ana kesi huyo!´´- ni moja ya onyo hasa marafiki zangu wa MOROGORO hunipa pale wakihisi kuna ZALI aka MTOTO MZURI ananilenga au tu kinamna imetokea mie mwenyewe nimelisifia ZALI kitu nikimaanisha labda mwendo, dimpozi au tu miakili ya kimwana katika kunyambulisha hoja za kitu zikatokea kustua marafiki zangu kuna kunafununu ya kaudhaifu napandikiza kwa ZALI ,....
.... kitu ambacho kinawafanya wawe na wasiwasi nini kitatokea bila miye kuijua HISTORIA ya KIMWANA.
Na wakisema MTU ana kesi MAANA YAKE huwa kuwa inajulikana kashafiwa labda na MME wake, Mke wake, poozeo, au tu shughuli zake vitani wengi wanamuhusisha na mauaji ya MPENDWA mtoto wa mtu ambaye anaitwa marehemu siku hizi kutokana na gonjwa wajanja walihisio lilipewa ujanja na busti ya mashambulizi kwa kuwa mwilini alikuwa hana KINGA YA MWILI.:-(
Kwa kifupi,...
... katika pitapita zangu hasa MOROGORO na ARUSHA nimekutana na mazingira yanikumbushayo stori nilizokuwa nasikia kutoka kwa BABU upareni jinsi utafiti ulivyokuwa unafanywa katika kuhakikisha KIDUME anaopoa ZALI lililotafitiwa ili kuhakikisha KIDUME huingii zali katika kujipatia KIMWANA.
Kwa kifupi zaidi hasa kama wewe hujatokea BONGo kwa muda mrefu,....
......siku hizi SI JAMBO LA AJABU ukimchekea mtu wakujalio KUKUSHUSHIA BONGE la historia ya UMCHEKEAYE hasa katika mrengo wa ana KESI NGAPI.:-(
Swali:
Unafikiri leo hapa BONGO kama hupuuzii mambo unaweza kujiamini KUPENDA mtu?
Samahani NAANZA UPYA taralila hii kwa mwendo wa kusuasua!
UKIMWI UPO!
....Ila UKIMWI wa watu kumtungia mtu nao UMESHAMIRI maeneo kibao niliyokatiza TANZANIA na KENYA mpaka sasa.
Lakini MAPENZI yapo!
... labda pia ni kitu kizuri HICHO kuwa bado MAPENZI YANASHAMIRI hata kwa wale ambao kwa kuwa WAMEWAHI KUFIWA basi ukiwachekea WANAOKUJALI hata kwa sauti ya zaidi ya ile ya TISHA TOTO watakustua kuwa TOTO ZURI lina kesi a.k.a LIMESHAFIWA tayari na limpenzi lake.:-(
NA ile sifa ya PESA kuwa ni sabuni ya roho bado IPO!
... na PESA katika uwajibikaji wake hasa UKIDHANIWA UNA PESA unaweza kujikuta kuwa kuanzia MALAYA, wababaikaji wa kawaida au mpaka mchumba wa ASKOFU wote wamekulenga na kama unajali TAMUTAMU ZA GHAFLA unaweza kujikuta umejitafutia kesi KILAINI wakati wala hupendwi wewe ila ni POCHI lako tu ambalo wala halina kitu kihivyo hasa ukizingatia pesa zilizotunisha POCHI labda ni kodi ya nyumba kwa kuwa kujenga NYUMBA pesa huna.:-(
Swali:
Unafikiri ni wangapi wametungiwa kuwa wanamdudu BONGO nyoso na wapiga taralila tu?
Hivi wewe hujawahi kutishika na LIMTU zuri kisa maonyo ya watu ?
Unafikiri watu wanatoa wapi historia na siri za watu ukizingatia ukiulizia unaweza ambiwa mapaka ya chumbani kwa watu na watu ambao hata sebuleni kwa huyo mtu hawajawahi kuingia?
Ni STORI FUPI tu nazokutananazo safarini MHESHIMIWA na wala usijali kwa kuwa NAACHIA HAPA.
Ngojea miye niende zangu BAA kufanya mazoezi ya kuacha kunywa POMBE unajua tena wikiendi bado.:-(
BAADAYE!
Hebu tujikumbushe Loon wa enzi za Badboy akiwa na Mario Winans katika mnyuko- Down For Me
Au ngojea tujikumbushe Loon aongeleye UISLAMU na Allah baada ya kugeuka
Mipango ya HARUSI,...
......ambao wanaandaa HARUSI hufanikisha HARUSI TANZANIA.:-(
Aandaaye bajeti ya KICHENI PATI Tanzania kabla ya HARUSI,....
..... bonge la profesa wa bajeti za KITANZANIA kwa kuwa KICHENI PATI zina tako kubwa kweli kwa mpenda matako makubwa KIUFANIKISHAJI katika mtikiso TANZANIA.
Swali:
AU?
Si unajua Harusi hufanikiwa BONGO ila kujenga zahanati ni shughuli TANZANIA kama tu kutafuta hela za kuchangia ada ya shule?
Ndio,..
... kuna walipa kodi BONGO.:-(
Ndio ,...
...tuna RAIS , wabunge, diwani na mpaka .... BONGO.:-(
Swali:
Hujawahi kufikiria kama TANZANIA ingeendeshwa kwa umakini wa waaandaa HARUSI wa TANZANIA hata kama ITAENDESHWA kama kile kikao cha kuhusu chupi ya bibi harusi haijalipiwa labda TANZANIA ingeshakuwa imefanikiwa kwa kuwa kufanikiwa kwa tendo linuiwalo KWENYE HARUSI huwa ni muhimu kuliko chupi YA BIBI HARUSI ni bei gani katika kulifanikisha?
Kuna sababu NYOKO zisababishazo MWALIMU ajisikie MAISHA YAKE yanaleta MAANA kwa kufundisha,...
.....kama tu MALAYA ajisikiavyo MAISHA YAKE yanaleta maana baada ya kurizisha mtu kwa ufundi na UMAHIRI WAKE katika kazi yake muhimu ya kusaidia watu katika MGAO wa utupu.:-(
Swali:
SI kunauwezekano maana ya maisha ni nyoko ndio maana MENEJA na MESENJA wanaweza wakawa wanaridhika na kazi zao ndani ya ofisi moja?
NAACHA HII TOPIKI HAPA ila ruksa kwako kuiendeleza kimawazo hata kama KWA USTAARABU WAKO unahisi nimetukana .:-(
.....kitendo kidogo ambacho kila mtu anajua kila mtu anakifanya inaweza kuwa ni ujanja kukifanya siri.:-(
KWA binadamu,...
... haki ya nani hata KUJAMBA kama nia na malengo yako huna uhakika na wakuzungukao wana kuathiri vipi inawezekana kama umejaliwa USHUZI WAKATI HUO na ukautoa kwa neema na furaha labda weye ni MJANJA na unaweza kutajirika kwa kuwauzia waliokusikia ukijamba kwa furaha mbele za watu hiyo SIRI.:-(
Swali:
Unabisha?
Ndio,...
... kuna ambao walistukia tokea UTOTONI kuwa kujamba HADHARANI SIO USTAARABU na wakaanza hapohapo mazoezi ya KUJAMBA kwa siri.
Swali
SI unajua sikuzungumzii wewe?
.....na HAKI YA NANI TENA,...
... kama hao watu kama WANANUKIA PAFYUMU NZURI unaweza usistukie wakati umekutananao WAKINUKIA VIZURI kuwa wakati huo labda wametoka KUJAMBA au kwa lugha ya kitaaalamu ,...
....wametokea kuachia USHUZI.
Swali:
Unauhakika ni mara ngapi katika uwaaminio kama vile , PADRE, mchungaji , SHEKHE, RAIS ... wakati wanakupa hoja zinukiazo vizuri bila wewe kustukia walikua wanaachia ushuzi wakati huo WAKIKUPA HOJA MWANANA au walitoka kuachia ushuzi wenye undugu na mayai yaliyooza kitu ambacho huwahusianishinacho wakati msikilivu na wakati huo una busara?
Si unajua kuna uwezekano hapa siongelei KUJAMBA aka USHUZI ?
... lakini kuna MAELEZO kwa MPENZI labda sio busara MAMA YAKO ajue .:-(
Ndio hata katika MTONGOZO bomba,...
.... ambao unasababisha mahausiboi wote mtaani wanafikiri dili ni MAMA MWENYE nyumba WEYE ya kwenye kona ndio unalipa zaidi katika siri za ushujaa huo wa mama mwenye nyumba,...
....si lazima SIE WENGINE tujue.:-(
Swali:
AU?
Na wakati MJOMBA anasikiliza MAONGEZI alengwayo SHANGAZI,....
....inaweza sababisha MPAKA MJOMBA AKATWE mizizi ya UTAMU wa SHANGAZI kama nia ni kuokoa uwezekano hata wa uwezekano ZILIPENDWA YA SHANGAZI inaamsha anasa ZILIPENDWA za MJOMBA kisa kasikia tu aambiwacho shangazi hasa kama kiokolewacho ni UJOMBA TU.:-(
Swali:
Kwani humjui MTU ambaye anataka KUSIKILIZWA ili tu aeleze wengine kisa kagundua kusikilizwa ndio tamu yake ilipo na KWA HIYO ANAHISI ITABIDI aongee tu hata ya chupi wakati kikao ni cha sidilia?
SI unajua kuna uelezwayo mengi ambayo hutaki kusikia ila kwa kuyasikiliza kuna watu siku hiyo walilala vizuri kisa wamehisi wamesikilizwa?
Unafikiri aelezaye yasiyokuhusu hafanyi hicho katika kujitafutia shughuli kama tu afanyaye mtu bila kuwa na hamu?
NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA samahani!.:-(
Hebu tubadili kwa ndude ya Gil Scott Heron ,Jay Z asaidie ili watu fulani wasikie iitwayo - Home Is Where the Praying Is
Au tu GIl Scott Heron ailete kavukavu ndude katika -Home is where HATRED is
Au tu ngoje Gil Scott anyuke kwa-Dont give up Read more...
... ina sura kama TAKO kwa kuwa TAKO KATIKA SWALA ZIMA LA KUJISAIDIA kinamna ni NENO TU.:-(
NGUVU,....
.... inaweza kuwa UCHOCHEZI kama imeelekezwa kwa ambaye NGUVU YAKE ni ile ambayo haina nguvu kwa kuwa HAJIAMINI NA AFANYACHO CHENYE NGUVU na hata KABLA HAJAKIRI afanyacho ni kupiga KELELE KATIKA MFANYO UHITAJIO VITENDO kitu ambacho kinguvu kinahitaji vitendo na sio kukivulia chupi kitaralila TU.:-(
NGUVU,...
...ukiwanayo UNAWEZA usijue nini ni NGUVU kwa kuwa katika dunia ya sasa unaweza usijue mwenye nguvu ni RAISI au FISADI MESENJA WA RAIS AMBAYE ni jirani yako katika kuhakikisha kwa shilingi ngapi una pata choo kinamna ambayo unaweza ukawa unamlaumu mpaka mama yako ambaye katika mchezo mzima alicho kifanya ni kukuzaa tu.:-(
Swali:
Unauhakika nguvu ni nini?
Unauhakika naongelea nini?
NI WAZO TU HILI!:-(
Hebu Frankie Paul aje live kwa kurudia kumsifia mtoto mzuri-SARAH
Au tu turudi studio Frankie Paul amsifie tena -Sarah
... sijali harufu na labda wewe hujagundua tu bado kuwa pamoja na harufu kuwa ni moja ya kifanyacho pilau kwako inavutia BILA KUIONJA ila hujali harufu ndio maana labda hata kuna choo fulani ushawahi kukikimbilia ingawa kinanuka KIHARUFU.:-(
Ni kweli,....
...tamu ukionja kama kwako ni tamu kweli kimgido ,...
...kama inanuka,.....
.....cha mwisho kusumbua MUONJO WAKO si harufu.:-(
Swali:
AU?
Swali kwa MPENZI kinuka MKOJO;....
SI unajua anogewaye na CHAKULA wakati wa njaa huyo hana njaa vizuri?
Si unakumbuka mwenye njaa umuhimu ni kushiba na sio kushughulika na swala la maharage yanajambishaje?
Ndio,...
....kuna uwezekano mkubwa anogewaye na CHAKULA wakati kinanuka ukitaka kumgawia tena chakula katika KIBAKULI KILEKILE akakubali kwa nguvu zote KUGIDA tena,....
.....maana yake ANAUMWA na njaa VIZURI huyo, zile njaa za kumgeuza asiye penda kugida akagida tu hata ukoko wa mlenda wa jana kwa kuwa KULA CHAKULA ni tofauti kama ulaji wako ni katika staili ya kusikilizia utamu au tu ni kwa kuwa unakula kwa kuwa una njaa.:-(
NI WAZO TU HILI ambalo lina UTAFITI HAFIFU NYUMA YAKE mheshimiwa .:-(
NAACHA WAZO!
Hebu Twende SenegaliViviane Ndour abadili kwa mfinyo- Fima Tollu
Au tu AFFO LOVE alete alete tena coupe decale katika-INFIDELITE Sexy Boulance