Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tusisahau!

>> Monday, October 31, 2011

African albinos killed for body organs




 Hii kitu haijaisha WAJAMENI,....
...TUSISAHAU!

Read more...

Ya DUNIA :Corrective Rape/ KAMA BINTI ni MSAGAJI abakwe kama TIBA

Cheki mwenyewe stori






Read more...

WAKATI UNAJIZUIA kufanya KIBAYA au kuharibu kwa kufanya KIWEZEKANACHO,...

... yawezekana WAKATI HUOHUO kwa kujizuia kutoharibu  na kwa hiyo HUFANYI,....
... kunauwezekano MKUBWA TU kuwa ufanyacho ni kuzuia pia KIZURI ambacho UKIFANYA KITU  ni kiwezekanacho.

Swali:
  • Si  kwa kuepuka KUFANYA VIBAYA  wengi hawafanyi chochote KABISA?

Ndio,...
.... kwa KUOGOPA KUKOSEA leo ,...
.... labda ambayo yasingekosewa MAZURI TU  nayo kwa bahati mbaya HAYAFANYWI!:-(

Ni wazo tu hili NGULI!
JUMATATU NJEMA!


Hebu Kenny Rogers aimbe wimbo wa Lionel Richie ule- Lady




Diana Ross na Lionel Richie warudie-Endless Love




Joe Cocker aingilie kati kwa wimbo wa Lionel Richie ule - You Are So Beautiful




Rod Stewart ajaribu kubadili halafu tubaki palepale -Have I told you lately




Eric Clapton arudie - Wonderful Tonight




Ila sijui kwanini hebu Lionel Richie azime kwa-Brick House


Read more...

Wakati NAAMINI TU kwa kuwa ``FULANI ´´ ndiye KASEMA!

Ndio,...
..... kuna yaaminiwayo ,...
.... kutokana tu na JINA lioanishwalo na YALIYOSEMWA!:-(


Swali:
  • Lakini si unakumbuka kama LISEMWALO asili yake ni MTU labda BADO yawezekana ``USIKIALO ´´,``LILILOMAANISHWA ´´, na ``LILILOSEMWA ´´ bado ni vitu VITATU TOFAUTI?

Ndio,...
.... labda KUNA ya KWELI yasiyoaminiwa na MTU,...
..... na kisa tu chakutoaminika UKWELI WAKE ni kwa kuwa ni JINA LANGU au LAKO limeoanishwa na KISEMWACHO.

Ni wazo tu hili MKULU!:-(


Hebu turudi kwenye JAZZ pale Africa KUSINI tena ili Winston "Mankunku" Ngozi adinye-The BIRDS



Au tu hebu tu tena Winston "Mankunku" Ngozi aachie - Yakhal' Inkomo





South African Jazz legend Winston "Mankunku" Ngozi born 1943 and died October -11- 2009 of heart related illness,
R.I.P!

Read more...

JIHADHARI! Unayebishananaye kwa DHARAU na MATUSI MTANDAONI anaweza kuwa ni MZAZI wako!

Stori niliyopewa na MDAU wangu:


Rafiki yangu alinipigia simu jana baada ya MAKUBWA kumkuta.

Basi jana Jumapili alikuwa kaboreka na akaingia mtandaoni kwa simu kuperuzi na kujikuta yuko kwenye mtandao ambao mjadala unaendelea. Kwa spiriti ya kutaka kupoteza muda na pia kucharua mtu akaanza kubishana na ANONYMOUS mmoja mtandaoni  aliyemkera na mpaka matusi akampachika kisa kumchokoza zaidi na pia kwa kuwa alikuwa hapendi misimamo yake.

Baada ya mdahalo kupamba moto na kiu kumpanda akaamua kwenda chumba cha malaji (DINING ROOM)ambako kuna FRIJI ili kupata kimiminika cha aina ya juisi na kumpita BABA YAKE akiwa kakaa SEBULENI naye kazama kwenye simu yake.

Hapo ndio machale yakaanza kumcheza kwa kuwa akawa anastukia kila akituma meseji simu ya Baba yake aliyezama kimawazo kwenye simu na ambaye hakuwa mbali naye inabipu. Na kumbe vilevile BABA MTU kumbe naye machale yakaanza kumcheza kwa kuwa alianza kustukia pateni ya kubipu kwa simu ya BINTI(Mdau wangu) na atumavyo meseji hasa kwa kuwa malumbano  katika tovuti waliyokuwa walibaki watu wawili  wakiendeleza malumbano.

Haikuchukua muda kwa swala kuwa wazi kuwa BINTI ambaye ni MDAU wangu kustukia amtukanaye ni BABA YAKE ambaye anaamini mpaka jana alikuwa anaamini kuwa kalea BINTI na kaleleka kabisaaa kwa tabia nzuri  na kakaa wala sio mbali naye wakati anamtusi .

Na nahisi kilichoendelea unaweza kuhisi hasa baada ya BABA MTU kuwa nauhakika aliyekuwa analumbana naye  ni BINTI YAKE na wala si masaa mengi walitoka pamoja KANISANI .

Na MDAU anadai kuwa anahisi asingekuwa mkubwa angekula mkong'oto jana.

Na sasa hivi hata kumuangalia usoni BABA YAKE anaona haya hasa kwa jinsi alivyokuwa anamtukana na hata pia alivyokuwa anatamba kwa uelewa wake wa mahaba na chakula cha usiku kitu ambacho hata siku moja asingependa hata MAMA YAKE  /Mwanamke mwenzake asikie anayoongea kutoka kwake.

NDIO ! 
HAWAONGEI mpaka sasa hivi naenda MTAMBONI!

------------------_____________________-----------------------------

Kwa hiyo MDAU,..
...jihadari ukiwa MTANDAONI na unayetongozana naye au hata KUMTUKANA anaweza kuwa ni NDUGU yako na hapo ni kama siyo MZAZI WAKO na wakati huo mto chini ya PAA MOJA wakati mnaendeleza mambo zenu hayo hasa kama mchezo ni kujiita ANONYMOUS au tu MAJINA ya UONGO kama ilivyokuwa kawaida ya wengi.

Swali:
  • Si ushastukia  kuna watu  WATOTO unawezafikiria ni WATU wazima MTANDAONI na WATU  WAZIMA ambao tuna mambo ya kitoto MTANDAONI?
  • Na si nasikia  MTOTO na MKUBWA wote wakikosea  bado kiutamaduni wa TANZANIA ni mtoto mwenye makosa kwa kuwa eti ni WATU WAZIMA tu waheshimiwao kihalali na ndio mpaka wawezao toa LAANA ukiwakosea?
  • Na si ushastukia  kuna MIDUME inajiita majina ya kike MTANDAONI na MIDADA ijifanyayo MIDUME?

Ndio,...
... yamtandaoni ya SIRI,...
... yanamchezo wa KUBUMBURUKA  siku nyingine na ANONYMOUS hustukiwa ni NANI kwa hiyo  tahadhari MWANAKWETU  kama unamchezo wa kujiamini  kuwa YAKO ya MTANDAONI  ufanyayo kisiri ,...
... basi hayo MILELE ni SIRI!

Ni hilo tu MHESHIMIWA!



Hebu Josky Kiambukuta aanzishe upya kwa - Baby




Turudi Guadeloupe ili FUCKLY arudie-Doudou



Halafu Biggie Irie aingilie kati nakuzima kwa- Nah Going Home

Read more...

Matukio mbali mbali ya Safari Miss Vodacom Tanzania 2011 SALHA ISRAEL katika kuelekea Fainali za mrembo wa Dunia

Hapa Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa kwanza kushoto akiwa katika Vazi la Ufukweni na Wenzake katika maonesho ya Mavazi hayo hapo jana.


Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Kumi kutoka kulia akiwa na wenzake katika Dina la nguvu Huko Scottish maeneo ya Scottish Hydro.
Miss Vodacom Tanzia 2011 Salha Israel aliye vaa Nguo za Njano katika Mazoezi ya nguvu kabisa wakati wa maandalizi ya shindano la Miss World Tanzania

Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa pili kutoka kulia akiwa Edinburgh Castle hivi karibuni katika safari ya kuelekea katika mashindano ya kumsaka Mrembo wa Dunia.

Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Pili kutoka kulia akiwa anapiga Chiazi na wenzake .. katika safari ya kuelekea kumtafuta Mrembo wa Dunia.
Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa kwanza kushoto aliye simama akiwa katika picha ya pamoja na wenzake





Miss Vodacom Tanzania 2011 Salha Israel wa Tatu kutoka kulia akifurahia kwa Shangwe wakati wa Highland Games kuelekea kinyang'anyiro cha Mrembo wa Dunia







Kwa picha zaidi Tembelea: www.fredynjeje.blogspot.com


Nimetumiwa na :
FREDY NJEJE

Read more...

KIFO cha BATA kwa KUKU,...

>> Sunday, October 30, 2011

.... kinaweza kutopewa UMUHIMU au HATA  tu HUZUNI kwa kilo za kutosha na KUKU,...
.....ingawa KIUACHO BATA  labda  kina mchezo wa KUDEDISHA KUKU PIA  ,...
.... na tena kwa sababu ZILEZILE!:-(

Swali:

  • Si  kuna wasiojali JIRANI  kaibiwa  kisa hawajaibiwa WAO?


Ndio,...
... kifo cha KUKU  kwa kuugua MDONDO,...
.... labda kikudedishwa ndege ,...
... chaua BATA pia!:-(



JUMAPILI njema KAMANDA,...
..... na  kumbuka ni wazo tu hili  BINGWA!

Hebu Andy Narell aanzishe upya  kwa - Down de Road



RAY C akiwa na FRENCH BOY alaininshe siku kwa - Moto moto





RAY C aongezee- Na Wewe Milele








Smokie Robinson abadili mchezo kwa-The Tracks of My Tears





Mariah Carey akatizie denge tena kwa-I Want To Know What Love Is






Halafu FELA KUTI azime tu tena kwa-Gentleman



Read more...

Katika kumbukumbu: MALCOLM X

You Are Afraid To Bleed




Wake up, Clean up and Stand up!




Daka udakacho! 
CHUKUA UCHUKUACHO!
Na ni kumbukumbu tu hii MHESHIMIWA,...
...na usikonde!

Read more...

"Clintonomics." kiduchu

Ukiweza oanisha na AFRIKA asemacho Bill CLINTON kiaina!:-(


NDIO,...
....The Clinton Foundation hosted a conference Friday on the lessons of "Clintonomics."


SWALI la KIZUSHI:
  • Rais MWINYI upooo?

Read more...

ENZI ZILE:- WAPIGA PICHA WAKUU NA VIONGOZI WA VYOMBO VYA HABARI WAKIMUAGA BABA WA TAIFA IKULU MWAKA 1985




BAADHI YA WAPIGA PICHA TOKA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI NCHINI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BABA WA TAIFA MWL. NYERERE WAKATI WA KUMUAGA BAADA YA KUSTAAFU URAIS IKULU JIJINI DAR ES SALAAM 1985.WALIOSIMAMA TOKA KUSHOTO MAX MADEBE(MFANYAKAZI),SAM MMBANDO(SHIHATA),VINCENT URIO, (DAILY NEWS),JOHN MAKWAIA (MAELEZO), MZEE SILEN(AVI), JUMA DIHULE(SHIHATA), ADINAN MIHANJI (SHIHATA)NA KIYUNGI WA KIYUNGI (MAELEZO). WALIOCHUCHUMAA WAPILI TOKA KUSHOTO,CHARLES KAGONJI (MAELEZO),GERVCE MSILLO (DAILY NEWS), MWANAKOMBO JUMAA (MAELEZO), KHATIBU ALLY (UHURU) NA RAPHAEL HOKORORO (MAELEZO).




BAADHI YA VIONGOZI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MWL. NYERERE SIKU YA KUMUAGA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM BAADA YA KUSTAAFU MWAKA 1985.

KUSHOTO NI DAVID WAKATI(RTD),NYUMA YA MWL. NI MZEE SAILEN(AVI), GERVACE MSILO (DAILY NEWS, ADINAN MIHANJI (SHIHATA) NA KIYUNGI WA KIYUNGI (MAELEZO)


Picha zote na HABARI na: www.latestnewstz.blogspot.com


Nimetumiwa na:

Read more...

MATUMLA, MIYAYUSHO WAKIPIMA UZITO JANA KWA AJILI YA MPAMBANO LEO


Bondia Mbwana Matumla akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kugombea ubingwa wa UBO na Fransic Miyayusho leo jumapili.







Mabondia Francis Miyayusho (kushoto) na Mbwana Matumla wakitunishiana misuri jana baada ya kupima katika ukumbi wa Amana Dar es salaam  kwa ajili ya mpambano wao leo.










Na Mwandishi Wetu Ilala
(Jumamosi OKTOBA 29)


Mabondia Mbwana Matumla 'Golden Boy' na Francis Miyayusho 'Chichi Mawe' leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Ubingwa utakaofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam kesho jumapili OKCTOBA 30.

wakizungumza wachezaji hawo kwa wakati tofauti baada ya kupima wamesema wapo tayari kuonesha mchezo mzuri wa ngumi na kuwapa raha zisizo na kifani kwa sababu akuna kisingizio chochote kile kwa kua tumejiandaa vya kutosha

Licha ya mabondia hawo kupima uzito pia wamepima vipimo mbalimbali ususani Ukimwi, Mkojo kwa ajili ya kuangalia kama mabondia hao kama wanatumia madawa ya kuongeza nguvu.

Pambano hilo kubwa litakuwa la 12 la uzito wa Bantam, ambapo kabla ya mpambano kutakua na mapambano mengine ya utangulizi.

Mapambano hayo ya kati ya Juma Fundi na Fadshili Majia, Mohamed Matumla na Ramadhani Mashudu, Issa Sewe atazidunda na Ramadhani Shauli wakati kwa upande wa ngumi za wanawake Asha Nzowa (Asha Ngedere) atazichapa na Salma Kihobwa (mwajuma Ndalandefu)

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinbu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, MOhamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D;



--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Read more...

Ujumbe kutoka kwa Mbunge ZITTO ZUBERI KABWE hospitalini INDIA.

>> Saturday, October 29, 2011





Ndugu zangu,

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha muda huu kuwa na nguvu za kukaa katika kiti na kuweza kuandika haya machache kwenu. Nawashukuru sana Wanamabadiliko kwa salaam zenu nyingi za pole mara mliposikia ninaumwa na kulazwa hospitalini. Najua hamkuwa na taarifa kamili za kuumwa kwangu na kwa kweli suala la kuumwa ni suala la mtu binafsi (hata kwa mtu mwenye dhamana ya kiuongozi wa umma japo umma nao una haki ya kujua kinachomsibu kiongozi husika).

Mwanzo


Nilianza kupatwa na maumivu ya kichwa usiku wa siku ya Ijumaa tarehe 20 jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kutoka Jimboni tayari kwa kazi za Kamati za Bunge ambapo Kamati yangu ilikuwa imekwishaanza kazi wiki hiyo kwa kupitia mahesabu na utendaji wa Mamlaka za Maji nchini. Kama kawaida yangu niliona maumivu hayo makali kama ni sehemu tu ya uchovu wa ziara za Jimboni na safari za mara kwa mara nilizofanya kuinigilia ziara za Jimboni ikiwemo kuhudhuria Mdahalo wa Umeme na Mkutano wa Uwekezaji Kanda ya Ziwa Tanganyika. Hivyo nililala na nilipoamka kichwa kilikuwa kimepona na hivyo nikahudhuria kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma katika Ofisi ya Bunge mpaka saa saba mchana.

Siku ya Jumapili saa kumi na moja jioni nikiwa katika Hoteli ya Southernsun nilipatwa na homa kali ghafla. Nilikatisha mkutano niliokuwa nao na kuamua kurejea nyumbani, lakini nilishindwa kuendesha gari na hivyo kumwomba Dereva wa Mhe. Mhonga anifuate ili anisadie kunifikisha nyumbani. Nilipofika nyumbani kwangu Tabata, homa ilizidi kupanda na hivyo kuamua kwenda Hospitali mara moja. Nikapelekwa Agakhan Hospital na nikapata huduma. Nilipochukuliwa vipimo ilionekana sina malaria wala homa ya matumbo na pia hawakuweza kuona sababu ya homa ile namna ile (maana ilifikia degree 40). Walituliza homa, nikapewa Panadol na baadaye nikaruhusiwa kurudi nyumbani mnamo saa tano usiku. Nilipoamka siku ya Jumatatu nikaenda kazini kuongoza Kikao cha Kamati ya Bunge ambapo tulikuwa tunashughulikia Hesabu za Bodi ya Utalii na Benki ya Posta Tanzania. Nilipita Agakhan kupata majibu ya ziada na kuambiwa nipo sawa ila nipumzike nisifanye kazi kwa siku kadhaa na nitakuwa sawa.

Hali kubadilika

Siku ya Jumanne niliamka nikiwa salama, kichwa kikiuma kwa mbali lakini sio vya kutisha. Nikawajulisha wajumbe wenzangu wa kamati kuwa sitakwenda kazini na wao waendelee na kazi. Hata hivyo ilipofika saa sita kamili nilianza kutetemeka mwili mzima na homa kuwa kali sana huku kicha kikiniuma sana sana sana! Dada zangu wakamwita Driver na kunikimbiza Hospitali ya Agakhan. Wakarejea vipimo vilevile na matokeo yakawa yaleyale. Joto lilifika degree 39.8 Hivyo wakanipa dawa za kupoza homa na maumivu ya kichwa kwa drips na sindano kadhaa. Siku ya pili hospitalini nikafanya vipimo zaidi ikiwemo ultra sound na vyote kuonekana sina tatizo lolote.

Niliendelea kuwepo Hospitali na kwa kweli hali ilikuwa inatia moyo sana kwani nilipata nguvu na hata kuweza kuzungumza, homa ilikuwa imepungua sana. Pamoja na kwamba Mganga Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Waziri wa Masuala ya Bunge na Daktari wangu binafsi kuwataka waangalie upya vipimo vya malaria, madaktari wa Agakhan waliwahakikishia viongozi hawa na Daktari wangu kwamba hawajaona Malaria na hivyo wanaendelea na uchunguzi wa 'a trigger' ya homa kali niliyokuwa napata.

Hali kuwa Mbaya

Usiku wa siku ya Jumatano Hali ilikuwa mbaya sana. Joto lilipanda tena kufikia 40 na kichwa kuuma zaidi. Nilikuwa kama ninatwangwa kwenye kinu kwa kweli. Nilikuwa natetemeka sana. Ilikuwa taharuki kubwa sana katika chumba nilicholazwa. Wageni waliokuwa wamekuja kunijulia hali wakati hali inabadilika ilikuwa ni pamoja na Ndugu Murtaza Mangungu na Mohamad Chombo ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya POAC, walishauri mara moja nihamishwe Hospitali kupelekwa Muhimbili. Muda si mrefu kupita Waziri Lukuvi na Katibu wa Bunge walifika, wakaafiki na nikahamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwa hali niliyokuwa nayo nikalazwa katika Chumba wanachokiita Mini-ICU. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Mama Blandina Nyoni alikuwepo Hospitalini tayari.

Usiku huo huo nilifanyiwa vipimo upya. Full Blood picture pamoja na BS. Vile vile kufuatia malalamiko kuhusu maumivu ya kichwa ikaamuliwa kuwa nifanyiwe CT Scan usiku ule. Ikaonekana nina wadudu wa Malaria 150 na mara moja nikaanza matibabu. Namshukuru sana Daktari kijana Dkt. Juma Mfinanga kwa umahiri mkubwa aliouonyesha tangu nilipofika pale Mini ICU. Asubuhi ya siku ya pili nikapata majibu ya tatizo la maumivu ya kichwa. Nimekuwa nasumbuliwa na kichwa kwa miaka zaidi ya Kumi sasa na katika kipindi hicho mara nne nilipoteza fahamu na kuanguka (Mara ya kwanza mwaka 2000 nikiwa Jijini Mwanza nikielekea kwenye Mkutano wa Vijana wa National Youth Forum, Mara Pili Mjini Dodoma katika mkutano kama huo mwaka 2001 lakini ilikuwa usiku, Mara ya tatu Nikiwa chumbani, Hall II mara baada ya kutoka  Prep, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2002 na mara ya Nne Bungeni siku ya kupitisha Muswada wa Madini 2010 kufuatia wiki nzima ya Kamati na Mjadala wa Bunge (Ndugu Katulanda anakumbuka siku hii kwani yeye ndiye niliyemkamata njiani kunikimbiza Zahanati ya Bunge).
Tatizo lililogundulika ni SINUSITIS, ambayo tayari imekuwa sugu. Daktari Bingwa wa magonjwa haya Dkt. Kimaryo akanieleza kwa kirefu juu ya tatizo hili na kuniambia suluhisho ni 'surgery' na pale Hospitali ya Taifa hawafanyi hiyo operesheni. Akashauri niletwe India ambapo kuna Daktari mpasuaji wa ugonjwa huu. Nikakubali.

Baada ya kuwa Malaria imedhibitiwa kwa kufikia nusu ya 'dozi' nilopewa na wadudu kuonekana kutokomea, Ofisi ya Bunge ikaandaa safari. Nimefika India. Nimebakiza sindano mbili ili kumaliza 'dozi' hiyo na tayari nimefanyiwa taratibu zote kwa ajili ya 'surgery' hiyo.

Sijafa


Uvumi ulienezwa nimekufa. Kwa kupitia kwenu ndugu zangu WanaMabadiliko, napenda Watanzania wenzangu wajue mimi ni mzima wa Afya. Nimepata maradhi kama Binadamu mwingine yeyote anavyoweza kupata na namshukuru Mungu kwamba ninapata matibabu mazuri kabisa.

Shukran


Nawashukuru sana Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Prof, Mwafongo kwa juhudi kubwa walioonyesha katika kunihudumia. Naishukuru Ofisi ya Bunge kwa Kutimiza wajibu wao kwangu kama Mbunge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na watumishi wote wa Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa kwa ufuatiliaji wa karibu wa Afya ya Naibu wake, Wabunge wajumbe wa Kamati ya POAC, Dkt. Alex Kitumo, ndugu, jamaa na marafiki zangu wote. Nawapa pole wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa uvumilivu mkubwa hasa kufuatia uvumi mbalimbali ulioenezwa, pia Watanzania wengine kwa uzito huo huo.

Nitawajulisha kwa lolote Mungu akipenda. Ninaendelea na matibabu na hali yangu ni nzuri

Ndugu yenu

-Zitto

--
Kabwe Z. Zitto,MP- Kigoma North, Tanzania.
Chairman Parliamentary Public Investments Accounts Committee (POAC),
Deputy Secretary General CHADEMA and Deputy Leader of the Opposition,
Shadow Minister of Finance


The gratification of wealth is not found in mere possession or in lavish expenditure, but in its wise application. -Miguel De Cervantes

Na karibuni kujiunga katika mjumuiko wa  wanamabadiliko,...
...uitwao   MABADILIKO

Read more...

UCHESHI: Bill COSBY aliwahifikiria jina lake ni JESUS CHRIST ,Rais mtarajiwa HERMAN CAIN aimajini THERE IS NO PIZZA na RICHARD PRYOR ajua DANGANYA za WATOTO !:-)

Swali:

  • UMENUNA?
Ndio,..
... baada ya KUNUNA kuchekelea kanyau kuna starehe zake aisee!

Ila kwa BAHATI MBAYA kila mtu  anachekeshwa na vitu tofauti,...
....na ndio MAANA wakati mwingine anaangu kuna WACHEKAO.

Hebu RICHARD PRYOR asimulie
-When KIDS lie



Halafu  tudeku ni kwanini ,...

....Bill Cosby -Thought He Was Jesus Christ



Cheka BASI bwanaaaa,..
... si unajua KUCHEKA ni DAWA?

Au tu Rais Mtarajiwa wa MAREKANI  HERMAN CAIN ,...
.......achukue side ya PIZZA katika- Imagine There's No Pizza



Tukiacha utani ,...
... hebu John LENON arudie -IMAGINE


Read more...

Flora Mbasha Blog Now On Air ; The Home Of Gospel Music






Tanzanian Gospel Singer Flora Mbasha wishes  to declare publicly the launching of her Blog as it was promised two weeks ago by her husbabd Mr Emmanuel Mbasha. The Blog is made up of mix of stories, live performance, photos and so on.

“Wherever You Are In The World , feel free to visit even comment on My Blog which in fact it is Gospel Oriented Blog for it intends to impact the so called pro-Gospel  movement in Tanzania and beyond” Flora Mbasha was quoted this morning at her home in Dar es salaam.

Flora Mbasha argued many people to visit her blog, comments, send news as well as photos so as to make everyone part of it(but she warned that all the informations, news and photos should correspond to her Blog motto which is Gospel Music for Serving God&Community).

Flora Mbasha is an International Gospel Singer based in East Africa particular in Tanzania and she has performed in different countries across the world. She has number of Albums since she got into the service more than five years ago.

You can Now Reach her through her Blog

The Report Has Been Filed By Nova Kambota From Dar es salaam on saturday 29,october,2011.


Nimepigiwa krosi hii na:
Nova Kambota

Read more...

Ili KIDOSHO awe mpiga GITAA mahiri, unahitajika UWEPO wa gitaaa!

Na ili KIJEBA awe MPISHI mahiri,...
... unahitajika UWEPO wa cha KUPIKA.
Swali:
  • Si UWEPO wa KITU ndio moja ya siri ya WATU kuwa MAHIRI wa hicho kidude?
  • SI huwezi kuwa NGULI wa hata KUSOMA kama chakusoma HAKUNA?

Ndio,...
... na kama hakuna GARI,...
... hata kazi ya UDEREVA ni alinacha TU!:-(


Swali:
  • AU?


Ndio,...
... na ukikutana na MAHIRI YULE wa kitu ``CHOCHOTE KILE´´,...
... kumbuka tu UMAHIRI wake wa CHOCHOTE KILE labda siri yake iko katika sababu ibebwayo na kwa sababu alipokuwepo huyo MAHIRI kulikuwa na UWEPO wa kile ``CHOCHOTE KILE´´,...
... ambacho kimewezesha MAHIRI kuwa MAHIRI wa hicho ``CHOCHOTE KILE´´.:-(

Ni wazo tu hili KAMANDA!
Nakutakia Jumamosi KIBONGE kwako MKUU!



Na hebu tena  moja kwa moja O'Yaba warudie-Haleluya



Zasha aendeleze kwa - I've been Good to you




Slave Band wakatizie denge kwa- Judgement day



Binti ya Lucky Dube yule Nkulee Dube naye aingilie kati kwa -Who Dem



Halafu huyuhuyu Nkulee Dube akiwa na One People Lucky Dube Band azime kwa ~ Give it to Me

Read more...

JUSTIN KALIKAWE -katika KUMBUKUMBU

Mwanamuziki Justin Kalikawe


Ndio,...
.....JUSTIN naweza kusema ni Mwanamuzi pekee wa Reggae za Kibongo ambaye aliyewahikukubalika sana mpaka na wasiopenda Reggae nyumbani Bongo Nyoso enzi hizo na nahisi hasa ni kutokana na aliyokuwa anaongelea.
R.I.P NGULI!
Ndio tupo tusiokusahau KAMANDA!


Hebu tujikumbushe,..
UGENINI






Kitendawili



Panapofuka





Noijuka




Credit ya picha KIBIRA FILMS

Read more...

Bethlehem Tilahun Alemu -MWANAMKE wa SHOKA kutoka ETHIOPIA!

>> Friday, October 28, 2011

Bethlehem Tilahun Alemu


Mwanamke huyu  kageuza biashara ya MAKATAMBUGA kuwa ya KIMATAIFA,...
... kitu ambacho unaweza kustukia ushoka wake kwa kuwa  unajua BIASHARA za viatu vya MCHAGA KAJITAHIDI,...
... kwetu BONGO jinsi  huishia ziishiako na hata watengeneza KATAMBUGA husikii wakikuza KATAMBUGA kuwa kitu kikubaliwacho DUNIANI!:-(


Habari zake zaidi msome HAPA


..au hata HUKU

....kama sio :http://solerebelsfootwear.blogspot.com/


Baadhi ya NDUDE zake ziendazo kwa BRAND :
SOLE REBELS





















Hebu tusikie alipoalikwa na Rais Bill Clinton alisema nini,...
... anaanza kwenye dakika kumi na tatu ya kideo hiki...


Watch live streaming video from cgi_breakoutseminar1 at livestream.com


Na sijui kwanini HEBU tupate tena-Tam Tam pour L'Ethiopie


Read more...

MIAKA FULANI nani angeamini ULAYA ingeombaomba msaada kwa CHINA ili kujiokoa KIUCHUMI?

Naamini iko siku AFRIKA ndio itakuwa kimbilio kiuokozi,...
... ingawa sasa hivi AFRIKA yaonekana ni MATATIZO tu!:-(

Swali la kizushi:
  • Hivi bado DEMOKRASIA na UBEPARI ndio njia moja sahihi kama MABEPARI na WENYE DEMOKRASIA mkombozi wao ni MKOMUNISTI na asiyehusudu DEMOKRASIA?





Hebu kwanza tuangalie hii,...
"Less Transparent" than China: EU Presidential Appointment Process


Halafu tucheki,...
China to Help Europe

Read more...

Jinsi ya KUBUSU Kiswahili!

ALAAH!

  • Kwani MABUSU si kama kuvaa chupi tu ambavyo yadaiwa ni vitu vya KUIGA?

Tukiachana na hilo,...
... kwa wapendao kuiga ya wenzetu,...
... labda DEKU

How To Be a Good Kisser



How To Kiss With Passion


How To Kiss Creatively




Eee BWANA eeh!

Tukiachana na BUSU
Ijumaa njema MDAU,...'
.... lakini ikibidi KULA DENDA MKUU!

Read more...

Karibu tule KONOKONO Mshikaji!

Watu kwa kujivunga BWANA,...
... ndio maana tunakufa na njaa,...
..... wakati PANYA , Konokono, MENDE ,nyoka... na minyoo ipo!

Hebu tujifunze kuhusu kula KONOKONO





Au tu hebu tujifunze kula  NYOKA


Read more...

Mengi ni RAHISI kwa MTAZAMAJI tu asiyehusika , na muhusika ndiye labda ajuaye ni kwanini pamoja na kujua mabaya ya UMALAYA haachi UMALAYA!

Na ingekuwa RAHISI,..
... labda kila MTU angekuwa kama WEWE!

Na ingekuwa RAHISI,...
... labda wote wangeaamini  UAMINICHO.

Na ingekuwa RAHISI ,...
.... labda  kila mtu angefanya,...
... na afanyacho kingefanywa ufikiriavyo ni RAHISI.

Swali:
  • Si ushastukia KUKOSOA WENGINE na MENGINE ni RAHISI na ndio maana karibu  kila mtazamaji MPIRA WA MIGUU hudai anajua KOCHA anakosea wapi na aliyepiga mpira nje ya goli  ni mzembe kwa kuwa ingekuwa  yeye  goli lingeingizwa kizimbani?

Ndio,...
... labda MENGI  ni MARAHISI kimtazamo tu,...
... hasa kwa wale WASIYOYAKABILI!:-(
Ni mtazamo tu huu  MHESHIMIWA!:-(


Ghafla hebu Do Not Call Morgan Freeman "A Man of God"!



Hebu Amadou na Mariam waanzishe kwa - Je pense a toi




Amadou na Mariam warudie pia - Djama




Au tu Lady Ponce abadili mchezo kwa - Les Hommes

Read more...

ANGALIZO KWA WATANZANIA WOTE, UTAPELI HUU UNAANZA KUOTA MIZIZI.

>> Thursday, October 27, 2011

KUNA TAARIFA ZA WANIGERIA AMBAO WAMEWEKA MASKANI MAENEO YA SINZA, SHUGHULI AMBAZO WANAFANYA WANAIGERIA HAWA BADO HAZIELEWEKI, NI TATA.
MUDA MWINGI HASA VIPINDI VYA JIONI WANAPENDA KUSHINDA KATIKA BAA KADHAA AMBAZO ZINA AMBAA AMBAA NA BARA BARA YA SHEKILANGO, KUANZIA MAENEO YA URAFIKI MPAKA BAMAGA.

HIVI KARIBUNI WATUMIAJI WENGI WA SIMU ZA KIGANJANI NA INTERNET WAMEKUWA WAKITUMIWA MESEJI MBALI MBALI ZA KUSHINDA ZAWADI FLANI, MFANO WATUMIAJI WA SIMU ZA KIGANJANI WAMEKUWA WAKIPATA MSG AMBAYO INAWAONYESHA WAMESHINDA ZAWADI KUTOKA KAMPUNI YA NOKIA, WAKATI UNAKUTA ULIOTUMIWA MSG HIYO MUDA HUO UNATUMIA SIMU YA MCHINA AMBAYO HAINA HATA JINA, NA WALE WATUMIAJI WA INTERNET WANAPATA EMAIL ZA KUTAKA WAINGIZE DETAIL ZAO ZA AKAUNTI ZAO ZA BENKI, HIYO EMAIL INAKUONYESHA KAMA VILE ULICHEZA BAHATI NASIBU FLANI.

WATANZANIA WOTE KAENI CHONJO, KAPINGAZ Blog BADO INAWAFUATILIA HAWA JAMAA ILI KUWEZA KUJUA UNDANI WAO, NA VILE VILE TUNAVIOMBA VYOMBO VYA USALAMA NAVYO VIWEZE KUJUA HAWA JAMAA WANAFANYA NINI, HOFU YETU INAWEZEKANA WAO NDIO WANAJIHUSISHA NA UTAPELI HUU AMBAO NAAMINI WATANZANIA WENGI BADO HAWAJAUJUA VIZURI WIZI HUU WA KUTUMIA MITANDAO.


Nimetumiwa HABARI hii na:
Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog

Read more...

VIPAJI MCHEZO WA NGUMI VINAINULIWA HIVI






Kocha mkongwe wa mchezo wa ngumi Habibu Kinyogoli akimwelekeza mtoto Salim Mponda (5) jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi ya klabu ya ngumi ya Amana Dar es salaam jana.





Nimetumiwa HABARI na PICHA na Nguli:
--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Read more...

Kwa kutumia AKILI , kunayadaiwayo ni busara USITUMIE akili!

 Kwa kutumia AKILI,...

.... yasemekana  BINADAMU atakabili tu yale ambayo kwa UBONGO wa KIBINADAMU yanawezekana kitu ambacho  yawezekana  ya KIMUNGU  jitihada za kuyatatua kwa akili za KIBINADAMU  sio  akili!:-(
Swali:
  • SI umestukia  kuna wadaio  kwa mfan maswala ya IMANI  sio ya  kujaji  WAAMINIO  kwa ni jinsi gani wanaaakili?
  • SI umeshastukia kuwa mengi yahusuyo MUNGU   ukitumia akili   ni rahisi kukwama au hata kuona hata MADINI  yaongozayo imani za  WALIMWENGU hayamekiSENSI ingawa yamejaa WAFUASI ujuao KIBINADAMU  wana bomba za miakili?

Na LABDA  mara nyingi tu  pia  na wala sio KIDOGO,...
... mtu huhitaji   mengine  kuacha  kimakusudi kutumia akili ,...
.... ili  KIAKILI  yasibishane na  ambayo  ni BUSRA na MSAADA kwa binadamu KUISHI maisha yake mafupi  kwa amani zaidi.

Swali ZAIDI:
  • SI lolote la KIJINGA kwa kutumia akili  waweza ligeuza  kuwa ni BUSARA ingawa kwa amani ya roho labda mtu angerizika kirahisi kwa atambuayo kuwa ni UJINGA yakiendelea kubakia UJINGA na hayana chembechembe za BUSARA?

Ndio,...
... ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(











Hebu tupitie tena Nigeria Chief Ebenezer Obey aanzishe upya kwa- Ota Mi Dehin Lehin Mi



Onyeka Onwenu na King Sunny Ade warudie- Wait for me


Halafu tu tena hapahapa Nigeria Onyeka Onwenu azime kwa kibao - Ekwe



Ila sijui kwanini hebu turudi Afrika Kusini ili Caiphus Semenya azime tena kwa- Angelina

Read more...

Kwa kujua MOJA kuhusu MTU kunawakoseshwao kujua MENGI kuhusu huyo MTU!

 Kuna MENGI kuhusu MTU,....
.... ambayo  hayaonekani tena kisa WATU wanajua MOJA kuhusu huyo MTU.

Swali:
  • Si  kunawasioona ujinga wa MTU  kisa wanajua MOJA kuhusu huyo MTU ambalo ni MZURI?
  • Na si wasioona MAZURI ya MTU  kisa wanajua moja kuhusu huyo MTU  kuwa ni KIBAKA?

Ndio,...
.... na kuna wasioona UJINGA wa MTU  kwa kuona cheti kimoja tu chake kionechasho  kuna kipengele katika ya WASOMI huyo ni PROFESA kama tu wasahauo  kuona mengine KATIKA MTU kisa kimtazamo wao moja walilostukia ni kuwa MTU  huyo ni MLOKOLE na kwa hilo hawastukii tena  kuwa  huyo ni MAMA MBAYA  kwa wanawe kisa tu huyo tayari anaoanishwa na MAZURI.

Swali:
  • SI unajua labda MOJA ujualo kuhusu MTU labda ni hilo tu MOJA na kwa kujua  moja lifanyalo MTU ni maarufu kwa kucheza mpira  labda hakumaanishi huyo MCHEZA MPIRA ki-BEKHAM  yake mengine  yana umahiri kama hayo ya mpira?

Ndio,...
... labda MOJA mtu ajualo la MUUZA SURA kimodo,.......
....linapofua kustukiwa  mengine ya MUUZA sura  kiulimbwende.

Swali:
  • AU?
  • Na si unakumbuka KUTOKUJUA KITU kuhusu MTU hata kama ni huyo MCHUMBA WAKO  yawezekana ndio kifanyacho WAMPENDA -kitu kifanyacho KUTOKUJUA kuwa ni kitu kizuri pia?
  • Kwani ni mangapi ujuayo yafanyayo uridhike na MTU?

Ndio,...
.... kuna  wenye KUKOSA KUJUA MENGI  kuhusu MTU,...
.. kwa sababu katika MAMILIONI yafanyayo huyo ni MTU moja tu WAJUALO KUHUSU MTU tayari linauwezo kwa wengi  kuwafanya wajisikie ni MAPROFESA wa MASWALA yote kuhusu huyo MTU.:-(

Swali:
  • Unabisha?



Ndio,..
....na kituliza kujua LILE usilojua kuhusu KITU,...
.... mara nyingi ni lile ujualo tayari na likakutuliza UDADISIwa KITU.:-(

NI wazo tu hili MHESHIMIWA!

Turudi Afrika Kusini ili Caiphus Semenya aanzishe kwa - Dial Your Number



Hapa hapa UGANDA Afrigo Band warudie- Tusiimye Nyo


Hawahawa Afrigo Band warudie tena - Sirina Reverse



Halafu hapahapa UGANDA hebu Rudeboy Devoh azime kwa- Kampala

Read more...

Ukiremba SWALI unaweza kupata JIBU ulitakalo!

NDIO,...
....LABDA pia,...
.... kwa kurembesha SWALI,...
.... .... maana yake MTU anajua atakalo JIBU

Swali:

  • Na si labda UMESHASTUKIA hata katika KURA ZA MAONI a.k.a OPINION POLL mahitimisho mara nyingi ni DANGANYIFU kwa kuwa maswali waulizwayo WATU yameundwa kutaka JIBU lioane na atakacho kiwe ndio JIBU mtafiti adaiye anataka kujua WATU wanawaza nini katika hiyo OPINION POLL aka KURA YA MAONI?

Ndio,...
....labda CCM , CUF na CHADEMA wanaweza kufagiliwa SAWASAWA katika KURA za MAONI ya WATU WALEWALE WATANZANIA ukigeuza tu MASWALI!:-(

Ni mtazamo kiwazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu Jamhuri Jazz Band warudie-Oh Masikini


Au tu tena Jamhuri Jazz Band warudie na- Shingo La Upanga



Read more...

MPIGIE GEOFREY MWAKIBETE KURA YA MPIGA PICHA BORA WA MITINDO.

Geofrey Mwakibete


Wapenzi wadau na wasomaji wa napenda kuwafahamisha kuwa Geofrey Mwakibete wa MO BLOG  ambaye amebahatika kuchaguliwa kuwa miongoni mwa washiriki wa shindano la SWAHILI FASHION WEEK AWARDS  katika kundi la Wapiga picha bora wa Mitindo.

Bila nyinyi asingefanikiwa kupata nafasi hii hivyo tunaomba tuendelee kumpa sapoti na hamasa kwa kumpigia kura GEOFREY MWAKIBETE kupitia mtandao

Asanteni kwa Ushirikiano wenu.

Operation Manager.
MO BLOG.

Regards,
--
Zainul A. Mzige,
Operation Manager,
MO BLOG,

Read more...

NAFASI ZA MASOMO AWAMU YA TATU ZATANGAZWA KATIKA BAADHI YA VYUO TANZANIA MWAKA WA MASOMO 2011/2012



Kwanza kabisa Tunapenda kuchukuwa nafasi hii kuwasalimu watu wote Wakubwa Shikamoo na wadogo Mambo vipi!


Umoja wa Matukio na wanavyuo Tanzania (www.tzwanavyuo.blogspot.com) unayo furaha kuwaletea habari njema wale wanafunzi wote ambao walikosa nafasi za kujiunga na vyuo katika mchakato mzima wa awamu ya kwanza na awamu ya pili. Lakini sasa baadhi ya vyuo vikuu vikiwemo Teofilo Kisanji University, Stefano Moshi Memorial University College,St. Augustine University of Tanzania, Ruaha University, National Institute of Transport, Iringa University College, Institute of Finance Management, Eskerforde Tanga University, University of Dodoma na Ardhi University vimetangaza baadhi ya nafasi hizo.

Nafasi zimeelezewa vema na pia mwaweza tazama wapi unataka kujiunga. Fungua sasa na ufuate maelekezo na kutuma maombi yako bila kuchelewa . Tunawatakia mafanikio mema wale wote ambao wataenda kujiunga.

Mwisho tunapenda kuwakumbusha kwamba ule mtandao wenu wa wanavyuo bado unakungoja wewe ambae haujajiunga
 


Nyote mnakaribishwa. na kama mna matukio mbali mbali ya vyuoni kwa wanavyuo wote watanzania waliopo nje na Ndani ya Tanzania na Watumishi wa vyuo kama mna matangazo ama matukio mnataka kuyaposti pia tutumieni kupitia twanavyuo@live.com

Kutazama nafasi mpya za masomo bofya hapa:

Kwa niaba ya Wenzetu ni sisi,
Matukio na wanavyuo Crew

Read more...

Sherehe za uzinduzi wa kituo cha uwekezaji(TCI) jijini Mbeya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu akikata utepe kuzindua ofisi ya kituo cha uwekezaji (TCI) nyanda za juu kusini mjini Mbeya.








 Jengo la TCI Mkoani Mbeya

Akizindua ofisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Mbeya, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu alisema ofisi hiyo ni muhimu katika kusaidia wajasiriamali na wawekezaji wa mikoa ya Ruvuma, Iringa Rukwa na Mbeya kuitumia kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali ya uwekezaji.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIC, Balozi Elly Mtango.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Raymond Mbilinyi alisema Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.



Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimkaribisha waziri Mary Nagu alisema mkoa wake unazo fursa nyingi zikiwemo za kilimo katika Bonde la Mbarali na maeneo mengine, ufugaji, uvuvi katika ziwa Nyasa, utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo na uchimbaji wa makaa ya mawe katika eneo la Kiwira.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa kituo cha uwekezaji jijini Mbeya kutoka Kushoto Mbele ni Mrs Kadyanji na anaefuatia ni Mrs. Yunge na wajasilia mali wengine.




Picha zote na Mbeya yetu Blog


Na nimetumiwa HABARI na PICHA na:
WADAU wa MBEYA YETU Blog.

Read more...

Ariel SHARON yule aliyewahikuwa Waziri Mkuu ISRAEL bado yuko HAI - na yasemekana WAYAHUDI ndio wawezao kufufua WAFU kama kuna awezaye!

>> Wednesday, October 26, 2011

26 February 1928-.............

Swali:
  • SI unakumbuka ni MIAKA kibao imepita tokea Waziri Mkuu Ariel SHARON awe kwenye ``COMA ´´ na ni mashine tu zifanyazo anapumua na kutoitwa MAREHEMU kiufu?
Ndio,...
... tokea  Januari 4 mwaka  2006 jamaa hajawahi kupepesa UKOPE,..
... na yuko HAI kimtazamo wa WAJANJA.
  
Na unaweza kujikumbusha NDUDE hii,...
...hata kwa kubofya HAPA.
.
TUNAKUMBUSHANA tu KITU MKUU!




Hebu turudi ARUSHA tena kupata SINDIMBA kwechukwechu ,SINDIMBA ngoma ya KIMAKONDE kwa msaada wa MS Ngoma Troupe



Arusha ALLSTARS waingilie kati kwa ndude-ARUSHA





Au tu kiaina TITI ajaribukubadili mchezo mzima  kwa kuingizia ndude- Tayumako

Read more...

Injinia FRANCO CHANDE

DO YOU KNOW IT ENGINEER FRANCO CHANDE?

IT Engineer Franco Chande.


Franco Chande is among of IT Engineer in Tanzania, had an experience in computer Maintenance( Assembling and Installation), Computer Networking, (LAN/WLAN) and Configuration of any IT devices (Servers, Routers, Modems, etc.)

According of the shortage of IT Expert in Tanzania, Franco Chande advice every young boys and Girls to join in this field to help our Nation and to make sure we develop our Country in this Industry, which is running the World.



Nimetumiwa HABARI ya jamaa kama ilivyo na:
Mdau  Elman Kimath

Read more...

FRANCIS MIYAYUSHO na MBWANA MATUMLA watambiana , MPAMBANO JUMAPILI







Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) na Mbwana Matumla wakitunishiana misuri mbele ya waandishi wa habari wakati wa utambulisho wao wa mpambano wa kugombea ubingwa wa UBO jumapili hii katikati ni mratibu wa mpambano huo Mohamedi Bawaziri .





Mratibu wa mpambano wa ngumi Mohamedi Bawaziri  katikati akiwa na mkanda wa ubingwa utakaogombaniwa na mabondia Fadhili Majia (kushoto) na Juma Fundi siku ya jumapili.








Nimetumiwa PICHA na HABARI na:
--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP