LEO nawatakieni UCHAGUZI Mwema !
Wiki hii nimejikuta nikisikikiza malumbano ya UCHAGUZI kutoka kwa marafiki watokao BRAZIL, Ivory COAST na Tanzania ambao wote LEO ni siku ya kupiga kura katika NCHI ZAO.
Katika kuilenga TANZANIA:
Tuombee AMANI na uchaguzi huu uende SHWARI!
MUNGU IBARIKI TANZANIA!
Hebu Ze comedy wabadili kwa -Muziki mnene huu
Ze comedy katika - Kurudisha chenji muhimu
Au tu ngojea Lágbájá na abadili tu na- Bling Bling Panda
AU tu Lágbájá ambaye ni msanii nimuheshimuye labda kuliko wote Nigeria sasa hivi arudie-Gra gra
Read more...
Kila la kheri WABRAZIL,...
......WaIVORY COAST na WATANZANIA mpigao kura leo!
Katika kuilenga TANZANIA:
Tuombee AMANI na uchaguzi huu uende SHWARI!
MUNGU IBARIKI TANZANIA!
NI HILO TU!
Hebu Ze comedy wabadili kwa -Muziki mnene huu
Ze comedy katika - Kurudisha chenji muhimu
Au tu ngojea Lágbájá na abadili tu na- Bling Bling Panda
AU tu Lágbájá ambaye ni msanii nimuheshimuye labda kuliko wote Nigeria sasa hivi arudie-Gra gra
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Aliyeandika kuhusu swala la TITI labda sio HASA ni yule MTAALAMU wa MATITI!:-(
>> Saturday, October 30, 2010
Wakati unakula MLENDA,....
....kumbuka TU kuna WATAALAMU WALIOKUBUHU KATIKA KUJUA ambao wako kimya,...
....wasiopata nafasi ya kuandika KIUTAALAMU WAO kuhusu MLENDA,....
...au wasiojua tu jinsi ya kusimulia KIMAANDISHI jinsi ya kupika MLENDA wakati unasikiliza AU UNAWASOMA waongeleao MLENDA.:-(
Na umsomapo Simon Kitururu akiongelea kipengele cha mwili kitumikacho sana MSALANI,....
..... kumbuka tu kuwa kuna wataalamu ZAIDI wa jinsi ya kubana matumizi ya muda na umadhubuti wa utumiavyo kipengele huko MSALANI ambao wako kimya kwa sababu mbaimbali zikiwemo za kawaida kama zile za HESHIMA kwa kudhani wakiongelea kipengele anuai wataonekana kama SIMON kuwa si WAHESHIMIWA .
Swali:
- SI unajua labda SHEKHE YAHYA pamoja na kutoongelea zaidi BIBLIA kama aongeleavyo utabiri labda anaijua BIBLIA kuliko hata ASKOFU kadhaa za KILUTHERI katika mpekecho wa BIBLIA?
- Si umestukia kuwa labda kunauwezekano ingawa ni wanawake ndio wenye titi lenye ujazo NA UTAALAMU WA JINSI YA KUISHI NA TITI NONO wa kutosha lakini labda kuna mwanaume ndio muongeleaji titi zaidi?
Nawaza tu MKUU!
Hebu ARRESTED DEVELOPMENT warudishe ustaarabu kwa-Revolution
Walete- Tennessee
Arrested Development warudie-Mr Wendal
Au tu ARRESTED DEVELOPMENT wamalizie na-People Everyday
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Binadamu WAKIZOEA KITU hupenda kuendeleza kutenda walivyozoea HATA kama walivyovizoea havifanyi kazi tena hata katika jinsi viamshavyo PENZI kama MCHUMBA ageukapo MKE!:-(
Binadamu wakizoea hata kuliambia limtu ``I LOVE U!´´,....
.....wanaweza kujikuta WANAENDELEA TU KULIAMBIA limtu ``I love U´´,....
....hata kama siku hizi hawalipendi hilo LIMTU ki ``I LOVE U!´´,....
..... kisa kisa wamezoea tu na mazoea yamegeuka TABIA nyumbani wakati siku hizi ni HAUSIGELI apendwaye kuliko MKE hasa tokea HAUSIGELI ajulie KUJISOPUSOPU na kuzibua uzuri wake uliokuwa umejificha kwa KIDUME aka MME wa MTU chini ya miguu yenye MAGAGA, bonge la kikwapa na kadhalika nyingine kadhaa zilizokuwa hazina mvuto kwa kidume mwanzoni kutokana na familia KIFISADI ilivyo zoea kutafuta mahausigeli kutoka katika famili zisizojiweza ili wa MDHULUMU mfanyakazi wa ndani kwa kumpa mshahara mdogo kabla hajastuka.:-(
Swali:
- AU?
Ndio,....
.... watu wakizoea kuweka mbolea ya chumvi chumvi kwenye shamba lao,....
..... kirahisi wataendelea kutumia mbolea ya chumvi chumvi hata wakiambiwa inaharibu udongo wa shamba lao kama tu waliozoea kupiga kavukavu wakataavyo kondomu hata wakisimuliwa stori za UKIMWI.:-(
Swali:
- AU?
Ndio,...
..... binadamu hupenda kuendeleza walivyozoea hata kama walivyozoea havifanyi kazi tena,...
.... na labda ndio maana bado ndoa yako imedumu ukizingatia labda ulichuja utamu zamani tu ,...
.... kitunzacho uhusiano wako na MWENZI WAKO ni mazoea tu ya kuendeleza tu VILIVYOZOELEKA.:-(
Niwazo tu hili MHESHIMIWA !:-(
Jumamosi NJEMA!Hebu Snoop DOGG abadili kwa kitu-Sixx Minutes
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Wakati MOHAMMED ndio jina maarufu wapewalo WATOTO Uingereza na FINLAND!
Taka usitake kunakitu chaweza kukuingia akilini KITAFAKURI,....
..... kama utatafakari kuwa nchi kama FINLAND ambayo ni ya KIKRISTO mpaka SEREKALI ndiyo itozayo watu sadaka za KANISA kwa kukata watu mshahara kama kodi ya KANISA kwa ajili ya KANISA hasa la KILUTHERI ,....
.....katika data unakuta watoto wengi wapya wakiume MOHAMMED ni moja ya jinalitawalalo,....
.....pia nchi kama UINGEREZA ambayo kihistoria ni ya KIKRISTO ukisikia pia ni jina hilohilo MOHAMMED ndio linatawala.
Hebu deku watu wanasemaje kuhusu hilo UK...
Swali:
- Wakristo MPO ?
- Au ndio nyie mliozidisha kugeuza kipengele cha kutengenezea mtoto kuwa ni KIBURUDISHO MURUA tu KWA KUWA TAMU na mitoto hamzai kwa kuwa kuilea mitoto ni kibano kama kupanga foleni RTC kununua UNGA WA YANGA enzi za NYERERE baada ya vita na Mheshimiwa Idd AMIN?
NAWAZA TU MKUU usikonde!
Hebu Gilberto Gil abadili mkao wa wazo kwa kurudia -Aquele Abraço
Au hebu tubakie Brazil ELIS REGINA anisaidie kuendelea kubadili hali ya hewa hapa kijiweni kwa ndude -Madalena
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Ngojea RUMMY mutoto ya KARIAKOO aendelee... na ALIKO MWAKANJUKI aage!!
>> Friday, October 29, 2010
Nimemkumbuka tu mtoto wa kariakoo RUMMY aka Mr B aka Rumpunch kwa kuwa sijamuona siku nyingi!
Nafikiri mara ya mwisho ambao ni muda kitambo kidogo nilivyomuona ni tulivyopiga picha hiii...
Hebu aendeleze na bendi yake Mighty 44....
THIS love!
Abandike pia....
PUSH IT
Rummy nakusabahi Mkuu!
Pamoja sana MKUU!
Halafu watu MLIOKO au mtakao weza kufika HELSINKI,....
ALIKO Mwakanjuki aka DJ ALTUNEZ ambaye ni huyu hapa.....
AU huyu hapa na mimi....
Anaaaga marafiki waliokuwa naye mitaa ya ULAYA kwa kuwa anahamia bara jingine siku ya tarehe 13.11.2010 kama tangazo linong'onezavyo.....
Huyu namchagulia jiwe SHUB IN la FRANKIE PAUL
Pamoja sana MKUU!
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Sikiliza LABDA unaweza kuelewa, SIKILIZIA , na labda KWA HILO utapata OGAZIMU!:-(
[Tahadhari: Wazo katika TARALILA HII limepinda na linamapengo!:-(]
Tatizo moja LA WATU ni kuwa WANAPAPARA na,....
..... ndio maana wwanaweza kunogewa kwa papara kama WATANZANIA wawezavyo kunonogewa kwa papara na Waziri LIYATONGA MREMA kuliko,...
......Waziri MKUU MORINGE Sokoine.:-(
Swali:
- AU?
- Samahani kama huzijui siasa za Tanzania na kama hilo linakusaidia kutojua SIASA ya Liyatonga Mrema na Moringe Sokoine si nasikia sikuizi kunakitu kina itwa GOOGLE ambacho ukigoogle unaweza kujua kuwa Profesa Lipumba ni PROFESA kweli?
Kama HUNIELEWI,....
....tulia,....
...na wakati umetulia UKIKUNWA sikilizia,....
..... na akiguna SIKILIZA pia,....
...na labda KISIKILIZWACHO bila PAPARA katika MAISHA kinaweza mpaka kukuwekea wazi UDHAIFU WA DINI YAKO PIA katika tu kukuelewesha MACHACHE utakayo ELEWA au tu utakayo kuwa na moyo wa kukubali kuwa umeelewa na hayako kama uyafuatavyo kisa PAPA BENEDIKTI kasema usitumie KONDOMU,...... hata kwa kisingizio kuna kitu unajua sasa kuliko BABU YAKO kama wanasiasa wa CCM walivyojua hata kabla NYERERE hajafa kuwa kuna kitu alikuwa anawaficha kwa kuwa yeye IKULU alikuwa anaangalia BBC kwenye TV tokea enzi TANZANIA kunaaminika hakuna TV wakati wewe TANZANIA BARA KUWA NA VIDEO ilikuwa noma.:-(
SWALI:
- SI unajua ni RUKSA kutoelewa TARARILA HII inalenga hasa nini?
.....sikiliza LABDA unaweza kuelewa, SIKILIZIA , na labda KWA HILO utapata OGAZIMU!:-(
NIMEACHA !
WIKIENDI NJEMA kwa kuwa naiunganisha kiKHERI KWAKO Ijumaa hiii kwenye hiyo kitu WIKIENDI kwako MHESHIMIWA!:-(
Hebu SHAKIRA alete -LOCA
SHAKIRA arudie pia - HIPS dont lie
Au tu hebu BIG YOUTH awaulize TENA wajifanyao wajanja SIKU HIZI kuwa wakati SHUGHULI inafanyika mwanzo -Where were all dem boys
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Lile SWALA la kuwa pamoja na nguo zote ASKOFU ajivalishazo chini ya nguo kama WEWE bado yuko UCHI!:-(
Kuvaa NGUO labda PAMOJA na yote YA USTAARABU wa jamii ya yakwepayo kukabili tusi la ndani ya nguo,...
.......ni kwamba ,....
......CHINI YA NGUO yako au hata ya SISTA WA KIKATOLIKI aaminiwaye KWA KUSALI sana kama vile YESU ni MCHUMBA WAKE ,........ ni kama tu juhudi ya WASUKUMA kukataa wali haunogi ,....
..... au katika upande huohuo KINAMNA wa kuwa WALI SIO bomba sana kama MATOKE au KUMBIKUMBI WALIOKAANGWA kwa WAHAYA katika swala la ,....
.... chini ya nguo hata kama navyojaribu kutafuta lugha ambayo itakuwa laini na unastukia kuwa sijapata ni ,...
....uko UCHI!:-(
Kuna MAMBO yasiyouchi,...
....WATU wayafikiriayo mpaka yanageuza kifikira kuwa UCHI,....
.... kwa kuwa KWA KUFIKIRIA HATA UGUMU WA MAISHA wanayapanua miguuu hata yenye chupi kwenye ENGO ya kati yenye goli,....
.... mpaka unaweza kuzani ni kweli HAYO ;....
....DUKA LA MZUNGU LIWAZI , lauza MCHELE NA NAZI , kaniona mimi HALAFU eti anafunga!.:-(
NIMEACHA na wazolilikuwa linaendelea na liendeleze MKUU!
- AU?:-(
Hebu Sankomota adinye mdinyo- Papa
Au tu Jabu Khanyile aendeleze mtekenyo - Mbombela
Basi bwana hebu JUDY MOWATT amalizie na -BLACK WOMAN
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Jifanye MJINGA mapenzi yako yadumu na limpenzi lako KIBOGOYO!:-(
>> Thursday, October 28, 2010
Siri ya MAFANIKIO ya mengi ni TIMING a.k.a KUJULIA MUDA wa kuongelea au hata kufanya jambo,....
....kitu kifanyacho kuwa moja ya siri ya kutogombana na WAKO MPENZI kibogoyo,....
.....ni kuhakikisha kuna muda unajifanya MJINGA wakati mpenzi YUKO katika MUDI ya kujifanya kila kitu ANAJUA.:-(
Kumbuka kwa kujifanya mjinga,....
.....wewe bado sio MJINGA.:-(
Swali:
- SI unakumbuka mara nyingi siri ya kugombana kwa watu wawili ni kwamba wote wawili hakuna anayejishusha katika lumbano lipandishalo jazba ambalo laweza kuzalisha fulu kupigana ngeu?
Ndio,....
....mara nyingine hakuna sababu ya kubishana NA MPENZI kama unajua jibu lako ndilo sahihi,....
....kwa sababu KATIKA MAPENZI kama unamjua vizuri MPENZI,....
....basi wajua kuna wakati JAMBO asilokusikiliza hata UKIBISHANA atakuwa katulia anakusikiliza kama tu UJUAVYO ni wakati gani mzuri kumchuna buzi MPENZI wakati kakaa mkao wa kukubali kila kitu na weye unataka kwenda SHOPINGI.:-(
Swali:
- AU?
- Si unajua kuna muda BWANA LAKO BAHIRI ni rahisi kukupa pesa kama unalijulia MATAIMINGI?
- Na siunajua KATIKA TAIMINGI muda mzuri wa kumshushua MKE wako sio mbele za watu ?
Ndio,....
..... kama unataka kukwepa migongano isiyo na maana MAISHANI,....
..... kama unajijua sio MJINGA ,........ki-TAIMINGI si vibaya kujifanya MJINGA na mwenzio naye aonyeshe maringo yake dingilidingili mpaka chini kuwa naye ANAJUA.:-(
Swali zaidi:
- Kwani kila siku ni lazima MJUAJI awe wewe tu jamaniiiii?Loh Lione Vile!
Habari ndio HIYO na NI WAZO TU HILI LA LEO MKUU!
Hebu Tshala Mwana aingilie kati kipengele
Au tu Caiphus Semenya arudie tena jiwe-Angelina
Na Chicco aingilie ghafla na -We Miss You Manelo
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Jana ndani ya mji wa Tampere na Bloga MALKIORY MATIYA na Deo Mponda!
Katika kuhangaika naye,...
....jana nilijikuta katika mji uitwao TAMPERE ambao Bloga MALKIORY MATIYA na DEO MPONDA ndiko wahangaikako naye mpaka kieleweke......Ingawa muda ulikuwa na kibano chake kwa kuwa mie ilibidi nidandie USAFIRI na kuanza kivyangu tena ,....
.... kwa mara ya kwanza nilikutana uso kwa uso na BLOGA huyu ambaye ukimtembelea kwenye blogu yake ya ; MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI/Forward ever BACKWARD NEVER,...
.... utajua yuko makini.
STORI kibao na kama kawaida kujifunza kitu kulikuwepo.
Baadhi ya Picha zilizotunguliwa katika tukio.....
Bloga Malkiory Matiya |
Nguli DEO MPONDA |
Ilikuwa ni furaha sana tu kukutana na ndugu hawa na NI HILO TU MKUU!
Au hebu Letta Mbulu arudie - Mahlalela
Letta Mbulu aingizie-Carry on
Au tu tena Dorothy Masuka aingilie shughuli na kumwaga -Teya TEYA
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Nachosema na UNACHOSIKIA vinaweza visiwe na uhusiano!:-(
>> Tuesday, October 26, 2010
Labda sio unachosema ndio chenye umuhimu,.....
.... kwa kuwa ni kile wanaokusikiliza wanachosikia ndicho KASHESHE!:-(
Na kwa bahati mbaya si kila asemaye cha muhimu,....
...... husikilizwa na akisemacho kutiliwa maanani moja kwa moja na ndio maana hicho hicho CHA MAANA kitu akikiongea Mama NTILIE adharauliwaye chaweza kutopewa umuhimu ingawa akikiongea hivyohivyo MANDELA kuna watu watasikiliza na kukipa umuhimu kama ubwabwa wa msibani kwa aliyezamia msibani bila KASHESHE.:-(Swali:
- SI bado kunauwezekano nilichoandika na ulichotafsiri baada ya kunisoma labda havina uhusiano?
Naendelea kuwaza....:-(
Lakini unaweza tu kujiliwaza kwa kushuhudia ulimwenguni katika SHOO BIZ ustaarabu wa watu umefikia wapi kwa kudeku hii promosheni ya Puppetry of the PENIS
Au tu cheki na Puppetry of the vagina
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Kwa wale washabiki wa Paul the Octopus!
Jamaa kaanza hivyo leo ,....
POLENI!:-(
Naamini huyu Paul the psychic Octupus (hatched January 2008 - 26 October 2010) ni moja ya ushahidi mambo ya kishirikina au imani za ajabu ajabu ni hai dunia nzima ukizingatia kuna watu kibao walikuwa wanamchukulia VERE SIRIASI na tabiri zake katika World CUP!
Ni HILO TU!! Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
R.I .P Gregory Isaacs!
Gregory (15 July 1951 – 25 October 2010) ni miongoni mwa wanamziki wa Reggae niwapendao sana.
Asante kwa miziki lukuki Mkuu!
R..I..P!
Hebu arudie-Tune in
Aingizie- Number one
Au aachie tu pia -Sad Mood tonight
Read more...
Lebo:
R.I.P
Wakati MSAADA TUTANI unaanza kutishia kugeuza TUTA kuwa ni kituo rasmi cha BASI.
Adoado HUZOELEKA.
Na kwa dogo kama KUSHIKWA KIBINDO labda ndio mwanzo wa kupigwa MUELEKA.
Na wakati kuombwa dogo INAELEWEKA,...
... labda OMBI hata kwa MUNGU liwe ni wakati ombi katika hitaji kikweli LAHITAJIKA.
Kwani azoeaye tegemezi la MSAADA hata wa DALADALA lisimame TUTANI linaloeleweka,....
..... labda afanyacho katika OMBI ni tabia tu kutokana na mazoea kwakuwa kutojitegemea nako HUZOELEKA.:-(
Swali:
- Unafikiri wengi hata MAKANISANI wamuombacho MUNGU sio ni kwa kuwa kumuomba MUNGU ni jambo LILILOZOELEKA tu?
NI WAZO TU HILI BINGWA na wala usikonde!:-(
Hebu tumsikilize tena Robert Mugabe
Au ngojea tujikumbushe tena baadhi ya mitazamo ya nguli Muammar Gaddafi
Au tu tena Simple Minds warudie tu tena - Mandela Day
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Katika kufikiria nje ya BOKSI unoko wa RAIS NYERERE ,....
>> Monday, October 25, 2010
.....................
Swali:
- Hudhani kunauwezekano KUBANIA ULAJI kwa RAIS NYERERE ndio moja ya sababu zilizozidisha WATOTO WA MJINI waliochukua SEHEMU ZENYE ULAJI kupandwa mdadi zaidi wa UFISADI?
Naendelea KUTAFAKARI SWALA.....:-(
Hebu FALLY IPUPA adinye-MABELE
Fally Ipupa aendelee tena na -Bakandja
J Martins ft. P Square na Timaya wa dondoshe nyundo - Good Or Bad (Owey)
Au tu Ngojea J Martins na FALLY IPUPA waanzishe...
Au tu ngojea waache nyolinyoli na kuuatu jabali -Jupa
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Uzuri wa KUMA na MBOO,....
.... labda unaongezeka bila SABABU kwa kuwa HADHARANI WAHESHIMIWA kama wewe ambao katika jamii MNAHESHIMIKA kuliko mimi,....
....kisa mnataka kuamini kuwa HESHIMA na NENO vinauhusiano kama muaminivyo zaidi kuwa MTU ASIPOTAMKA NENO kama mkundu kirahisi kama atamkavyo EMBE BOLIBO basi yeye ndio wakuheshimiwa zaidi INGAWA INAJULIKANA KWENYE AFIKIRIAYO yaitwayo MATUSI YAPO na INAJULIKANA PIA kwa kuwa YEYE ni fisadi na UFISADI WAKE ndio usababishao watoto wa masikini hata wakienda shule watabakia wajinga kwa kuwa hata walimu wenyewe wazuri hupenda kufundisha watoto wa matajiri ujinga ni nini,...
.... labda yeye ndio mwenye matusi ingawa PADRE wa kiroma na WEWE labda hamoni hilo.:-(
Swali:
- SI unajua neno mboo kama tu kisimi kwa lugha ya KIINGEREZA ipendelewayo na wasomi wa BONGO havina maana?:-(
Ni wazo tu HILI Mheshimiwa na samahani kama katika ustaarabu wako moja ya tafsiri ya nilichoandika ni MATUSI na ni RUKSA KUTONIELEWA MHESHIMIWA!!:-(
Hebu CHIWONISO arudishe TENA ustaarabu hapa kijiweni kwa jiwe-Wandirasa
Louis Armstrong aingilie kati ustaarabu kwa -Hello Dolly
Louis Armstrong aendelee kustaarabisha kwa - La vie en rose
Lois Armstrong adinye tu kistaarabu pia-What a wonderful world
Au tu hebu katika kubadili mguno Heavy D arudie nyundo-Truthfull
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
SI kila mtu ATAKUBALIANA na wewe hata katika JAMBO ZURI ufanyalo lenye MAANA kijinga!:-(
PAMOJA NA YOTE,...
.... labda ni vizuri kukumbuka,....
..... KILA MTU anashabiki wake hata kwa ambayo kwa MTAZAMO WAKO afanyayo mtu na SURA YAKE MTU ni kama usilolipenda PARACHICHI ingawa hata bila kumchunguza kikojoleo unajua kwa vyovyote hata kisivyo kibusara bado kama wewe huyo sio PARACHICHI aka MAKATAPELA ,....
.... na haki ya nani hata pamoja na umalaika umsukumiao ukimnusa maeneo kabla hajajiswafi wajua KIUHAKIKA pamoja na harufu kama shombo za samaki huyo ni MTU.:-(
Swali:
- SI unakumbuka hata HITLER alikuwa na girlfriend?
Ndio,...
.....PARACHICHI kama tu makande sio tamu kwa kila MTU.:-(
NIMEACHA na ruksa KUTOELEWA Mkuu!:-(
Ndio huyu ni mimi Simon Kitururu wakati bado kijana na nachana nywele.:-(
Hebu jamaa alie tena...
Au tu hebu JIMI HENDRIX asawazishe tena kwa -All along the watch tower
Au tu James Brown na Lenny Kravitz walainishe tena kwa -Papas got a brand new bag
SIjui kwanini lakini hebu Jimi HENDIX arudie kitu live
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Kuhusu MOROGORO Sekondari!:-(
Kuna kipindi tuliosoma hapoMOROSEKI ilikuwa ni wale WALIOPASI MITIHANI ya darasa la saba vizuri na ilikuwa unaweza hata kumringia mtu kama udhaifu wako ni huo kwa kuwa ukionekana tu MOROGORO MJINI na yunifomu ya MOROSEKI wanajua weye kichwa.:-(
Nachosikitika si kwa kuwa wenye akili MOROGORO ni MOROSEKI ni shule ya mwisho kujaribu kuipa shavu ni MOROGORO SEKONDARI siku hizi,....
.... ila pia tuNI SWALA ZIMA NCHI NZIMA ilivyofikia kuwa siku hizi karibu NCHI NZIMA YA TANZANIA shule za serekali ndizo zinazokwepwa,...
....kisa ndizo ambazo unaweza kwenda kuondoa ujinga na kubakia MJINGA,:-(
Swali:
- SI unajua kwa aliyewahi kusoma MOROSEKI siku hizi ukisikia yanayoendelea hapo kama una aibu ni AIBU TU?
- SI unajua si wanafunzi tu wakwepao shule za SERIKALI kwakuwa hata walimu nao wamestukia kukwepa shule za serikali inalipa pia?
Hebu akina Jeff Msangi wa BONGO CELEBRITY na wengine ambao mpo katika ulimwengu wa kublogi ambao mnawezwa kuguswa na SWALA LA MOROGORO SEKONDARI nisaidieni mtazamo kama mtasoma hiii ndude kwa kuwa nahisi Moroseki inawahusu pia.:-(
SAMAHANI kama huhusiki na hii taralila MKUU!
Moja kwa moja hebu AMERIE aanzishe kwa-Gotta Work
Au labda LL Cool J na Boyz II Men katika kubadili tena zaidi kwa kulainisha zaidi warudie-Hey Lover
Au labda LL COOJ na Amerie katika kuondoa ulaini kidogo tena wadinye-Paradise
Au tu Amerie peke yake arudie mdinyo nyundo - 1 THING
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
JHIKOMAN!
>> Sunday, October 24, 2010
Huyu jamaa ni rafiki yangu tokea zamani.
Na ndio,...
.... alinitangulia darasa moja Morogoro Sekondari.
Barikiwa na baadhi ya kazi zake....
Mapenzi
Kuagana
Au tuendelee kutatua swala la Jhikoman ni nani...
Baadhi ya picha wakati nimemtembelea BAGAMOYO kwake...
Baadhi ya picha tulipokutana mitaaani kusipokuwa Tanzania....
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
WAKATI natafakari kwanini inaweza kuonekana FIDEL CASTRO kawashinda WAMAREKANI lakini ushindi HUO sio wa CUBA!
[Tahadhari: Naongea kimaandishi nikiwa naifikiria pia TANZANIA na kutafakari ya Robert Mugabe]
Moja ya UDHAIFU wa NCHI ZA MAGHARIBI ,...
.... ni siasa zake za uangalifu katika kutaka kuuza danganya toto zionekane ni TAKATIFU zenye watu wazuri wenye kupenda amani na hazina agenda mbaya kwa nchi nyingine.:-(
Na ukifikiria utastukia pia ,....
.... kama MAREKANI isingekuwa inajali DUNIA itaionaje nchi hiyo,...
....FIDEL CASTRO asingeshinda vita na WALA nchi kama AFGHANISTAN , PAKISTAN au hata LIBYA chini ya Muammar Abu Minyar al-Qaddhāfī zisingezingua kihivyo kwa kuwa kirahisi tu kwa nguvu za mabomu zingefutiliwa mbali ,.......hasa kama MAREKANI ingekuwa inafuata mfumo wa KI -Al-Qaida wa kama kuna wakumlipua ukilipua na wasiohusika MUNGU hana noma na hiyo ishu.
Na watu kama FIDEL CASTRO ni miongoni mwa watu wajuao sana MAADUI ZAO ,...
... na baada ya kujua udhaifu wa MAADUI zao ,...
.... hupatia kucheza na UDHAIFU wao.
Swali:
- Hufikirii kuwa moja ya udhaifu au kiwapunguziacho nguvu VIONGOZI wa magharibi ni DEMOKRASIA?
- Kwani hujui KIONGOZI mwenye nguvu kabisa ambaye yuko juu ya mahakama zote za DUNIA sasa hivi ni Rais wa CHINA kutokana na kutokuwepo demokrasia na kutokuwepo awezaye kupamburua AMRI yake ambayo hakuna mahakama ya CHINA iwezayo kupingana nayo?
Ndio,...
.... pamoja na washabiki wa FIDEL CASTRO kustukia huyu MZEE kashinda na atakufa kama El Comandante,....
.... hivi tunauhakika ushindi wa FIDEL ni wa CUBA ambayo wananchi wake kibano wanakiona?Unafikiri ushindi wa Robert Mugabe ni ushindi wa Zimbabwe?
Tukirudi Tanzania ,...
.... unafikiria nini ukitafakari ushindi wa Marais wote waliowahikuchaguliwa TANZANI A, unafikiri ushindi wao ulikuwa ni ushindi wa TANZANIA,....
...hasa kwa kuwa kuanzia Rais Nyerere pamoja na kujua moyo wake ulikuwa mahali sahihi bado unaweza kupata watakaodai alikuwa na udhaifu katika kujua udhaifu wa anaokabiliana nao ndani na nje ya nchi ya Tanzania?:-(
Naendelea kuwaza......
Tubadili mkao kwa kuwasikiliza Jagged Edge wakibinya jipu kwa-Walked OUTTA Heaven
Craig Mack aingilie kati na kurudia-Flava In Ya Ear
Au tu nitafakari Fela Kuti angekuwa hai leo angekuwa anafikiria nini akiusikiliza wimbo wake na ROY AYERS uitwao-2000 Blacks Got To Be Free
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Siri ya MAFANIKIO ya WENGI katika KUJENGA GHOROFA, kupata KURA au tu hata KUPATA DEMU ni kucheza na UDHAIFU wa watu WENGINE!
Na siri KUBWA ya WACHUNGAJI, mapadre, maaskofu ,MASHEKHE au tu hata wainjilisti,....
.... ni KUJULIA tu jinsi ya kucheza na UDHAIFU wa WAUMINI wenye misingi kwenye HOFU ZAO WAUMINI za kuogopa JEHANAMU au tu ule udhaifu mkubwa zaidi wa WAUMINI kutopata maana ya maisha yao BILA msaada wa yaendanayo na HALELUYAH au ASALAM ALEIKUM,........ambayo hudindishwa na KIDINI na hao wajanja ndani ya SWALA ZIMA ambalo ni bonge la kiosha ubongo ni DIMNI.:-(
Swali:
- SI unajua kuna watu kuabudu NG'OMBE au tu KUKU anayetetea ndicho kifanyacho maisha yao yawe na MAANA HAPA DUNIANI hasa kama WAINJILISTI wa hizo dini wanajua kuwapukuchulia waumini wahizo dini kama tu WEWE KWENYE DINI YAKO uoanisho KIMAANA wa hizo DINI na maana ya MAISHA YA MUUMINI wa dini hizo?
Ndio,...
...labda siri ya mafanikio yako ,....
.... ni udhaifu wa MTU mwingine ambao umefanya leo wewe UMEFANIKIWA.:-(
NI WAZO TU HILI MKUU na RUKSA kutolielewa!:-(
Hebu A.K.A KOXX arudie-Girlfriend
Au tu A.K.A KOXX arudie pia-More Than Gold
Nimekumbuka tu filingi zilizokuwepo kwenye siku hii.....
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Nachojaribu kuongea HAPA katika BLOGU hii,....
>> Friday, October 22, 2010
....nikiitacho UjingaBUSARA,....
....kinaweza kuwa ni KWELI ni UJINGA kwa WATU fulani ,....
..... hasa wafikiriao katika UJINGA hakuna CHAKUJIFUNZA.:-(
TUNAKUMBUSHANA tu MKUU kabla sijakutakia BOMBA la IJUMAA na WIKIENDI NJEMA.

Haya basi WAKUU,...
..Ijumaa njema na BOMBA la WIKIENDI Waheshimiwa!
TUKO PAMOJA WAKUU!
Mie naanza hivyo kivyangu lakini siwezi kukuacha bila kukuachia DWELE anong'oneze kitu ambacho unaweza kumshutumu kama unaingilia mambo kwa papara bila kusikiliza na kuelewa katika -I am cheatin'
Dwele amwage tena na nyundo-Weekend LOVE
Halafu hebu tu na MUSIQ abandike tu pia nyundo-HALFCRAZY
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Kama tukichunguza Waheshimiwa WAHAYA walikuwa wanafikiria NINI kilicholeta uvumbuzi muhimu wa KATELERO,...
.... waweza STUKIA staili hiyo ya FIKIRA inachakuigwa.
Kama tu ukichunguza ni kwanini kila MKOA Tanzania kuna WACHAGA na biashara zao kama KENYA ilivyo kuwa na WAKIKUYU na biashara zao na kulipaumakini swala la JINSI wahahavyo ILI tu kuhakikisha WANAJIAJIRI hata kama ni wasomile na KAZI ZA KUAJIRIWA WANGEPATA na kushuka UNG'ENG'E wanashuka kama tu WAZENJI washukavyo KIUNGUJA nyororo kuliko wa wa DAR mabishororo,.....
...... katika nchi kama TANZANNIA ambayo serikali kamwe haitaweza kutoa ajira kwa wote LABDA basi kwao kuna la KUIGWA.:-(
- SI unajua nchi kama MAREKANI ajira kubwa hutolewa na wafanyabiashara ambao hulka zao ni kama WACHAGA Tanzania na sera nyingi za nchi hiyo ni za kujaribu kukuza uwepo wa watu wenye silika kama za KICHAGA?
Na haki ya nani UKILICHUNGUZA KABILA lako utagundua kuna ya KUIGWA MENGI TU ingawa KWA BAHATI MBAYA na ya kuyatolea nje kinamna kama yale ya kutahiri KIDUDE mabinti yapigiwayo kelele yaachwe kwa sababu zihusishwanishwazo na utamu, AFYA au tu kwa kuwa shughuli nzimaYA KULIPIGIA KELELE SWALA inalipa watu mishahara Ki- N.G.O iliyostukia ulaji,.....
.. bila kusahau yale ya KAMA ya BAADHI ya WALUGURU ya KAZOPATA ya kuona ni afadhali WAHINDI au hata WAPARE wapate kuliko apate MLUGURU mwenzao,...
.....YAPO.:-(
Swali:
- AU?
Ndio,....
.....Ukichunguza ubunifu wa WAHAYA katika kitu chenye uhusiano na pekechapekecha kama KATELERO ,...
.... halafu ukawaza NJE YA BOKSI na kustukia karibu kila kitu ukifanyacho labda kina katelero yake,....
.... au badala ya kuwa mzibua vyoo wa kawaida waweza kujikuta unamiliki KAMPUNI ya kuzibua vyoo AFRIKA MASHARIKI,....
Swali nje kidogo ya tundu:
- SI unakumbuka uwezekano wa MAREKANI aka USA kuwa nchi inayoendelea na SIO ILIYOENDELEA hapo baadaye kama unakumbuka MONGOLIA enzi za Ginghis Khan, MISRI yakina Farao , hadi URENO zilishawahi kuwa ndio nchi tajiri na zilizoendelea kuliko zote kama isifikavyo MAREKANI sasa?
- SI unajua ukifikiria NJE YA BOKSI suluhisho la jirani la jinsi ya kuboresha VITUMBUA inaweza kukufanya WEWE ugundue jinsi ya kuboresha KEKI kwa hiyo labda kwa kudadisi katelero unaweza kupata mwanga katika ugunduzi wa manukato ya kunako?
- Si unajua karibu kila kifaa utumiacho chanzo chake kilikuwa ni TATIZO na kwa hiyo kama unatatizo labda unamwanya wa kuwa wewe ndio MTATUZI?
Kabla hatujaachana na KATELERO:
- Je MHESHIMIWA umeshawahi kuifanyia utafiti hii kitu?
Basi BWANA kama hujawahi kuifanyia UTAFITI HII KITU na hujui maliwazo yake katika umadhubuti wa maliwazo kwa ushirikiano wake na PEMBEJEO ZA KAZI NANIHINO usitishike KAMA TARALILA HII HUIELEWI inalenga nini katika KUAMSHA hisia na TAFAKARI wala zisizo na uhusiano na KATELERO ambayo mamasta wake ni WAHAYA by reputation Mheshimiwa.:-(

NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!:-(
Update:
- Baada ya kusoma comment ya Papaa Mubelwa ambaye ni MUHAYA naamini neno KATELERO katika taralila yangu HII lisomeke: KATERERO .:-(
Moja kwa moja Majek FASHEK aingilie tena kati na kurudisha ustaarabu hapa kijiweni kwa kuongelea -AFRICA UNITY
Majek Fashek aendelee na -So LONG
Au tu Baaba Maal amalizie tu kwa kurudia -Yela
Read more...
Lebo:
UjingaBUSARA
Subscribe to:
Posts (Atom)