Tahadhari :SOMO linagusa swala kwa JUUJUU !:-(
Habari zenu WADADA!
Aah jamani nawasabahi JAMANI mbona mmenuna namna hiyo?
Naomba TABASAMU kidogo basi!
AKSANTEEEE Dada zangu,....
... na moja kwa moja ngojea tuongelee mapumbu.!:-(
Ndio,...
...najua kati yenu kuna watundu ambao TAYARI mshawahi kuona hii kitu wakati toto la KIUME linaogeshwa au hata kupapasa hiki KIFAA ,...
....tukiachilia mbali na hata kujua kuwa HII NDUDE ikigongwa inauma kweli kwa hiyo tayari ni wastaarabu na hamjaribu kubinya au hata wakati wa ugomvi kupiga teke hiki kifaa MAKENDE kwa kuhurumia mchango wake kwa vizazi vijavyo.
Na nashukuru kwa hilo yani!
Ila bado ,...
...wanawake WENGI ni miongoni mwa watu wengi wasiostukia kwanini WANAUME wanajihadhari kubinywa KORODANI ,...
...na pia wasiostukia hiki kifaa hakiko kwa ajili ya UZALISHAJI TU wa malighafi shahawa aka MBEGU za KIUME ambazo ni maarufu sana kwa kuchafua mashuka kama tu kusababisha mimba zikilengwa kwenye tundu lenye yai lihitajilo rutuba.:-(
Hiki kifaa kina kazi zaidi ya UZAZI aisee,...
..... kwa kuwa ni chombo kitengenezacho pia HORMONES aka HOMONI ambazo hutumika kurekebisha mwili wa BINADAMU kutokana pia na kuwa na mfumo ujulikanao kama
endocrine system au System of Glands ambazo hutengeneza hizi Hormones na kuzimwaga kwenye damu ya mtu ambazo hurekebisha kuanzia UKUAJI wa MTU, anavyojisikia mtu (MOODS) , mpaka jinsi ni kwa spidi gani unasikia njaa kutokana na hizi HORMONES kucheza na ndude
METABOLISM ya mwili,...
....ingawa NDIO ,...
...kifaa HIKI hujulikana zaidi labda kwa mchango wake wa sperms au kwa lugha ya kitaalamu SHAHAWA na kwa homoni moja zaidi ya aina ya TESTOSTERONE ambayo inafanya DUME akae kidume ,...
.... yani fulu MIDEVU na minywelenywele bwelele mwilini isababishayo hata gizani kama mjanja ukipapasa ustukie ulipapasalo ni dume RIJALI , misuli mikubwa na mpaka bonge za mifupa kiujazo pia,..
....kitu isababishayo BODE la njemba liwe tofauti kidogo na BODE la kimwana mrembo mwenye kiuno kama nyigu,...
...ikiwa na maana inasaidia DUME lisikae KIJIKE - ki fulu bonge za titi.
Na ukitaka kuijua zaidi hii ndude ninliyopapasa mpaka hapa ,...
....Testicle,....
.....Testosterone ,....
.......kitu kizima ENDOCRINE SYSTEM,.....
.......hormones ,....
.....au hata kitu Sperm aka Shahawa ,...
.....gugo aka GOOGLE tu hizo MSAMIATIZ,...
....ambazo ndizo nimechezanazo katika somo mpaka hapa MKUU kwa shule zaidi isiyo ya juujuu kama ya vidokezo tu niistuayo hapa KIADOADO.:-(
Lakini kwa kifupi ,....
... nafikiri tutakubaliana kuwa MAPUMBU ni muhimu aisee mdada!:-(
Hebu tupate kwanza kielelezo cha hiki kifaa :
Hiki kifaa hutunzwa katika kifuko kilichoumbwa kwa mchanganyiko wa ngozi na misuli ``SCROTUM´´ ambacho kazi yake kubwa ijulikanayo ni kuweka KORODANI kijoto chini ya joto la mwili kwa kuwa KENDEZ zikiwa na joto kama la mwili mbegu za kiume zitengenezwazo huingia udhaifu na kufanya kidume sio kila goli lake lina afya na nguvu kwa kutokana na joto kuathiri kitu kiitwacho na wabongao ung'eng'e -
Sperm Count.
Na kutokana na hilo mpaka kuna wadaio bila USHAHIDI WA KITAALAMU kuwa labda MIDUME ijihadhari na chupi aka VIFICHA NYETI vibadavyo sana na kuzuia kazi ya kifuko ya kusogeza makende mbali na mwili joto likizidi na kuyarudisha karibu na mwili kama kipupwe kimezidi kushusha joto za pumbuz .
Hebu tukideku kipicha kifaa:
Hapa ni kitu kikivutwa juu ikiwa kinabaridi iathiriyo joto litakiwalo katika kiwanda cha shahawa na na kikishushwa chini kidogo kimnig'inio ikiwa joto la mwili ni kubwa zaidi kidogo kuliko lihitajiwalo kiwandani.
- Na nadhani unakiona wakati kimesogeza BALLS karibu na mwili hapo kulia .
- Na kikiachanisha KORODANI na mwili huteremka kama ionekanavyo hapo kushoto.
Kazi hii ya kupandisha na kushusha GOLOLI hufanywa zaidi na Misuli ya cremester aka
Cremaster muscle ambayo huvuta pia makende juu kama MHESHIMIWA KIDUME ananyege na kitu kimesimama ,...
... kazi ifanywayo PIA ili kulinda shehena za aina ya KORODANI zisiathiriwe KATIKA KURUPUSHANI hasa wakati mheshimiwa anakula ngoma aka ANANGONOKA.
Mpaka hapa nimepapasa,...
....Cremaster muscle,...
.....Scrotum,....
....na Sperm Count ,...
,....ambazo kwa shule zaidi wewe ZIGUGO tu ukizingati katika taralila hii nazigusia kwa juujuu.:-(
Na kifuko aka KITUNZA MAKENDE HIKI kinasemekana kuwa na undugu sana na
Labia Majora kwa wanawake.
Asanteni WADADA,....
... na nimatumaini kuna angalau jambo MOJA ili taralila hii ifanikiwe labda mtalifanya na hilo ni angalau kujiuliza kitu kimoja ambacho kitazalisha angalau MGUGO aka M-Google kitu kimoja zaidi KUTOKANA na TARALILA HIII na kujua angalau kitu kimoja zaidi kuhusu hizi KENDEZI ambazo historia yake kwa UZALISHAJI na hata yakufanya MIDUME iote NDEVU na kuwa na TITI ndogo ukilinganisha na NYONYO za WANAWAKE ,...
.... ni tokea enzi za ADAMU na HAWA.
SASA TARALILA inaegemea kwa WANAUME zaidi ,...
..... na hii,...
.... ni KITU siriasi zaidi hasa kwa kuwa inagusa zaidi SARATANI ya Ze PUMBUZ!:-(
Hebu tuanze upya na twende shule kuhusu MAPUMBU,...
...kwa msaada wa MWANADADA,...
.....
Dr. Susan Jewell kwa .....
Mdada
SUSAN aendelee..
Somo zaidi kwa wanaume kuhusu kucheki hiki kifaa hasa kutokana na saratani ya kiaina ichezayo maeneo kwa kumdeku huyu MDADA akizidi kufunza katika hii
-Testicle exam
Kabla sijaacha labda tucheki SHULE MCHANGANYIKO ,...
...hasa kwa wazazi ambao wamepata mtoto wa KIUME ambao labda inabidi wajue tu pia kuna kitu kiitwacho-
Undescended Testicle kwa kumsikiliza
Dr Steven Friedman
Mpaka hapa kwa shule zaidi unaweza KUGUGO,....
....Undescended testicle,....
...Testicular cancer,..
... ambavyo nimevigusa kwa juujuu .:-(
NIMEACHA!
Samahani tunakumbushana tu SWALA na madhumuni ilikuwa nikuchokoza udadisi wako ili udadisi zaidi kujua zaidi kuhusu hii kitu MHESHIMIWA,...
.....na kama umekwazika au hukujifunza kitu KATIKA PROSESI ya KUDAKA USHUSHAJI wangu wa HII ishu KI-UjingaBUSARA maana yake mlengwa wa TARALILA HII haikuwa wewe,...
... na kwa hilo SAMAHANI!!:-(!
Read more...